Bila Waajemi kuingilia kati, leo hii Syria, Lebanon, Palestina yote na sehemu kubwa ya Misri zingekuwa zimechukuliwa kwa nguvu na Israel

Ya ni kweli, hayo makundi yote ya kina Osama na wenzake yametengenezwa kupigania masilahi ya waliowatuma. Ndio maana utakuta makundi yote yamejikita katika maeneo yenye utajiri wa mafuta.

Kamwe hauwezi kusikia Islamic state au alkaida wamevamia Israel au kuwaunga mkono Hamas. Wao wako busy kupambana katika zile nchi zilizokuwa target kuvamiwa na Israel ili waanze kuzichosha mapema kabla ya uvamizi kamili. Bahati nzuri wamedhibitiwa vikali na waajemi kupitia vijana wao waliopo katika nchi hizo.
 
Waafrika wengi ni wapumbavu, wanaamini story za kuandikwa au kuhadithiwa, kuliko zile za kujinea wenyewe na macho.

Ndio maana nchi nyingine Afrika zimetawaliwa mpaka na nchi chovu na dhoofu kama Ureno. Pia ndomaana kuna mfalme alitoa ardhi yake na baadhi ya jeshi lake kuwakabidhi wazungu baada ya wazungu hao kumpa mfalme huyo kioo cha kujiangalia kila siku asubuhi akiamka.

Yani mfalme mzima anawapa watu ardhi yenye utajiri wa madini na rutuba ya kutosha kwa sababu ya kuletewa kioo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Tatizo lako hauongei kwa kufikiri unaongozwa na chuki za Madrasa tu. Kama umewah kufika Israel utagundua vitu ni tofauti na story mnazolishwa huko Madrasa chief. Israel inao Ethiopia Jews wa kutosha tena mpaka jeshin. Wapo Arabs Jews mpaka jeshin wapo Iranian Jews mpaka jeshin wapo Jews wa kihind Moroccan uzungun na hata Yemenis. Wapo mpaka majews wa kiafghanistan. Hao Jews unaoona walioletwa hapo kutoka uzungun ndio wale waliokuwa wanauawa huko walikotoka kwasababu ya nasaba zao na jealous za mafanikio yao. So Jews wa maeneo mengine hawakuwah kuuwawa zama za karibun ndio maana hawakuwa na haja kurud kwao. Hiyo kuuwawa ni kawaida Mzee haimaanisha sio binadamu wanauwawa na wenyew wanaua. Wametawaliwa na kuwa free kwa vipind tofauti. Na sasa wanatawala itakuja kipind nao watatawaliwa. Ni kawaida sana. Kabla hujazungumzia misaada wanayopata zungumzia huko misaada inakotoka ni akina nani wanasimamia hizo taasisi za misaada. Wenzio wamewekeza kwenye maeneo nyeti nchi za kiume.
 
Yeye leo akiambiwa na wahadzabe awapishe katika shamba na nyumba aliyojenga atakubali?

Maana historia iliyoandikwa na wazungu inatambua kuwa wahadzabe ndio wenyeji halisi wa Tanganyika ambayo ndio Tanzania ya leo. Historia hiyo inasema makabila mengine ya kibantu yaliobaki yote likiweko kabila lake yalitokea nchini Cameroon, Centre Africa na Congo.

Sasa wahadzabe wakimletea kitabu hicho cha historia sijui atakubali na yeye kichwa kichwa kuwaachia wahadzabe hao ardhi na nyumba yake!
 
Sunday's school zimewaharibu mno kifikra. Ndomaana mnaaminishwa zaidi kupitia vitabu ambavyo hata hao Jews wenyewe hawavikubali. Mahaba ya Sunday's school yameshindwa kukufanya uone kile kilichowatokea Jews wa kiethiopia na waafrika wengine waliotaka kuonesha kuwa wao ni wa jews kama wewe.

