Habari naomba kusaidiwa dawa ya kupona bile acid reflux, nilienda hospital baada ya kuwa nasumbuliwa sana na tumbo kuwaka moto kama naungua tumboni baada ya kipimo cha endoscopy shida ilionekana mlango wa chini wa tumbo upo wazi nyakati zote( sphincter pyloric) kwahiyo unaruhusu alkaline kutoka utumbo mdogo kuingia katika tumbo, tumbon ni acid na utumbo una alkaline sasa vikiwa mixed ndo inatokea hicho kitu kama moto tumboni pia nikaonekana nina michubuko tumboni, nilipewa dawa protonex 40mg na gel lakini shida ndo kama vile inazidi mtu yoyote aliyepona tatizo kama langu naomba msaada nateseka siwezi kula maisha yangu yamekuwa ya huzuni