Bilal Waikela ni nani?

Bilal Waikela ni nani?

Waislamu wamelipua watu Manchester huko umesikia?
Al Watan nimesikia lakini nakuomba uzingatie jambo moja. Hayo si katika mafunzo ya Uislam na ni bahati mbaya sana wanatumia jina la Uislam. Leo katika Ukristo lipo tatizo kubwa la ushoga tena kwa viongozi wakuu wa Kanisa. Haya si mafunzo ya Yesu Kristo. Mimi siwezi kupanua kinywa changu na kuwachafua Wakristo kwa vitendo hivyo kwani si katika yale yaliyo ndani ya Ukristo. Siwezi nikakuwekea hapo post nakuambia, "Umesoma mahali kadhaa padri analawiti watoto wadogo?" Nitakuwa sijatumia akili yangu kutafakari mambo.
 
UKristo umesema umewapa wafuasi wake sheria mpya ya upendo.

Labda wanatekeleza sheria hiyo.

Katika Uislamu/ Quran hakuna mafunzo ya kuua makafiri?

The Quran's Verses of Violence

Quran

Quran (2:191-193) - "And kill them wherever you find them, and turn them out from where they have turned you out. And Al-Fitnah [disbelief or unrest] is worse than killing... but if they desist, then lo! Allah is forgiving and merciful. And fight them until there is no more Fitnah [disbelief and worshipping of others along with Allah] and worship is for Allah alone. But if they cease, let there be no transgression except against Az-Zalimun(the polytheists, and wrong-doers, etc.)" (Translation is from the Noble Quran)
 
UKristo umesema umewapa wafuasi wake sheria mpya ya upendo.

Labda wanatekeleza sheria hiyo.

Katika Uislamu/ Quran hakuna mafunzo ya kuua makafiri?

The Quran's Verses of Violence
Al Watan mimi sina haja ya kufanya ubishani na wewe katika Uislam na mafunzo yake. Post yangu iliyopita nimekujibu hilo uloniuliza la mauaji kwa kukuonyesha matatizo yaliyopo. Hapa ilikuwa tunajadili historia ya Bilal Waikela.
 
Huna haja ya kufanya mabishano au huna majibu?

Dini yenu inafundisha uuaji.

Mstari mmoja huo hapo juu. Kutoka katika Quran.

Huo ni ukweli ambao huwezi kuubishia.

Ukibisha utaibishia Quran.

Ndiyo mana hutaki kujadili.

Dini yenu ni ya kigaidi na kiuaji.

Ukisema hao magaidi wanaoua watu hawafuati mafundisho ya Uislamu unadanganya.

Kwa sababu Quran imewaambia waue.

Bisha.
 
Hapana kaka mimi si mtu wa ubishani.
 
Hapana kaka mimi si mtu wa ubishani.

Ukisema "hapana kaka mimi si mtu wa ubishani" ushabisha tayari na hivyo ushakuwa mtu wa ubishani.

Hujibu si kwa sababu wewe si mtu wa ubishani, bali kwa sababu huna jibu ambalo linaweza kusimamia amani bila kuikataa Quran.

Ndiyo sababu hujibu.

Hilo la kukataa ubishani ni kisingizio tu.

Uislamu ni dini ya kigaidi na kiuaji. Quran inafundisha hayo. Mistari nimeiweka hapo juu. Kubisha hili ni kuibishia Quran.
 
Mmoja wa Waasisi wa TANU Mikoa ya Magharibi

Don wa Zamani Mpigania uhuru aliekuwa anamiliki Rizki ya kutosha ikiwemo 'Motokari' Miaka ya 1960 enzi hizo kwa Sheria ya Nyerere kumiliki gari lazima Muwe Watu Sita kuombea Kibali cha Umiliki

Mpinga Bakwata wa awali kabisa Tangu inaanzishwa1967 akipinga kwa hoja kuwa inafanywa tawi la TANU/CCM ni Mzaliwa wa Tabora
Anyetaka kumjua zaidi atafute video iliyorekodiwa siku ya muungano wa UKAWA maana Prol Lee Pum Bah ndio aliyemualika ili amtumie kama steping stone.
 
Nadhani Mzee Bilal Waikela nae alitopea kwenye udini ndio maana historia yake ilitupwa sababu ilikwenda mlengo tofauti na Mwl Nyerere japo ni kweli ni mtu muhimu sana kwa uhuru wa nchi hii na hata vijana wa leo tunaona mifano hai, pia mambo ya kujitambulisha kwa kigezo cha dini hakikubariki katika nchi yetu sababu imeleta shida sana kwa wanadamu rejea mfano mdogo wa nchi ya Afrika ya kati huo udini ulivyoleta tabu ukiachia mbali nyingine tuzijuazo.