Watu wanaangalia uhalisia wa nani aliekutwa katika ardhi husika. Hayo mambo ya biblia, msahafu na vitabu vingine hayawezi kuamua kuhusu swala la mipaka ya nchi. Ndomaana hata Umoja wa mataifa ambao ndani yake kuna hizo nchi zinazoisaidia Israel hawatumii biblia wala msahafu kujua mipaka ya nchi, bali wanatumia fact ya nani aliepo pale miaka na miaka kabla ya 1948. Hivyo vitabu viliandikwa miaka fulani tu iliyopita, kabla ya babu yako au babu yangu kuzaliwa. Hivyo hakuna mtu mwenye uhakika wa Mia kwa Mia kuwa yalioandikwa humo yana ukweli.

Kama wayahudi wenyewe wanapingana na maandiko mengi yaliopo katika biblia kwa kuyaona kuwa ni porojo tupu zilizotengenezwa na wazungu, sasa wewe mmatumbi wa vigwaza ni nani mpaka ukimbilie ku support wazungu wanaochukua nchi ya watu kwa kisingizio cha kuandikwa kwenye biblia?
 
Acha makasiriko ya madrasa sheikh. Naomba nikuize swali. Hiv unajua misri na nchi zote zao northern Africa zilikuwa ni za waafrica waarabu wakawaua wakachukua nchi zao. Unajua mafarao walikuwa ni Africa? Turud kwenye mada. Neno biblia lina maana ya vitabu sio kitabu. Ukichukua Jews holy book inaelezea nchi yao na mipaka yao. Hata hicho kitabu cha mudy kinajua na kutambua Jews walikuwepo na nchi yao. Nachokusaidia ni kuwa kama Jews walikuwepo hata wakat wa ottoman impaya basi. Hapo ndio kwao shida iko wapi. Wapo kwao na wamejitengenezea nchi. Hiv wale wazungu wa South Africa ni wenyeji au wagen au Australia au America
 
Bado uliyoandika yanaonesha upeo mdogo wa kufikiri kichwani kwako. Yani upeo mdogo wa kuamini kuwa kila anaepingana na Israel ni muislam. Upeo wako mdogo unashindwa kufahamu kuwa serikali ya Afrika Kusini iliyoifungulia Israel kesi ya mauaji ya kimbali inaongozwa na wakristo 99%.

Upeo wako mdogo umekufanya ushindwe kujua kwamba kuna watu kama kina hayati Desmond Tutu walikuwa wanaijua bibla zaidi ya vile uijuavyo wewe myahudi wa kimatumbi, lakini kwa sababu ya haki na uhalisia wa kile kinachoendelea Palestina aliamua kusimama upande wa wapalestina na kuweka mihemko yake ya kidini pembeni. Hata huko Marekani kuna maseneta wazungu tena wakristo ambao hawapendezewi na kile kinachoendelea na Israel huko Palestina. Sasa hayo mambo ya dini katika swala nyeti kama hili yanatoka wapi wakati Palestina kwenyewe kuna waarab na wayahudi wakristo, halikadhalika Israel kuna waarab pia ambao ni wasrael na pia waislamu. Hivyo kuingiza dini hapa ni kukosa hoja ya msingi.


Kuna mambo ukitanguliza mihemko ya dini mbele basi hauwezi kuona ukatili, mateso na mauaji wanayopitia wale wasiokuwa wa dini yako. Hivyo sio kila anae support Israel ni mkristo au anaepingana nayo ni muislamu, huu unakua ni ujinga na upeo mdogo wa kufikiri.

Tukija katika swala sijui hilo la waarab kuwauwa watu weusi sijui liliingiaje, maana kama kuuwa watawala wote waliuwa wakiwemo wazungu.

1. Chief Mkwawa aliuwawa na nani?
2. Kinjekitile aliuwawa na nani?
3. Milambo aliuwawa na nani?
4. Wadai uhuru katika nchi zote za kusini mwa Afrika waliuwawa na kina nani?
5. Red Indians huko Amerika waliuwawa na nani?

