PreGE2025 Bila VPN hauwezi kuingia X (Twitter) Tanzania. Vipi huko mnaotumia Facebook na Instagram?

PreGE2025 Bila VPN hauwezi kuingia X (Twitter) Tanzania. Vipi huko mnaotumia Facebook na Instagram?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Angalia na comments za watu walivyokuwa wakimjibu huyo jamaa kwakutoelewa alichoongea Gwajiboy. Hapa situmii VPN wala nini mkuu Elungata
Screenshot_20250524_223254_Samsung Internet.jpg
 
I remember that time hata mimi nililazimika kutumia VPN. Mimi natumia Tigo by now na mpaka sasa na surf fresh huko twitani.
Voda wahuni hawa bila VPN utaishia kuona ulipoishia tu na picha hazifunguki sema VPN imesaidia hapa
 
Haina haja ya kuswitch line kama VPN inafanya kazi fresh. Hapo ni bundle lako tu mkuu.
Ndio hivyo sema wanachofanya government ni uswahili kabisa social networks haziwezi kuwa threat sema tu labda wanafanya mambo yao ya giza ndio maana wanaopt kufungia mitandao
 
Loh, ndiyo najua now after kuingia JF.
Since yesterday nimeshindwa ingia X, nikadhani ni unstable network. Sasa nipo Hotelini natumia WiFi napo patupu kwa laptop.
 
Ndio hivyo sema wanachofanya government ni uswahili kabisa social networks haziwezi kuwa threat sema tu labda wanafanya mambo yao ya giza ndio maana wanaopt kufungia mitandao
Ni kiongozi asiye shupavu na aliyepikika kisiasa haswa kuogopwa critics kwenye social media mpaka kufikia hatua ya kuamuru kuzima Internet au a certain social platform kwasababu anakaangwa huko. Ukiona kiongozi anashindwa hata kutega muda wa kuongea na wananchi wake hata kwa mwezi mara moja na kuwapa nafasi wananchi wake wamuulize maswali naye akayatolea ufafanuzi zaidi ya mipasho pale jambo linapokuja juu kwenye mitandao, huyo si kiongozi shupavu bali ni mtawala legelege.
Mitandao husaidia kujua wapi umekosea na kurekebisha, wapi unasifiwa kiukweli na wananchi na wapi unakandiwa. Yote haya yahitaji kuwa mwanasiasa mkomavu haswa na si wakupewa pewa nafasi mpaka kufikia level flani bila kujua what it takes to be admirable by the whole society.
 
Ndio hivyo sema wanachofanya government ni uswahili kabisa social networks haziwezi kuwa threat sema tu labda wanafanya mambo yao ya giza ndio maana wanaopt kufungia mitandao
Ni threat,tuacheni unafiki,inajulikana wazi kuwa internet ilikuwa ni project ya Pentagon Tangu mwanzo,,kabla ya internet nchi za magharibi zilijitahidi kuweka idhaa za redio mfano,BBC Swahili,VOA Swahili, Deutsch well,BBC Persian,etc,,
Media zinaplay part kubwa Sana katika ku influence agenda mbalimbali zikiwemo za kisiasa,
Social media Ina phaseout rule ambayo redio na magazeti yalitumika kuinfluence agenda,,
Kiufupi social media unaweza kutumika kwa watu kuji organise kufanya machafuko Kama yake ya Arab spring.

Kwa ushauri wangu wafungie x,Facebook,Instagram. Yaani ibaki JF tu🤗😂
 
Loh, ndiyo najua now after kuingia JF.
Since yesterday nimeshindwa ingia X, nikadhani ni unstable network. Sasa nipo Hotelini natumia WiFi napo patupu kwa laptop.
Ni wakati mwafaka wa jf kurudisha members wake,wengi tulitorokea x,,saa hizi hatuna ujanja inabidi turudi jf🤗🙆
 
Wakuu nauliza tu maana ni muda wa karibu siku 5 Sasa bila kutumia VPN huwezi kuacess maudhui ya mtandao huu nchini Tanzania. Shida ni Post za mange kudisclosure taarifa za bosi wa Polisi ama shida ni Nini?
 
Wanatest mitambo maana uchaguzi wao unakaribia. Wanajua akili nyingi ziko kule X na dawa ni kuuzima maana hawawezi kujibu hoja zao. Ila VPN bado inatuweka X'ni
 
Back
Top Bottom