PreGE2025 Bila VPN hauwezi kuingia X (Twitter) Tanzania. Vipi huko mnaotumia Facebook na Instagram?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Watakuwa wajinga maana documents za Mange inaonekana amevujisha mtu wa ndani huko huko kwa kuchukua video na picha. Na amevujisha kwakuwa anaonekana hajapendezwa na huo wizi.
Watu wameshawachoka. Sasa hizo documents zitasambazwa facebook na kwenye mitandao mingine yenye watu wengi zaidi .
Halafu zile documents zingekuwa fake, wangeshakanusha. Wameumbuliwa vibaya sana.

All in all, huu uamuzi unazidi kuwafanya watu wengi zaidi waichukie serikali.

Mshauri wa hii serikali sijui ni mtu gani huyo!!!
 
Ila Watanzania ni watu wa ajabu Ukisoma majibu ya watu unagundua hata kujatibu tu kuifungua x hakuna ila wamejibu kukosoa.


Any way sina vpn na inafanya kazi kutwa nzima yanleo
 
Wanajisumbua tu hata China huko X, Facebook , WhatsApp ziko banned ila watu wanatumia.

Zama hizi hakuna namna utazuia hoja au usambaaji wa taarifa labda waue watu wote wabaki wafanyakazi wa ikulu waanze kuijenga upya Tanzania kinyume na hapo hawajazuia chochote.

Hapo ndio kwanza wameipa X umaarufu watu watadownload kwa wingi maana watajua huko ndio kuna taarifa "unfiltered" ambazo huwezi kuzipata mtandao mwingine wowote.

X ilijipatia umaarufu enzi zile Kigogo anawasumbua na sasa watu by nature ni kitu unachokikataza ndio hukijaribu kwa wingi waone kwanini kinazuiwa.
 
Bila VPN kibongobongo hutoboi, au uko nje ya Tz?​
Hapana boss nipo ndani ila si mbali na mpakani km kama 60/70 hivi labda ndo sababu, ngoja ntatest nikianza safari maana mda si mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…