Australia ilikuwa na wazawa kabla ya waingereza kuvamia nchi yao, unajua walichofanyiwa?

Tukija kwenye vitabu vya dini ulivyosema, naona unarudi kule kule nilipokwambia hapo juu. Kwamba mipaka ya nchi haipatikani kupitia hadithi za biblia wala msahafu. Hiyo misahafu na biblia imeandikwa na watu tu kama wewe. Na sio kila mtu ana amini katika biblia au msahafu, hivyo kuleta habari za msahafu kwa watu wasiamini msahafu ni kupoteza muda bure, hivyo hivyo kuleta habari za biblia kwa watu wasiamini biblia ni kupoteza muda bure.

Umoja wa Mataifa ambao hauendeshi sheria zake kupitia mihemko ya kidini, wameshaweka wazi kuwa hao jamaa ni wavamizi. Sasa wewe mfia dini ni nani mpaka uje na habari zako za vitabu?

Kiuhalisia vitabu vyote vya dini vimejaa sintofahamu ambayo mtu mwenye akili hawezi kuingia kichwa kichwa kuamini kila kilichoandikwa katika vitabu hivyo.

Vitabu vinasema eti Yesu alikuwa myahudi, lakini wayahudi wenyewe wanakataa kuwa katika kabila lao au nchi yao hajawahi kuzaliwa au kutokea mtu anaeitwa Yesu. Yani mtu aje awambie majirani zako kwamba Mo Dewji ni mjomba wako na anaishi kwako, wakati wewe mwenyewe huyo Mo Dawji familia yenu nzima hamumjui, haishi nae nae wala haujawahi kumuona. Sasa kiuhalisia kati yako wewe mwenye familia husika ambae unakataa kuwa Mo Dewji sio ndugu yenu na huyo mtu anaesimulia nani atakaetakiwa kuaminiwa?

Wazungu wenye mission zao wanalazimisha kuwa Yesu alikuwepo na aliishi Israel, waisral wenyewe wanakataa kuwa huyo Yesu hakuwahi kuwepo katika nchi yao. Sasa wewe mmatumbi uliemezeshwa matango pori, leo unataka kujifanya unajua zaidi ya wayahudi wenyewe πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Unazungumzia mehemko ya kidini unairudia mwenyewe Mzee hebu soma ulichandika. Mi ninachokuambia ni kuwa hakujawah kuwepo taifa la Palestine. Ila ilikuwepo ottoman impaya Palestine territory. So ndani yake walikuwepo waarabu na wayahud. Sasa wakat wa utawala wa kiingereza umoja wa mataifa ulitoa suluhisho la mataifa mawili pamoja wapalestina wakakataa. Israel ikaamua kuunda taifa. Hamas mission yake ni kuifuta Israel so mi nawaunga mkono Israel coz kikawaida mtu akitaka kukuua ukimuwah huna dhambi. By the way kama waarabu walinyang'anywa hilo eneo na kizazi cha nne huko nyuma huyu mjukuu wa kiyahud leo unamuambia aende wapi badala ya kukubaliana muishi. Yaan mtu kama Mo dewji amezaliwa hapo umwambie arud uhindin kwa nani sasa.
 
Unazungumzia mehemko ya kidini unairudia mwenyewe Mzee hebu soma ulichandika.
Mimi nimeandika hivyo baada ya kuona wewe unaleta habari sijui za mudy, habari za madrasa, mara unaniita mimi sheikh wakati haunijui na wala sikujui, haujui labda mimi siamini katika dini zenu zilizoletwa na wakoloni nk. Ndomaana nikakuona wewe una upeo mdogo, maana ukiona mtu ana comment kinyume na kile unachotaka kukisikia wewe kuhusu Israel basi huyo wewe kwako unamuona ni muislam, sheikh.

