Bili yako ya maji mwezi Februari inaendana na uhalisia wa matumizi yako?

Meter inasomaje?.
Ilipoishia na ilipo sasa!?.
Namba zinakuja hivyo... lakini ukiangalia matumizi na jinsi maji yanavyokatika haimake sense kupata namba hiyo.

Kuna sehemu nilikaa wakati fulani, aisee bili ilikuja units 25... niko mwenye, sikuwepo nyumbani kwa wiki mbili, muda ambao nilikuwepo sishindi mchana - ni weekend pekee, lakini bili ilikuja hivyo! Alikuja mhudumu wa DAWASA baada ya kuwatafuta sana sikupewa maelezo ya kwanini bili imesoma vile, walibaki kusema tu itakuwa ni matumizi yako!

RoadLofa
 
Labda wewe ndio mvivu usitujumuishe wengine, kama hizo mashine zingekuwa nzima zisingekuwa zinasoma upepo, na ndio wanavyojitapa kuwa zina njia ya ku isolate upepo na kuhesabu maji pekee
 
Ndugu mteja A/C , KUMBUKUMBU , Bill yako ya Februari/2025 umetumia uniti 4, kutoka 326 mpaka 330 sawa na Tshs. 6718.52. Salio/Ziada ni Tshs. -3998.11, jumla unadaiwa Tshs. 2720.41. Tafadhali Lipia sasa, BILI HII NI NOTISI. (Piga 0800110064 bure)
 
Ndugu mteja A/C , KUMBUKUMBU , Bill yako ya Februari/2025 umetumia uniti 4, kutoka 326 mpaka 330 sawa na Tshs. 6718.52. Salio/Ziada ni Tshs. -3998.11, jumla unadaiwa Tshs. 2720.41. Tafadhali Lipia sasa, BILI HII NI NOTISI. (Piga 0800110064 bure)
Hongera Mkuu.... kupata bili ya hivi ilikuwa mwaka juzi sijui.... nikaanza unit 2, mara zikapanda 4, ikaenda 10.... ikashoot 15... ikaja ya 20+ matumizi hayajabadilika lakini bili ina evolve😢
 
Yaani wanapandisha kila mwezi 🥺
 
Meter inasomaje?.
Ilipoishia na ilipo sasa!?.
Mimi nimegundua kwangu tatizo ni mita yao inazunguka kwa spidi zaidi ya uhalisia wa lita zinazotoka kwenye bomba. Nilishafanya majaribio kujaza tank ya lita 3,000 huku nikiredi unit nilitegemea nipate unit 3 ila cha ajabu ilizidi zaidi ya mara 4 yake, nimewaeleza kwa vielelezo lakini hakuna kilichofanyika sasa na mimi nimekataa kuwa mnyonge ninalipa kile ninachotumia tu.
 
utajua hata muda wanaopita? sometimes usiku wa manane sijui jamaa wanga
 
NIMETOKA KUWAKA OFISIN KWAOO MKUU MBEZI BEACH N WAHUNI KUNA MCHAGA MMOJA ANACHEXA NA JAMAA WENYE BILL KUBWA MNAMCHANGIA KUWALIPIA WANAKULA CHA JUU
 
Wana ujinga huo sana. Kuna kipindi nilikuwa ninakaa kwenye nyumba fulani ina apartments 4 yaani kila family na apartment yake. Family iliyokuwa na watu wengi ni 1 yenye watu watatu na moja ina watu wawili na 2 zilizobaki mtu mmoja mmoja. Bill ilikuwa ikija tunagawa flat rate tunalipa. Average tulikuwa tunalipa around 6,000/= hadi 8,000/= kwa kila family kwa mwezi. Kuna kipindi families 2 zilihama tukabaki 2. Bill iliyokuja mwezi uliofuata ilikuwa units 365!!! Sawa na shilingi laki 5 na kitu!!! Kwenda kusoma mita inasoma kama ilivyokuwa ilivyoandikwa. Tukaenda kuuliza how imekuwa hivyo walitujibu hivyo hivyo eti tumetumia hayo maji. Maji yenyewe yalikuwa yanatoka twice a week. Tukagoma kulipa wakakata maji nikahamia sehemu nyingine. Baadaye niliwahi kuambiwa kuwa sometimes wanacheza na hizo mita sasa sijui kama ni kweli.
 
Saa hivi hizi mita mpya za dawasa xinaibasana mi juzi nimechota ndoo 30 za lita 20 imeenda unit moja wakati kiuhalisia inatakiwa ndoo 50
 
kuna suala la maji kuvuja na pia jambo ambalo wengi hawalijui ni suala la hewa kupita kwenye mita na inazungusha mita kama ilivyo maji. Unapaswa kuondoa hewa kwenye maji kabla maji hayajapita kwenye mita la sivyo utalipia hewa kila mwezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…