Sinoni
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 6,581
- 11,572
Nani amekudanganya ili uwe bora lazima uhame club moja kwenda nyingine, je hujui kwamba kuna wale wanaohama na wengine kubaki kwa sababu wanazozijua wao?naona umejifanya haujaelewa nilichokuwa namaanisha........
sister hapa chini ninakuwekea sababu kadhaa zinazowafanya wachezaji kuhama na wengine kuamua kubakia kwenye timu moja . . ..
Maslahi / mshahara: Cr7 na Bale ni mfano tosha wa wachezaji waliohama kwa kutamanishwa fedha.
Uwezo; van Persie aliondoka Man Utd kutokana na uwezo wake kushuka ndani ya uwanja na hicho hicho ndicho kilichowakumba Fabregas & A. Song pale BARCELONA.
Nidhamu: Hii imewakumba wachezaji Wengi aina ya Ballotel , utukutu na ulevi umewafanya washindwe kudumu katika timu moja.
Mapenzi: kuna wachezaji wanahama kutokana na upenzi, mfano Mzuri ni Lewandowski kutoka Dortmund kwenda Fc Bayern, alihama kutokana na kuwa na mapenzi na the Bavarians..