Ameandika mambo mazito ambayo akili zako huwezi kuchanganua.
Ukisikia Rwanda imeendelea ujue Congo imepata tabu sana usidhani Rwanda wajinga.
Kuendelea kwa nchi kunahitaji ujasusi wa hali ya juu, mambo sio marahisi tu ulale uamke ukusanye kodi nchi iwe tajiri, kuendelea ni zaidi ya kukusanya kodi na kukopa.
Hujiulizi miaka nenda rudi tunakopa mbona mbona hatuendelei? Mbona tunakusanya kodi mbona hatuendelei kivile?
Hizo China, USA zote zimefanya ujasusi kwa nchi zingine ndo zikafika hapo zilipo
Uingereza imefika pale ilipo kwa mishe mishe nyingi mpaka Mmarekani alitawaliwa na Uingereza, kwahiyo ujue nchi kuwa tajiri sio jambo la utani utani.
Ukisikia Russia imedukua taarifa za USA yote hiyo ni michakato ya nchi kusaka utajiri