Mazungumzo yale na Mzee Waikela ndiyo yaliyotengeneza sehemu ya tatu katika
kitabu cha Abdul Sykes na sehemu hiyo nikaipa jina, ''Njama Dhidi ya Uislam (1961 -
1970).''
mleta hoja unachobisha ni nini watu tunakuambia hapa unatuletea udini unabisha .kama hoja yako ilikuwa ni kutujulisha wanaharakati waliopigania sisi kupata Uhuru,basi hoja yako ungejikita kutuelezea wasifu wao na namna alivyochangia katika harakati.
Ajabu unatuletea habari za mpigania Uhuru huku hoja yako imebezi kwenye uislamu.tena unadiriki kuandika kabisa akaniambia andika uwambie waislamu.nawe ukaandika kitabu njama dhidi ya uislamu.
Alafu unatuambia nilikuwa huzungumzii udini je ulipoandika "njama dhidi ya uislamu " ulikuwa unamanisha nini.kama sio kupandikiza chuki za udini kwa waislamu kwamba mmedhurumiwa sana tangu kudai Uhuru.
Umechemka sana usiwe unatuletea porojo porojo zako hapa za udini ukidai ni harakati za uhuru.unadhani hatuijui fasihi[/QUOTE]
Tunene,
Hakika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika imejaa Waislam kila kona.
Ukijaribu kuwaondoa utakuwa umetoa sehemu kubwa ya historia ya kweli.
Kitabu cha
Abdul Sykes kilipochapwa London mwaka wa 1998 kilipofika Dar
es Salaam kishindo kilikuwa kikubwa.
Walipigwa na butwaa wale waliokuwa wanaijua historia ya uhuru kupitia
historia rasmi iliyoandikwa na Chuo Cha Kivukoni mwaka wa 1981.
Ndani ya kitabu cha Kivukoni historia ya TANU ilikuwa imefuta majina mengi
ambayo ndiyo haya sasa mnayasoma hapa ya akina
Sheikh Hassan bin Amir,
Bilai Rehani Waikela na kubwa matatizo yaliyotokea baada ya uhuru moja
ikiwa ni hili la kufuta historia ya kweli na kuweka nyingine.
Kuwa mimi nimeandika historia ya Waislam wala sikatai.
Hiyo ndiyo ilikuwa nia yangu khasa.
Kuwa palikuwa na njama dhidi ya Uislam baada ya uhuru ni historia ya uhuru
wa Tanganyika atakae anaweza akasoma akajua kilitokea nini na nani walikuwa
wahusika wakuu.
Ikiwa kuna mtu anakerwa na kuandikwa kwa historia hii hiyo ni bahati mbaya
kwake.
Ikiwa utaona hizi ni ''porojo,'' una uhuru wa mawazo yako siwezi kukuingilia.
Unaweza hata ukakataa kuamini kama kulikuwa na
Abdul Sykes na nduguye
Ally wakaunda TANU kutoka African Association aliyoasisi baba yao mwaka wa
1929 wakiwa na
Nyerere na vijana wengine waliokuwa Dar es Salaam ya 1950s.
Uhuru ni wako.
Nakuona umeghadhibika.
Hili ni katika jambo moja ambalo mimi sikulitegemea wakati naandika historia
hii.
Sikutegemea hata siku moja kuwa historia hii ya wazee wangu itawaumiza
baadhi ya watu.