Unasahau au unashindwa kujua kuwa kuna wakristo kibao ambao wanai support Palestina mmoja wapo akiwa baba wa taifa letu ambae ni mkristo halisi wa baba na mama, na kuna utaratibu unafanyika ili kuhakikisha anakuja kutambulika kama mtakatifu na kanisa lake alilokuwa anaabudia yani kanisa katoliki. Unasahau au unashindwa kujua kuwa Mandela, Mugabe, Desmond Tutu wote walikuwa wakristo na walisimama upande wa Palestina. So kuamini kuwa kila anaepinga uvamizi uliofanywa na Waingereza kupitia mgongo wa wayahudi kuwa ni muislam ni kukosa uelewa na ufahamu mzuri, ndomaana nikakutolewa mfano wa karibu tu wa watu unaowafahamu ili iwe rahisi kunielewa.
Mi ninachokuambia ni kuwa hakujawah kuwepo taifa la Palestine. Ila ilikuwepo ottoman impaya Palestine territory.
Hata taifa la Israel kabla ya Waingereza kuleta watu wao hapo halikuwepo. Kama lilikuwepo leta ushahidi wenye fact zinazotambuliwa na sheria za kimataifa kuhusu mipaka ya nchi. Sio ulete hadithi za misahafu na biblia ambazo hazitambuliki kisheria katika mahakama yoyote ya kimataifa.
So ndani yake walikuwepo waarabu na wayahud. Sasa wakat wa utawala wa kiingereza umoja wa mataifa ulitoa suluhisho la mataifa mawili pamoja wapalestina wakakataa.
Hapa pia umeendelea kuleta zile zile story za vijiweni ambazo hazina ukweli wowote. Unaposema kuwa wapalestina walikataa suluhisho la mataifa mawili umetumia kigezo gani kuamini hivyo. Mbona ushahidi wote unaonesha kuwa ni waisrael wenyewe tena viongozi wa juu ndio wanaokataa suluhu la mataifa mawili.

Netanyahu amekuwa akipinga wazi wazi hadi kupishana kauli na kina Biden wanaompa silaha na fedha za kujilinda kama mtoto mdogo. Ushahidi wa Israel kukataa suluhu ya mataifa mawili nitakuwekea hapo chini usome. Ila kwa huu ushahidi ulioandikwa kingereza, nakuomba utafute mtu mwenye kujitamba ndio akutafsirie kilichoandikwa. Ila ukimpa mfia dini kama wewe na yeye atakuongezea matango pori mengine, alafu urudi hapa kuandika vinginevyo πŸ˜‚πŸ˜‚
Israel ikaamua kuunda taifa. Hamas mission yake ni kuifuta Israel so mi nawaunga mkono Israel coz kikawaida mtu akitaka kukuua ukimuwah huna dhambi.
Suluhisho lilifanywa la Israel kuchukua upande mmoja na Palestina kuchukua upande mungine. Lakini Israel bado ilikuwa inaendelea kuingia katika ardhi za wapalestina huko west bank inajenga majumba na kuwakabidhi wazungu wenzao wakae katika ardhi za wenzao. Je ingekuwa wewe ungekubali mtu avuke katika ardhi yake aje ajenge katika ardhi yako?

Kibaya zaid wale wanaonyang'anywa ardhi zao wakiingia barabarani kuandamana ili dunia ijue na ione kile kinachofanywa na wazungu, serikali ya Israel inatuma polisi na jeshi lenye masilahi makubwa makubwa likapambane na raia wanaotumia mawe tu kuji defend ili wasiuwawe.

