Loftins
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 10,485
- 13,693
Fala wewe labda mamakoBaba Ako alikuwa mlevi ndo mana akakutoa wewe...wewe ni kizazi Cha kishenzi...**** ww
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Fala wewe labda mamakoBaba Ako alikuwa mlevi ndo mana akakutoa wewe...wewe ni kizazi Cha kishenzi...**** ww
Nusu kilo ya rubi tu imeshazidi bilioni moja uje useme tani? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tanzania hii wendawazimu wanaongezeka kwa kasi sana!
Na hiyo Ruby ya tani moja ipatikane kwenye dunia hii hii au wanaifananisha na yale mawe ya kutengenezea cement
Wewe ndio hujui. Ruby tani moja ni hela ambayo ni bajeti ya Tanzania kwa miaka mingi sanaKama hamjui vitu wakati mwengine ni kupita na kusoma comment za wenzio....
Mkuu, hata mimi nimemuwaza Kitoabu aje atupe mwanga kidogo. Tani tano sio mchezo!Ndugu mtanzania mwezangu TANI TANO za RUBY walizitoa shimoni na Crane ama
Aisee kitoabu njoo mara moja utupe muongozo
Kunywa maji ya bariidi mjomba,labda yatakusaidia kushusha hasira kidogoMtu mlevi ni mshenzi kabisa, kama wewe pia ni mlevi ni mshenzi pia.
Sasa kwanini wasipime hizo gram au kg za ruby baada ya kuchambua hayo mawe makubwa?kulikuwa na haja ya kutuambia hizo tani za mawe?au ndio utaratibu?Hapo wamepasua mawe makubwa makubwa halafu unaanza kulichambua kwa kulivunja ndio ukutane na viruby vidogo gram 1 au 2....unaweza kutumia miezi kuchambua huo mzigo ni kazi ngumu
Yaani uko kama mimi, kuchimba uchimbe wewe then uje na story za jiwe [emoji848], mimi huwa nahisi kuna utapeli hapo kama siyo propaganda. Tani tano walizitoaje ??Nikishaona mtu anaanza kutanguliza shukrani kwa awamu ya 5 na Rais basi kanipoteza.
Sitotilia maanani asilani!
Acha kurukaruka kama mahindi ya bisi, wapi kasema ni madini mchanganyiko? Yaani tani 5 =1.7 B?Mkuu acha kukalili hayo madini sio ruby pure yako mixer au ndo walewale note ya mia mbili mmeambiwa inauzwa million mia moja ukiuliza wapi utaambiwa dar nioneshe mteja hamna
Sina wasiwasi na fedha alizopata huyo bilionea. Wasiwasi wangu ni kuhusu huo uzito, tani tano za ruby ni uzito mkubwa sana. Ieleweke madini ya Vito hupata thamani yake kwa vile yanakuwa adimu na aghalabu uzito wake unakuwa katika gramu. Ili kupata tani tano za ruby, basi nafikiri mlima mmoja umesambazwa kabisa!Mchimbaji mdogo mdogo wa Madini ya Ruby yaliyopo katika kata ya Mundarara wilayani Longido Mkoani Arusha Sendeu Laizer ameibuka kuwa tajiri katika sekta hiyo baada kupata tani tano za madini hayo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.7.
Hiyo ni mara ya pili kwa wachimbaji wadogo wadogo kupata utajiri kwani mchimbani mwingine alikuwa Sanniu Laizer aliyefanikiwa kupata madini ya Tanzanite yenye thamani ya zaidi ya bilioni 8.
Akizungumza na wataalam na watendaji wa sekta ya madini waliotembelea mgodi huo mmliki wa mgodi huo Gabriel sendeu Laizer amesema mafanikio hayo ni matokeo ya hatua zinazochukuliwa na serikali kuwajengea wachimbaji wadogo mazingira mazuri ya uchimbaji.
Laizer ni kijana wa pili kutoka jamii ya wafugaji wa kimasai kuibuka Bilionea kupitia madini katika kipindi cha kifupi wa kwanza akiwa ni kijana mwingine Saniniu Laser ambaye alipata kilo zaidi ya 11 za madini ya Tanzanite yenye thamani ya zaidi ya Bilion 8.
Alisema na kuishukuru sekta ya madini hususani Rais Dr. John Magufuli kwa kuwathamini wachimbaji wadogo na kuwatetea hatua ambayo ndio iliyochangia mafanikio yake kwa sasa na sio vinginevyo.
Pia amewashauri wachimbaji wenzake wadogo wa madini kuendelea kuchimba bila kukata tamaa kwani kazi hiyo inahitaji uvumilivu na kujitoa kwa dhati.
