Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Ndugu zangu, Kuna mambo ya ajabu yanafanyika kwenye ajira za vibarua katika viwanda vya METL chini ya MO DEWJI. Kuna wanaojiita supervisors wa viwanda na wahusika wa kuajiri wafanyakazi na vibarua wamekuwa na utaratibu kuchukua rushwa ya Tsh. 50,000 hadi 100,000 kwa kila anayetaka kazi.
Kuna watu wengi wanajikuta wanaliwa pesa zao na kazi hawapati, wengine wanaingia kazini kwa ahadi ya malipo ya Tsh. 7000 kwa siku lakini zamu zao za kuingia kazi hazina mtiririko mzuri kwasababu wasimamizi hao wameshapokea pesa za watu wengi sana kwahiyo wanachokifanya ni kupanga zamu kutegemea na idadi ya pesa za watu walizochukua na sio idadi ya watu.
Sidhani kama MO ana taarifa kuhusu hili. Taasisi za Rushwa zifanyie kazi suala hili haraka kwasababu watu wengi wanaumizwa pale kila siku wanachukua hizo pesa kwa waombaji wapya.