Kuna wakati Askofu Gwajima aliwahi kutoa mfano hai kabisa japo mimi sio muumini wake, aliwahi kusema "itakuwaje mtu akahukumiwa kwa sheria za kiislamu (Sharia) muda huu halafu akakimbilia kwenda kuokoka kanisani muda mchache tu, je hapo hakutakuwa na mvutano kuhusu mtu huyo juu ya uhalali wake" na ikitokea itakuwaje?

Kuna swala kidogo tu ambalo na mimi nimelishuhudia kuhusu kuchinja lilivyoleta mvutano, sasa tukitaka tujitambulishe kwa udini wetu tutafikia wapi?

Tutafakari kwa umakini ndugu zangu wote ni Watanzania
 
Dini zenyewe zote uongo mtupu.
 
Peter...
Tatizo kubwa sana ninalokutananalo hapa Majilis ni kuwa wengi wenu hamuijui
historia ya uhuru wa Tanganyika.

Ingekuwa waasisi wa harakati hizi za kudai uhuru wangejikita katika maslahi ya
dini zao hali ingekuwa ngumu sana kwa TANU.

Kabla Abdul Sykes hajakutana na Nyerere 1952 yeye alikuwa na mpango wa
kumtia Chief Kidaha Makwaia katika TAA kisha waunde TANU na kudai uhuru
na Chief Kidaha aje kuwa Waziri Mkuu wa kwanza.

Chief Kidaha hakuwa Muislam na anaetaka kumleta katika TAA Abdul Sykes yeye
alikuwa katika Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika chama alichoasisi baba yake
1933 (elewa pia kuwa hata hiyio TAA aliasisi baba yake Abdul, Kleist Sykes 1929
na akajenga hiyo ofisi ambayo ilikuja kuzaliwa TANU 1954).

Lakini Hamza Mwapachu yeye alipendelea Abdul amtie Nyerere katika uongozi wa
TAA kisha ndiyo waunde TANU.

Nyerere hakuwa Muislam na wanaotaka achukue uongozi wa TAA na kuunda TANU
ni Abdul Sykes na Hamza Mwapachu, wote Waislam.

Kabla ya haya mwaka wa 1950 aliyesimama kwa juhudi kubwa kumtia Dr. Vedasto
Kyaruzi
katika uongozi wa TAA kama rais alikuwa Schneider Abdillah Plantan.

Kabla ya uchaguzi wa mwaka wa TAA 1953 kuchagua rais wake Abdul Sykes na Ali
Mwinyi Tambwe walisafiri hadi Nansio kwa Hamza Mwapachu, Abdul akitaka
kupata kauli ya mwisho ya Mwapachu kuhusu Nyerere kuachiwa na Abdul kiti cha
urais wa TAA.

Huyu Ali Mwinyi Tambwe ndiye kwa wakati ule 1950s alikuwa katibu wa Al Jamiatul
Islamiyya Fi Tanganyika.

Mwapachu alimwambia Abdul kuwa wakiasisi TANU na yeye Abdul ndiye rais na kudai
uhuru harakati zile zitaonekana za Waislam.

Mwapachu akasena lakini harakati akiongoza Nyerere Mkristo Waingereza watakuwa
watatulia.

Bilal Rehani Waikela
hakupata hata siku moja kwenda kinyume na msimamo wa
kiongozi wake Sheikh Hassan bin Amir ambae yeye alimuunga mkono Nyerere toka
siku ya kwanza alipopelekwa kwake na Abdul Sykes na Dossa Aziz.

Sheikh Hassan bin Amir ndiye aliyefanya juhudi ya kuifanya TANU isionekana kama
chama cha Waislam katika mkutano wa siri alioitisha usiku Mtaa wa Pemba 1955.

Hii ilikuwa 1953.

Bila kuijua historia hii ya uhuru wa Tangnayika mtu atahangaika katika kiza na kujikwaa
ovyo.
 
