Bili yako ya maji mwezi Februari inaendana na uhalisia wa matumizi yako?

Bili yako ya maji mwezi Februari inaendana na uhalisia wa matumizi yako?

Wakuu salam,

Bili za mwezi Februari zimetoka, jamani huku kwetu Mbezi Beach kila mtu anashangaa ubambikaji wa bili hizi. Yaani kwa kila mtu bili imeshoot kuliko kawaida wakati matumizi ni ya kawaida, sio kwamba ni shule au labda unafanya biashara ya kuuza maji.

Tena cha kushangaza zaidi ni kuwa maji yamekuwa ni ya kusuasua zana, mnakaa siku tatu nne hakuna maji, maji yakitoka presha ni ndogo sana yaani hata hayapandi kwenye matenki. DAWASA walitoa ushauri watu tuweke pump za maji lakini kutokana na presha ilivyo ndogo hata kuwa na pump ni kituko, maana zinakosa cha kubust, halafu eti bili inakuja umetumia unit 40, 50! Kivipi? Kwa maji yapi ya kufikia unit hizo?

Imagine kwenye nyumba mko watano, watatu hamshindi nyumbani, kuna safari za kufanya msiwepo nyumbani kwa wiki au hata zaidi, maji yanasua sua unaweza kusema kwa mwezi mmepata maji siku nzima bila kukata labda siku 3 halafu bili inakuja unit 40+, inaingia akilini kweli? Wizara ya Maji

Kama ndio mita zinahesabu upepo hii ya sasa imetia fora, itakuwa pump zinapigwa na kimbuka huko chini mpaka kupata units zote hizo.

Kwa upande wenu hali ikoje Wakuu? Bili zimekuja na uhalisia?

Wizara ya Maji
Bil za nyuma zilikuwa zinacheza 30-40K,ila mwezi huu imepanda mpaka 110k.
 
Mimi wameniongezea unit 1 tu
Ila sio kesi.
Kinachoniudhi wanadai kama Mkopo aisee! Kila dakika ndugu mteja bill hii ni notisi! Mara Dawasa tupo mtaani kwako lipa maji kuepuka usumbufu! Hapo unadaiwa mwezi wa2 na bill wametuma juzi ila sms za vitisho zishafika 5 na wanatuma mpaka usiku
 
kuna suala la maji kuvuja na pia jambo ambalo wengi hawalijui ni suala la hewa kupita kwenye mita na inazungusha mita kama ilivyo maji. Unapaswa kuondoa hewa kwenye maji kabla maji hayajapita kwenye mita la sivyo utalipia hewa kila mwezi.
Hakuna mahali popote palipokuwa panavuja. After all maji yalikuwa yanatoka twice a week hata kungekuwa kuna mahali panavuja tungepaona na isingefika units hizo.

Halafu kuhusu hewa yaani hiyo hewa iliamua kuingia mwezi huo tu? Mbona miezi mitatu iliyofuata kabla ya kukata maji bili ilikuwa inakuja kama ambayo tulikuwa tunatumia kabla ya kuleta hiyo Bill ya ajabu?!!! Mimi nina amini kuna kitu kilifanyika si bure.
 
Wakuu salam,

Bili za mwezi Februari zimetoka, jamani huku kwetu Mbezi Beach kila mtu anashangaa ubambikaji wa bili hizi. Yaani kwa kila mtu bili imeshoot kuliko kawaida wakati matumizi ni ya kawaida, sio kwamba ni shule au labda unafanya biashara ya kuuza maji.

Tena cha kushangaza zaidi ni kuwa maji yamekuwa ni ya kusuasua zana, mnakaa siku tatu nne hakuna maji, maji yakitoka presha ni ndogo sana yaani hata hayapandi kwenye matenki. DAWASA walitoa ushauri watu tuweke pump za maji lakini kutokana na presha ilivyo ndogo hata kuwa na pump ni kituko, maana zinakosa cha kubust, halafu eti bili inakuja umetumia unit 40, 50! Kivipi? Kwa maji yapi ya kufikia unit hizo?

Imagine kwenye nyumba mko watano, watatu hamshindi nyumbani, kuna safari za kufanya msiwepo nyumbani kwa wiki au hata zaidi, maji yanasua sua unaweza kusema kwa mwezi mmepata maji siku nzima bila kukata labda siku 3 halafu bili inakuja unit 40+, inaingia akilini kweli? Wizara ya Maji

Kama ndio mita zinahesabu upepo hii ya sasa imetia fora, itakuwa pump zinapigwa na kimbuka huko chini mpaka kupata units zote hizo.

Kwa upande wenu hali ikoje Wakuu? Bili zimekuja na uhalisia?

