Pre GE2025 Bila Uwepo wa CCM Madarakani Nchi ingekuwa Imesambaratika na Kugawanyika vipande vipande

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndugu zangu Watanzania,

Nikitizama na kufuatilia namna vyama vya upinzani vinavyoendeshwa ,vinavyofanya maamuzi yake,mfumo wa uongozi na n

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Acha ushamba dogo! Kenya, Zambia. Malawi nk. Kuna ccm? mbona hazijasambaratika?
 
Acha ushamba dogo! Kenya, Zambia. Malawi nk. Kuna ccm? mbona hazijasambaratika?
Kwani hoja yangu ni wapi ilipozungumzia habari za kenya au Zambia? CCM Ni Chama kiongozi na ndio maana vyama mbalimbali kutoka kila pembe ya Afrika huja kujifunza hapa nchini .
 
Mkuu Lukas acha kudanganya watu, nchi zote za Afrika zilipata uhuru zikiwa na vyama vingi vya siasa.

Na nchi nyingi sasa vyama vya siasa vikongwe vimeondolewa madarakani na hakuna nchi iliyosambaratika.

Tupe mfano wa nchi moja tu iliyosambaratika kwa sababu chama kikongwe kiling'olewa madarakani.

Kwa mfano Zambia, Malawi na kenya ni nchi jirani ambapo wamebadilisha vyama vya siasa madarakani mara kadhaa zimesambaratika???
 
Kama visingekuwepo vyombo vya ulinzi na usalama ndio nchi ingesambaratika sio CCM. !
Hata wao wanalindwa na vyombo hivyo kama vile wanavyolindwa watanzania wooooteee !!
 
Hakuna chama chenye uwezo wala nguvu wala uwezo wala ubavu wa kuweza kushindana na CCM katika sanduku la kura. Hii ni kutokana na ubora wa sera na ajenda zake zenye kugusa maisha ya watu wa rika na makundi yote.
Mkuu kama ndio hivyo ilikuwaje kura za wizi zikazagaa kwenye uchaguzi wa 2020?? Ilikuwaje wasimamizi wa upinzani wakawa wanazuiliwa kusimamia???
 
Mkuu kama ndio hivyo ilikuwaje kura za wizi zikazagaa kwenye uchaguzi wa 2020?? Ilikuwaje wasimamizi wa upinzani wakawa wanazuiliwa kusimamia???
Mimi niliko simamia uchaguzi hakuna wakala wa upinzani aliyezuiliwa.
 
Kama visingekuwepo vyombo vya ulinzi na usalama ndio nchi ingesambaratika sio CCM. !
Hata wao wanalindwa na vyombo hivyo kama vile wanavyolindwa watanzania wooooteee !!
Vyombo vya ulinzi na usalama vinaweza kuwepo na mipaka ikawa salama na kusiwe na tishio lolote lile la uvamizi lakini ndani ya nchi Kukawa hakuna Taifa zaidi ya mpasuko mkubwa sana.ambapo kuna kuwa hakuna umoja, mshikamano,upendo na ushirikiano zaidi ya kutamalaki kwa ubaguzi kwa misingi ya Udini, ukabila, ukanda,ujinsia pamoja na chuki katika mioyo ya watu. Kwa hiyo hata maendeleo hayawezi kuwepo kwa kuwa Taifa halipo pamoja na wala watu hawana umoja kwenye jambo lolote lile.
 
Hadi chakula nilimpa wakala wa CHADEMA kwa kuwa wao chakula chao kilichelewa saba kuletwa. Na nilikuwa msimamizi mkuu wa kituo cha kupigia kura. Na hadi leo yule jamaa wakala wa CHADEMA huwa ananishangaa na kunipongeza sana kwa moyo wangu wa upendo na utu usio na ubaguzi wala chuki.
 
βœοΈπŸ“πŸ‘πŸ‘ŒπŸ‘πŸ€πŸ’πŸ›‘οΈ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…