Sasa wanauwawa, wanateswa, wanapigwa, wanakamatwa, wanafungwa na wengine kunyanganywa mpaka nyumba zao walizojenga kwa gharama zao katika viwanja vyao. Alafu ulitaka Hamas au wapalestina waendelee kukaa kimya tu, waangalie mpaka waje kujikuta wamehamishwa wote kimya kimya?
By the way kama waarabu walinyang'anywa hilo eneo na kizazi cha nne huko nyuma huyu mjukuu wa kiyahud leo unamuambia aende wapi badala ya kukubaliana muishi. Yaan mtu kama Mo dewji amezaliwa hapo umwambie arud uhindin kwa nani sasa.
nimeshakutolea ushahidi kuwa wanaokataa suluhisho la mataifa mawili ili kila nchi iishi kwa amani ni waisrael. Leta na wewe ushahidi ambao unaonesha kuwa wapalestina wamekataa suluhisho hilo la mataifa mawili ili tuelewe ulichoandikwa.

Wengine ni kama kina Nyerere, hatujui habari za madrasa ila tunasimamia ukweli wa kile kinachoendelea huko Mashariki ya kati.
 

Attachments

  • IMG-20240125-WA0008.jpg
    58.7 KB · Views: 8
  • IMG-20240125-WA0007.jpg
    35.1 KB · Views: 7
NNakubariana mkuu ukiwa nimtu was kushughuriskushughurisha hakiri kwa maelezo yako hukosi kuuona ukweli was Jambo HiliπŸ™πŸ™
Asante mkuu. Wengi hawafahamu kinachoendelea pale Mashariki ya kati kwa sababu ya kuendekeza utaratibu wa kusikiliza upande mmoja wa wazungu tu. Ila ukiwa mtu wa kushughulisha akili yako kutafuta ukweli lazima utaupata tu, kama sio leo basi kesho.
 
Vijana mna maneno sana aisee...
 
We kumbe naongea na kilaza. Nil
Kumbe naongea na kilaza nilifikir naongea na mtu mwenye hoja kumbe wale wale. Ushasoma historia kabla wayahud kuanzisha hilo taifa lao waingereza by then wakiwa wanalitawala hilo eneo kama wadhamini baada ya ottomani mpaya kuanguka hujui walipeleka hiyo kesi UN ili liamuliwe huko. Na UN wakaja na jins ya kuligawa waarabu wakalikataa pendekezo. Ndio vita ikaanza rasmi. Unajua wewe ni wale vilaza wanaoamini akiongea Nyerere au mandela au Kikwete ameongea Mungu. Bro Nyerere mwenyewe alikuwa na makosa mengi tu. Ni kama alivyosema Pope juz mashoga wabarikiwe kwa akili yako kwa nafas yake kaongea jambo la maana. Mi siongoz na baba au mama. Mi ni binadamu kamili mtu mzima ninauwezo wa kuona Jambo na nikalitafsr ni libaya au lizur. So huongei na mateka wa fikra. Hamas wamesema hawaitambui Israel na watawafuta na hicho wanachopata ni style yao. Period. Mambo ya cjui wakristo waislam cjui vitabu vya Dini hizo ni ngonjera zako. Hata hao Iran wanapigana kwa maslah ya din nothing more.
 
unahisi Israel ni msumbiji , magaidi yanaua watu ila bado wanawachekea masheikh wanaoingia kule bila kaz maalumu zilizo waz
 
Hapo sasa wenyewe hilo hawalion usalama wake ajilinde akiwa kwenye ardhi yake
jiran yako anakurushia mabomu kila siku na anaimba kuwa anataka kukuangamiza usiwepo dunian , utajilindaje bila kumsogeza mbali na wewe ? hv hii dini imewafanya muwe vichaa?
 
Msaada mkubwa umetoka Iran japo na Mrusi nae kachangia kuyateketeza magenge ya marekani na washirika wake.
watu wapo kimaslai ww omba omba unasema kasaidia , baada ya miaka kadhaa mtamfuata Marekan awasaidie kumtoa mrusi na iran , historia haidanganyi
 
Aisee nilifikiri ni kiatu kumbe mguu wa binadamu., huyu atakuwa myahudi kutoka Buseresere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…