Wizara ya Maji
Bill yangu imepanda mara mbili na nusu zaidi shinda ya mwezi wa December. Kwa kweli tunaibiwa hapa.
 
Mimi nimegundua kwangu tatizo ni mita yao inazunguka kwa spidi zaidi ya uhalisia wa lita zinazotoka kwenye bomba. Nilishafanya majaribio kujaza tank ya lita 3,000 huku nikiredi unit nilitegemea nipate unit 3 ila cha ajabu ilizidi zaidi ya mara 4 yake, nimewaeleza kwa vielelezo lakini hakuna kilichofanyika sasa na mimi nimekataa kuwa mnyonge ninalipa kile ninachotumia tu.
Huwa hawakubali maelezo mengine zaidi ya kusema matumizi yako itakuwa makubwa, wakati ni dhahiri tatizo lipo kwao
 
Nadhani wana alternate bill mkoa hadi mkoa kwangu mwezi january ilikuwa 96000 kutoka 50000mwezi desemba.
Na hiyo January watoto wengi walikuwa wamerudi shule.Nyumba haikuwa na watu wengi.Nimejiuliza maswali mengi na jibu sijapata
Naripoti kutokea Mwanza
Yaani hakuna maelezo ya kueleweka kwenye hili
 
Wana ujinga huo sana. Kuna kipindi nilikuwa ninakaa kwenye nyumba fulani ina apartments 4 yaani kila family na apartment yake. Family iliyokuwa na watu wengi ni 1 yenye watu watatu na moja ina watu wawili na 2 zilizobaki mtu mmoja mmoja. Bill ilikuwa ikija tunagawa flat rate tunalipa. Average tulikuwa tunalipa around 6,000/= hadi 8,000/= kwa kila family kwa mwezi. Kuna kipindi families 2 zilihama tukabaki 2. Bill iliyokuja mwezi uliofuata ilikuwa units 365!!! Sawa na shilingi laki 5 na kitu!!! Kwenda kusoma mita inasoma kama ilivyokuwa ilivyoandikwa. Tukaenda kuuliza how imekuwa hivyo walitujibu hivyo hivyo eti tumetumia hayo maji. Maji yenyewe yalikuwa yanatoka twice a week. Tukagoma kulipa wakakata maji nikahamia sehemu nyingine. Baadaye niliwahi kuambiwa kuwa sometimes wanacheza na hizo mita sasa sijui kama ni kweli.
Doh... na haya ndio majibu yao, yaani unashangaa mita inasoma hivyo, hakuna panapovuja unaishia kuangushiwa jumba bovu
 
kuna suala la maji kuvuja na pia jambo ambalo wengi hawalijui ni suala la hewa kupita kwenye mita na inazungusha mita kama ilivyo maji. Unapaswa kuondoa hewa kwenye maji kabla maji hayajapita kwenye mita la sivyo utalipia hewa kila mwezi.
Unaondoaje hewa kwenye mita? Huku hutakiwi kuigusa na wenyewe wanasema mita zao zina uwezo wa kutenganisha hewa na kuhesabu maji pekee?

Suala la kuvuja ni kizingizio tu... moja ya sehemu nimekaa niliita DAWASA wakahakikisha hakuna sehemu inayovuja lakini bado bili haikuwa na uhalisia, maelezo waliyobaki nayo ni kulazimisha hayo ndio matumizi yangu
 
kuna suala la maji kuvuja na pia jambo ambalo wengi hawalijui ni suala la hewa kupita kwenye mita na inazungusha mita kama ilivyo maji. Unapaswa kuondoa hewa kwenye maji kabla maji hayajapita kwenye mita la sivyo utalipia hewa kila mwezi.
Unaondoaje hewa kwenye mita? Huku hutakiwi kuigusa na wenyewe wanasema mita zao zina uwezo wa kutenganisha hewa na kuhesabu maji pekee?

Suala la kuvuja ni kizingizio tu... moja ya sehemu nimekaa niliita DAWASA wakahakikisha hakuna sehemu inayovuja lakini bado bili haikuwa na uhalisia, maelezo waliyobaki nayo ni kulazimisha hayo ndio matumizi ya
Kujaza ndoo siyo kipimo sahihi, ile ndoo kubwa ikijaa maji ni zaidi ya lita 20.
Mkuu ndoo ni lita 20, inakuaje maji yanakuwa zaidi ya 20?🤔🤔 hata ingekuwa imezidi kama usenavyo ndio iwe ndoo 20?🤣🤣 the math aint mathing hapa
 
Same here, nimeitisha fundi aangalie kama kuna sehemu panavuja anasema hamna 🙌
Utaishia kuambiwa ni "Matumizi yako tu au uliacha bomba wazi" wakati hakuna kilichoongezeka na hujawahi kuacha bomba wazi
 
Back
Top Bottom