Acha makasiriko ya madrasa sheikh. Naomba nikuize swali. Hiv unajua misri na nchi zote zao northern Africa zilikuwa ni za waafrica waarabu wakawaua wakachukua nchi zao. Unajua mafarao walikuwa ni Africa? Turud kwenye mada. Neno biblia lina maana ya vitabu sio kitabu. Ukichukua Jews holy book inaelezea nchi yao na mipaka yao. Hata hicho kitabu cha mudy kinajua na kutambua Jews walikuwepo na nchi yao. Nachokusaidia ni kuwa kama Jews walikuwepo hata wakat wa ottoman impaya basi. Hapo ndio kwao shida iko wapi. Wapo kwao na wamejitengenezea nchi. Hiv wale wazungu wa South Africa ni wenyeji au wagen au Australia au America
Bado uliyoandika yanaonesha upeo mdogo wa kufikiri kichwani kwako. Yani upeo mdogo wa kuamini kuwa kila anaepingana na Israel ni muislam. Upeo wako mdogo unashindwa kufahamu kuwa serikali ya Afrika Kusini iliyoifungulia Israel kesi ya mauaji ya kimbali inaongozwa na wakristo 99%.
Upeo wako mdogo umekufanya ushindwe kujua kwamba kuna watu kama kina hayati Desmond Tutu walikuwa wanaijua bibla zaidi ya vile uijuavyo wewe myahudi wa kimatumbi, lakini kwa sababu ya haki na uhalisia wa kile kinachoendelea Palestina aliamua kusimama upande wa wapalestina na kuweka mihemko yake ya kidini pembeni. Hata huko Marekani kuna maseneta wazungu tena wakristo ambao hawapendezewi na kile kinachoendelea na Israel huko Palestina. Sasa hayo mambo ya dini katika swala nyeti kama hili yanatoka wapi wakati Palestina kwenyewe kuna waarab na wayahudi wakristo, halikadhalika Israel kuna waarab pia ambao ni wasrael na pia waislamu. Hivyo kuingiza dini hapa ni kukosa hoja ya msingi.
Kuna mambo ukitanguliza mihemko ya dini mbele basi hauwezi kuona ukatili, mateso na mauaji wanayopitia wale wasiokuwa wa dini yako. Hivyo sio kila anae support Israel ni mkristo au anaepingana nayo ni muislamu, huu unakua ni ujinga na upeo mdogo wa kufikiri.
Tukija katika swala sijui hilo la waarab kuwauwa watu weusi sijui liliingiaje, maana kama kuuwa watawala wote waliuwa wakiwemo wazungu.
1. Chief Mkwawa aliuwawa na nani?
2. Kinjekitile aliuwawa na nani?
3. Milambo aliuwawa na nani?
4. Wadai uhuru katika nchi zote za kusini mwa Afrika waliuwawa na kina nani?
5. Red Indians huko Amerika waliuwawa na nani?
Australia ilikuwa na wazawa kabla ya waingereza kuvamia nchi yao, unajua walichofanyiwa?
Tukija kwenye vitabu vya dini ulivyosema, naona unarudi kule kule nilipokwambia hapo juu. Kwamba mipaka ya nchi haipatikani kupitia hadithi za biblia wala msahafu. Hiyo misahafu na biblia imeandikwa na watu tu kama wewe. Na sio kila mtu ana amini katika biblia au msahafu, hivyo kuleta habari za msahafu kwa watu wasiamini msahafu ni kupoteza muda bure, hivyo hivyo kuleta habari za biblia kwa watu wasiamini biblia ni kupoteza muda bure.
Umoja wa Mataifa ambao hauendeshi sheria zake kupitia mihemko ya kidini, wameshaweka wazi kuwa hao jamaa ni wavamizi. Sasa wewe mfia dini ni nani mpaka uje na habari zako za vitabu?
Kiuhalisia vitabu vyote vya dini vimejaa sintofahamu ambayo mtu mwenye akili hawezi kuingia kichwa kichwa kuamini kila kilichoandikwa katika vitabu hivyo.
Vitabu vinasema eti Yesu alikuwa myahudi, lakini wayahudi wenyewe wanakataa kuwa katika kabila lao au nchi yao hajawahi kuzaliwa au kutokea mtu anaeitwa Yesu. Yani mtu aje awambie majirani zako kwamba Mo Dewji ni mjomba wako na anaishi kwako, wakati wewe mwenyewe huyo Mo Dawji familia yenu nzima hamumjui, haishi nae nae wala haujawahi kumuona. Sasa kiuhalisia kati yako wewe mwenye familia husika ambae unakataa kuwa Mo Dewji sio ndugu yenu na huyo mtu anaesimulia nani atakaetakiwa kuaminiwa?
Wazungu wenye mission zao wanalazimisha kuwa Yesu alikuwepo na aliishi Israel, waisral wenyewe wanakataa kuwa huyo Yesu hakuwahi kuwepo katika nchi yao. Sasa wewe mmatumbi uliemezeshwa matango pori, leo unataka kujifanya unajua zaidi ya wayahudi wenyewe 😂😂😂😂