Bili yako ya maji mwezi Februari inaendana na uhalisia wa matumizi yako?

Bili yako ya maji mwezi Februari inaendana na uhalisia wa matumizi yako?

Huenda wamepandisha bei ya hizo unit zao, mim mwez huu nimeletewa bili ya 5000 na ni unit 3 ndzo nilizotumia.
 
Wakuu salam,

Bili za mwezi Februari zimetoka, jamani huku kwetu Mbezi Beach kila mtu anashangaa ubambikaji wa bili hizi. Yaani kwa kila mtu bili imeshoot kuliko kawaida wakati matumizi ni ya kawaida, sio kwamba ni shule au labda unafanya biashara ya kuuza maji.

Tena cha kushangaza zaidi ni kuwa maji yamekuwa ni ya kusuasua zana, mnakaa siku tatu nne hakuna maji, maji yakitoka presha ni ndogo sana yaani hata hayapandi kwenye matenki. DAWASA walitoa ushauri watu tuweke pump za maji lakini kutokana na presha ilivyo ndogo hata kuwa na pump ni kituko, maana zinakosa cha kubust, halafu eti bili inakuja umetumia unit 40, 50! Kivipi? Kwa maji yapi ya kufikia unit hizo?

Imagine kwenye nyumba mko watano, watatu hamshindi nyumbani, kuna safari za kufanya msiwepo nyumbani kwa wiki au hata zaidi, maji yanasua sua unaweza kusema kwa mwezi mmepata maji siku nzima bila kukata labda siku 3 halafu bili inakuja unit 40+, inaingia akilini kweli? Wizara ya Maji

Kama ndio mita zinahesabu upepo hii ya sasa imetia fora, itakuwa pump zinapigwa na kimbuka huko chini mpaka kupata units zote hizo.

Kwa upande wenu hali ikoje Wakuu? Bili zimekuja na uhalisia?

Wizara ya Maji
Dah ndugu niliona mm tu huku kino kumbe hadi mbez jambo tofauti ni kua kwetu hayakatwi ila bill imeshoot sijawah ona
 
Hii nchi tunaibiwa sana na watawala.mpaka tutakapopata akili ndo tutakombolewa
 
Unaondoaje hewa kwenye mita? Huku hutakiwi kuigusa na wenyewe wanasema mita zao zina uwezo wa kutenganisha hewa na kuhesabu maji pekee?

Suala la kuvuja ni kizingizio tu... moja ya sehemu nimekaa niliita DAWASA wakahakikisha hakuna sehemu inayovuja lakini bado bili haikuwa na uhalisia, maelezo waliyobaki nayo ni kulazimisha hayo ndio matumizi ya

Mkuu ndoo ni lita 20, inakuaje maji yanakuwa zaidi ya 20?🤔🤔 hata ingekuwa imezidi kama usenavyo ndio iwe ndoo 20?🤣🤣 the math aint mathing hapa
Tumia air valve
 
Back
Top Bottom