Nadhani Mzee Bilal Waikela nae alitopea kwenye udini ndio maana historia yake ilitupwa sababu ilikwenda mlengo tofauti na Mwl Nyerere japo ni kweli ni mtu muhimu sana kwa uhuru wa nchi hii na hata vijana wa leo tunaona mifano hai, pia mambo ya kujitambulisha kwa kigezo cha dini hakikubariki katika nchi yetu sababu imeleta shida sana kwa wanadamu rejea mfano mdogo wa nchi ya Afrika ya kati huo udini ulivyoleta tabu ukiachia mbali nyingine tuzijuazo.

Kuna wakati Askofu Gwajima aliwahi kutoa mfano hai kabisa japo mimi sio muumini wake, aliwahi kusema "itakuwaje mtu akahukumiwa kwa sheria za kiislamu (Sharia) muda huu halafu akakimbilia kwenda kuokoka kanisani muda mchache tu, je hapo hakutakuwa na mvutano kuhusu mtu huyo juu ya uhalali wake" na ikitokea itakuwaje?

Kuna swala kidogo tu ambalo na mimi nimelishuhudia kuhusu kuchinja lilivyoleta mvutano, sasa tukitaka tujitambulishe kwa udini wetu tutafikia wapi?

Tutafakari kwa umakini ndugu zangu wote ni Watanzania
Naomba kujua kutoka kwako mlengo wa Mwl Nyerere ambao ulisalimika na "udini" ukiutofautisha na mlengo wa Mzee Bilal Waikela ambao kwa "kudhani" kwako ulitopea kwenye "udini"
 
Boywise,
Nimeeleza kila kitu kuhusu Bilal Waikela katika kitabu cha Abdul Sykes.

Nitakujibu hapa swali lako lakini kwa kuelewa historia nzima ya TANU
na uhuru wa Tanganyika ni muhimu sana tena sana ukasome kitabu hiki.

Farka baina ya Waikela na Nyerere ilitokea mwaka wa 1963 katika mkutano
wa EAMWS uliofanyika Dar es Salaam Waikela alipomsomea Nyerere risala
ya Waislam kuhusu chokochoko zilizokuwa zimejitokeza kwa serikali kutaka
ivunjwe EAMWS wakati walikuwa na mipango ya kujenga Chuo Kikuu.

Risala hii haijapatapo mwenzake sasa nusu karne imepita.

Waikela akimtazama Nyerere usoni alimkumbusha juhudi za Waislam katika
kupigania uhuru wa Tanganyika ili watu wawe huru kutokana na dhulma zote.

Ukitoa ugomvi wa 1958 baina ya Sheikh Suleiman Takadir na Nyerere hii
risala ya Waikela ilikuwa inawarudisha Waislam nyuma kutafakari upya hali
yao ya baadae katika Tanganyika huru.

Historia ya uhuru wa Tanganyika ina mambo mengi sana ya kusisimua.

Anaependa kuijua historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika asome kitabu cha
Abdul Sykes.
 
ivunjwe EAMWS wakati walikuwa na mipango ya kujenga Chuo Kikuu ili nao
Waislam wawe na uwezo wa kuweza kushiriki katika uongozi wa nchi.

Shukran Mzee wangu Mohamed Said, na kuhusu kitabu ninacho na nimetoa tongotongo nyingi sana kunako historia ya nchi yangu
Binafsi nilielekeza swali hili kwa peterwapeter ili anishibishe kunako hoja yake aloijenga kwa kudhani juu ya mada yetu
 
Maashaallah shekh Mohamed Said tunakuelewa jazaqallahu kheir
 
Asalaam aleikum maalim.
Nimekuwa mfuatiliaji mkubwa wa makala na maandiko yako mengine.Hongera sana kwa kuutangaza na kuutetea umma was kiislamu ingawa historia "ya pili" imekuwa ni kikwazo katika hili.
Naamini Allah (s.w) ataendelea kukuongoza udumu katika kheri.Inshaallah.
Pamoja na hayo, natamani kupata nakala(hata soft copy) za maandiko yako.
Maalim asante, sana sasa nimeelewa, kumbe ilikuwa ni Presidential Preventive Detention Order. Hii kitu iliwahi kumkuta Mzee wangu Andrew Mayalla (RIP) aliyekuwa RSO wa Mwanza. Nyerere kiukweli alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo, alikuwa hataki kabisa ujinga ujinga wa aina yoyote. Sisi Wakatoliki tuko kwenye mchakato wa kumtangaza Mwenye Heri ambayo ni daraja moja kabla hajawa Mtakatifu. Naomba tukimtaja Nyerere popote, tumtaje kwa kutazama only the bright side of him and not the dark side isije kuchelewesha mchakato wetu.

Paskali
 
Back
Top Bottom