Bilionea mwingine kutoka jamii ya Kimasai aibuka nchini, ni mchimbaji wa Madini ya Rubi

Bilionea mwingine kutoka jamii ya Kimasai aibuka nchini, ni mchimbaji wa Madini ya Rubi

Mkuu acha kukalili hayo madini sio ruby pure yako mixer au ndo walewale note ya mia mbili mmeambiwa inauzwa million mia moja ukiuliza wapi utaambiwa dar nioneshe mteja hamna
Sawa hizo ton tano kwa yeye peke yake ametumia siku ngapi kuzitoa kuna juu jaman mnajua uzito wa ton tano na aziweke kusubir ton 5 hii nahisi kama tunapandishwa minazi ya rufiji sasa
 
Hizo Zina it was ruby zoisite zinapatikana longido,mundarara zinauzwaga kwa kg
Kila mawe upande wa grade inakuwaga n bei yake kwa kg kna kg 1 =25000 mpaka 500000 inategemea na quality
Kwa hyo kwa tani moja Kufika bln ni kawaida

Ova
Hii tani 1 kupata hata 30m ni kazi,2017 enzi mundarara imechanganya tipa ulikua unauziwa 30m ....ukienda kusort inaweza rudisha mtaji na faida kiduchu au kukata mtaji wote.watu wengi mitaji ilikata wengine mpka leo wanayo majabali nyumbani hakuna wateja
 
Mkuu acha kukalili hayo madini sio ruby pure yako mixer au ndo walewale note ya mia mbili mmeambiwa inauzwa million mia moja ukiuliza wapi utaambiwa dar nioneshe mteja hamna
NAAMINJ HATA WEWE HUJAELEWA ULICHOANDIKA,MKUU TANI 5 ZA RUBY HIVI UNAELEWA LAKINI AU NA WEWE NI MWANAKWAYA SAUTI YA TATU
 
Mabilionea wa hivyo walikua wengi awamu zilizopita Ila waliuza kimya kimya.
Ndio haya magorofa unayoona mjini yasiyo na maelezo
 
Ndugu mtanzania mwezangu TANI TANO za RUBY walizitoa shimoni na Crane ama
Aisee Kitoabu njoo mara moja utupe muongozo
Katika jambo la kudhalilisha wanataaluma na wajuvi wa mambo ya madini ni hiki kitu kilicholetwa hapa kuhusu 'eti tani 5 za madini' haiingii akilini.

Mtoa mata hajui au ni kilaza, kwenye haya madini ya Ruby kuna aina nyingi, kama
1.Ruby Gem hii huuzwa mpaka 2mil kwa gram na inategemeana na ubora na ukubwa.

2 .Ruby nyingine nadhani ni kama anavyotaka kueleza mtoa mada, ambayo ni mwamba unaweza ukapata kutoka kwenye mwamba na ukapata au kutoa uzani wa 5gram za Ruby Gem.

Sasa hizo 5ton sijui ni kitu gani au tuseme 1ton =1,000kg na hiyo bilioni 1.7=1,700,000,000 gawanya kwa 5,000kg ni sawa na 340,000/= au ameeleweka huyo jamaa, ahahaa😁
 
Hii tani 1 kupata hata 30m ni kazi,2017 enzi mundarara imechanganya tipa ulikua unauziwa 30m ....ukienda kusort inaweza rudisha mtaji na faida kiduchu au kukata mtaji wote.watu wengi mitaji ilikata wengine mpka leo wanayo majabali nyumbani hakuna wateja
Nakumbuka kuna mhindi mmoja alikuwa anachimbaga huko wakati huo alikuwa anayazoa
Haswaa

Ova
 
Mchimbaji mdogo mdogo wa Madini ya Ruby yaliyopo katika kata ya Mundarara wilayani Longido Mkoani Arusha Sendeu Laizer ameibuka kuwa tajiri katika sekta hiyo baada kupata tani tano za madini hayo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.7.

Hiyo ni mara ya pili kwa wachimbaji wadogo wadogo kupata utajiri kwani mchimbani mwingine alikuwa Sanniu Laizer aliyefanikiwa kupata madini ya Tanzanite yenye thamani ya zaidi ya bilioni 8.

Akizungumza na wataalam na watendaji wa sekta ya madini waliotembelea mgodi huo mmliki wa mgodi huo Gabriel sendeu Laizer amesema mafanikio hayo ni matokeo ya hatua zinazochukuliwa na serikali kuwajengea wachimbaji wadogo mazingira mazuri ya uchimbaji.

