Bila Neymar Jr, PSG anamtoa Real Madrid mapema tu!!

Ha ha ha ha ha kweli mkuu,jana eti Shafih Dauda nae alisema ana imani Psg wanawatoa Madrid,kweli?
Huyo mpiga porojo jana nilimusikiliza, yeye na genge lake hua wanaongozwa na mahaba kuliko facts(mfano ukiangalia kwa mchezaji mmoja utaona Madrid ni bora kuliko Psg plus uzoefu na team player) na hata Madrid ifanye vizuri vipi coverage yake hua ni ndogo kwenye kipindi chao.

BTW, Madrid ndio timu kubwa ulaya kihistoria, acha waendelee na porojo.
 
Usiku wa game ya kwanza ya Madrid na Psg Shafih alisema kuwa Psg ni timu kubwa Ulaya,Edgar akamuuliza kivipi akamjibu ni kwakuwa imefanya usajili mkubwa na inawachezaji wazuri,Edgar akamwambia Psg bado si timu kubwa na itakuwa kubwa kama itazifunga timu kubwa kama Madrid,Barcelona,B.Munich.
Edgar katika uchambuzi wake alibashiri Madrid itashinda na ndicho kilichotokea.
Psg imepigwa nje na ndani,ona sasa Psg wanavyoonekana hovyo kabisa kwa usajili mkubwa halafu wanatolewa kirahisi mnoo hata robo hawajika... what a shame?
 
Naomba niongee hiki. Hizi timu mbili Madrid na Barcelona pamoja na kuwa zinacheza vizuri na zina wachezaji wazuri lakini amini nawaambieni marefa wanazibeba sana. Mara zote nimekua nikifuatilia mechi za hatua ya mtoano pindi hizi timu zinapokua zinashiriki.

Kumekua na influence kubwa kwa waamuzi na viongozi wa shirikisho la soka ulaya juu ya hizi timu mbili ndio maana tunashuhudia maamuzi mabovu kabisa yanayofanyika mara kwa mara.

Mfano mechi ya jana kadi nyekundu ya verati sikuielewa mpaka sasa hivi, game ya kwanza rabioti alipewa kadi ya njano pasipo kumgusa mtu. Msimu uliopita hatua ya robo kama sio nusu baina ya Madrid na buyernmunich Arturo Vidal alipewa kadi nyekundu ya ajabu ikiwa buyernmunich tayari anaongoza. Tukiachana na hilo kila mtu alishuhudia game ya pili ya 16 bora baina ya psg na Barcelona hakuna haja ya kuelezea nini hasa kilitokea. Hizi timu kinacho nifanya nizichukie ni huku kubebwa kwao. Hiki kitu UEFA hawanabudi kukiangalia kwa jicho la tatu.
 
Kuhusu Verratti nadhani kuna nidhamu ya kumfuata referee popote pale duniani na hiki ndicho alichokosa Marko huku akijua wazi kuwa ana kadi
 
Kuhusu Verratti nadhani kuna nidhamu ya kumfuata referee popote pale duniani na hiki ndicho alichokosa Marko huku akijua wazi kuwa ana kadi
Sio kutoa kadi kirahisi namna hiyo kwenye mechi kubwa yenye pressure kubwa namna ile. Bado kuna tatizo sana la waamuzi pindi wanapochezesha game za hizi timu.
 
Barcelona ndio hubebwa mkuu na sio Madrid,sio Uefa tu angalia hata La Liga wakicheza hasa na Madrid.
 
Mleta mada baada ya Madrid kum-prove wrong katukimbia.
 
Barcelona ndio hubebwa mkuu na sio Madrid,sio Uefa tu angalia hata La Liga wakicheza hasa na Madrid.
Hao wote wanabebwa hilo linajulikana na watu wamelalamikia sana. Wanasahau mpira ni mchezo watu walio wekeza fedha zao nyingi sana alafu maamuzi ya kijinga yanaweza kuicost timu kwa kiasi kikubwa sana. Nenda kamsikilize raisi wa PSG alichoongea mara baada ya game yao ya kwanza kuisha na Madrid utanielewa ninachoingea.
 
Kama raisi wa Psg kasema wameonewa ndio una-justify? Yeye ni nani mpaka kila anachosema kiwe sahihi?
Kila anaepoteza nafasi hutafuta maneno ya kujifariji......alichokisema Wengar baada ya kupigwa 3-0 na Man city kwenye fainali kombe la Carabao pia alikuwa sahihi?
 
Nimekumbia nenda kamsikilize alichokiongea. Ngoja nikusaidie kidogo kumnukuu kama nitakua nimekosea wajuzi wa mambo watanitaarifu. "Siwezi kusema tumefungwa kwa sababu ya marefa la hasha ila mara zote maamuzi yao yamekua yakituumiza na kuwapa nafuu wapinzani wetu. Mwaka jana kilitokea kitu kama hichi baina yetu na Barcelona na leo kuna baadhi ya kadi zilikua sio za ulazima. Uefa hawanabudi kuliangalia hili ili waendelee kulinda hadhi ya kombe hili" haya maneno aliyaongea game ya kwanza. Sidhani kama kuna viashiria vyovyote vya kujitetea ila amejaribu kuongelea hali halisi.
 
Nakiri kuwa Barca ndio wanaobebwa,na hii ndio ilipelekea maamuzi ya ajabu na Psg ikatolewa kwa aibu msimu uliopita.
Rais hapo alikuwa sahihi kufuatia matokeo ya nyuma lakini bahati mbaya Madrid huwa haipendelewi mkuu.
Je Psg jana wametolewa kwa kuonewa ama uwezo wao tu ndio mdogo?
 
Mleta uzi umeongea facts kabisa. Mimi nishasema kile kitoto cha mama hakifai kabisa. I'm so happy kutokuwepo mechi muhimu ya leo.

So nna matumaini makubwa sana na Fundi machachari ANGEL DI MARIA, ila sio yule mayai

Psg 2-0 Madrid
Haahahahaha,Mpaka kalitolewa nje hakuna kalichokifanya.Nyie wanazi wa Argentina mna shida sana.
Ni chizi tu anaweza kumfananisha Neymar na De Maria.Nyie tunajua ni chuki na wivu wa kike tu unawasumbua.Sasa umejione mwenyewe jana kwamba PSG Bila Neymar ni hakuna,Hata mechi za League 1.Mechi 4 Neymar hakuwepo wameshinda 1 tu tena kwa tabu wakiwa na hicho ki De Maria kinakimbia bila akili.
 
Yaani dunia imempa thamani ya billion 300+ wwe mchambuzi uchwara utoke kusikojulikana na uhasama wako na Neymar eti hajui Mpira mweeee
 
Mkuu Mimi huwa nawaangalia sana Hawa wachambuzi uchwara eti Neymar wa kawaida wakati kila kura zikipigwa yeye ni mchezaji nmba 3 kwa ubora halafu mshabiki uchwara anayehifunza kuangalia Mpira Jana anakuambia ni wakaida,Perez mwenyewe ametoa macho hapo bado mmamndenyi mmoja anakuambia ni overrate player daa,Mimi siipendi brazili wala sijawahi ishangilia PSG wala Barcelona,ila tukija kwenye ukweli tuongee ukweli Neymar ni nguzo ya PSG
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…