Laizer ni kijana wa pili kutoka jamii ya wafugaji wa kimasai kuibuka Bilionea kupitia madini katika kipindi cha kifupi wa kwanza akiwa ni kijana mwingine Saniniu Laser ambaye alipata kilo zaidi ya 11 za madini ya Tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Bilion 8.

Alisema na kuishukuru sekta ya madini hususani Rais Dr. John Magufuli kwa kuwathamini wachimbaji wadogo na kuwatetea hatua ambayo ndio iliyochangia mafanikio yake kwa sasa na sio vinginevyo.

Pia amewashauri wachimbaji wenzake wadogo wa madini kuendelea kuchimba bila kukata tamaa kwani kazi hiyo inahitaji uvumilivu na kujitoa kwa dhati.

Wakizungumzia hatua hiyo baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini hayo wamesema kupatikana kwa kiasi hicho kikubwa cha madini kimewaongezea ari ya kuendelea kuchimba japo wanasema wanakabiliwa na tatizo la mitaji na vitendea kazi ,

Mmoja wa wachimbaji wadogo katika eneo hilo Michael Lekule Laizer ambaye alikuwa mbunge mstaafu wa Jimbo la Longido na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} amesema upo uwezekano wa kunufaika na rasilimali hiyo kama taasisI za fedha zitaona umhimu wa kuwasaidia kwa kuwapa mikopo ya muda mrefu.

Viongozi wa vyama vya wachimbaji wa madini mkoa wa Arusha akiwemo Alfred Antony ambaye ni mwenyekiti wa chama cha wachimbaji na Jeremia Simion ambaye ni mwenyekiti wa wachimbaji wa kati wamesema wachimbaji wote wadogo wana ari ya kuchimba na wanafurahia mazingira waliyowekewa.

Naye Mkuu wa wilaya ya Longido ,Frank Mwaisumbe amewataka wachimbaji wadogo kuona umuhimu wa kuuunganisha nguvu pamoja ili waweze kupata vitendeakazi vya kuwawezesha kuchimba kisasa zaidi na kunufaika na rasilimali za madini ambayo sasa yame wekewa utaratibu mzuri wa kuhakikisha yanawanufaisha wazawa.

Aidha mwaisumbe pia amewashauri wachimbaji wadogo kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali ukiwemo kudhibiti utoroshaji wa madini ili yaendeleee kuwanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla.

Mtaalam wa kutoka wizara ya madini ambaye ni mjiolojia mwandamizi Mussa Shanyange amesema madini ya Ruby ni miongoni mwa madini yenye thamani kubwa ambayo yanapatikana kwa wingi katika eneo hilo

Kwa upande wake Kamishna wa Madini wa Mkoa wa Arusha (RMO), Aidan Muhando amempongeza Sendeu Laizer kwa kuona umuhimu wa kufanya uchimbaji kwa uwazi na kufuata sheria na taratibu zilizowekwa hatua ambayo imemuwezesha kupata mafanikio yeye mwenyewe , serikali na jamii kwa ujumla.

Hata hivyo amewataka wachimbaji wengine wenye leseni za kuchimba katika maeneo hayo ambao hawajaanza kuhakikisha wanaanza kuchimba ili kuongeza uzalishaji .

Amesema baadhi ya wachimbaji wamepewa leseni lakini hawachimbi utaratibu ambao haukubali na kama hatua hiyo itaendelea watalazimika kuchukua hatua ya kuyachukua maeneo hayo na kuwapa watu wengine wenye uwezo wa kuchimba

Wananchi wa Kijiji cha Mundarara wamesema hatua ya kupatikana kwa bilionea katika Kijiji chao imewapa matumaini makubwa ya kuanza kupata ufumbuzi wa matatizo mengi yanayowakabili

Kwa mujibu wa kamishina Madini ya Ruby pamoja na kupatikana katika wilaya hiyo ya Longido Mkoa wa Arusha pia yanapatikana wilaya za mkoa wa Tanga , na wilaya za mkoa Dodoma

Mwisho
Gharama za kuchimba Tani 5 za madini huenda zikazidi gharama ya Bili 1.7 kama uchimbaji ni wa Open space,!! Kuna walakini hapo...
 
Back
Top Bottom