Wakizungumzia hatua hiyo baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini hayo wamesema kupatikana kwa kiasi hicho kikubwa cha madini kimewaongezea ari ya kuendelea kuchimba japo wanasema wanakabiliwa na tatizo la mitaji na vitendea kazi ,
Mmoja wa wachimbaji wadogo katika eneo hilo Michael Lekule Laizer ambaye alikuwa mbunge mstaafu wa Jimbo la Longido na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} amesema upo uwezekano wa kunufaika na rasilimali hiyo kama taasisI za fedha zitaona umhimu wa kuwasaidia kwa kuwapa mikopo ya muda mrefu.
Viongozi wa vyama vya wachimbaji wa madini mkoa wa Arusha akiwemo Alfred Antony ambaye ni mwenyekiti wa chama cha wachimbaji na Jeremia Simion ambaye ni mwenyekiti wa wachimbaji wa kati wamesema wachimbaji wote wadogo wana ari ya kuchimba na wanafurahia mazingira waliyowekewa.
Naye Mkuu wa wilaya ya Longido ,Frank Mwaisumbe amewataka wachimbaji wadogo kuona umuhimu wa kuuunganisha nguvu pamoja ili waweze kupata vitendeakazi vya kuwawezesha kuchimba kisasa zaidi na kunufaika na rasilimali za madini ambayo sasa yame wekewa utaratibu mzuri wa kuhakikisha yanawanufaisha wazawa.
Aidha mwaisumbe pia amewashauri wachimbaji wadogo kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali ukiwemo kudhibiti utoroshaji wa madini ili yaendeleee kuwanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla.
Mtaalam wa kutoka wizara ya madini ambaye ni mjiolojia mwandamizi Mussa Shanyange amesema madini ya Ruby ni miongoni mwa madini yenye thamani kubwa ambayo yanapatikana kwa wingi katika eneo hilo
Kwa upande wake Kamishna wa Madini wa Mkoa wa Arusha (RMO), Aidan Muhando amempongeza Sendeu Laizer kwa kuona umuhimu wa kufanya uchimbaji kwa uwazi na kufuata sheria na taratibu zilizowekwa hatua ambayo imemuwezesha kupata mafanikio yeye mwenyewe , serikali na jamii kwa ujumla.
Hata hivyo amewataka wachimbaji wengine wenye leseni za kuchimba katika maeneo hayo ambao hawajaanza kuhakikisha wanaanza kuchimba ili kuongeza uzalishaji .
Amesema baadhi ya wachimbaji wamepewa leseni lakini hawachimbi utaratibu ambao haukubali na kama hatua hiyo itaendelea watalazimika kuchukua hatua ya kuyachukua maeneo hayo na kuwapa watu wengine wenye uwezo wa kuchimba
Wananchi wa Kijiji cha Mundarara wamesema hatua ya kupatikana kwa bilionea katika Kijiji chao imewapa matumaini makubwa ya kuanza kupata ufumbuzi wa matatizo mengi yanayowakabili
Kwa mujibu wa kamishina Madini ya Ruby pamoja na kupatikana katika wilaya hiyo ya Longido Mkoa wa Arusha pia yanapatikana wilaya za mkoa wa Tanga , na wilaya za mkoa Dodoma
Mwisho
Una bahati sana nilikuwa na classmate miaka fulani ambaye ni ana akili nyingi na mstaarabu sana.Kunywa maji ya bariidi mjomba,labda yatakusaidia kushusha hasira kidogo
Wewe ndio hujui. Ruby tani moja ni hela ambayo ni bajeti ya Tanzania kwa miaka mingi sana
Sina wasiwasi na fedha alizopata huyo bilionea. Wasiwasi wangu ni kuhusu huo uzito, tani tano za ruby ni uzito mkubwa sana. Ieleweke madini ya Vito hupata thamani yake kwa vile yanakuwa adimu na aghalabu uzito wake unakuwa katika gramu. Ili kupata tani tano za ruby, basi nafikiri mlima mmoja umesambazwa kabisa!
Ndio serikali yetu ilivyo comedian,hayo wanatoa bei kabla hata hawajasort mawe hayo,thamani yake iko chiniSasa kwanini wasipime hizo gram au kg za ruby baada ya kuchambua hayo mawe makubwa?kulikuwa na haja ya kutuambia hizo tani za mawe?au ndio utaratibu?
Hiyo ni ruby thamani yake ni ndogo sana,huo mwamba umeungua ruby nzuri iko tunduruyani tani tano nilitegemea jamaa apewe hata tilion 50 hivi basi kitoabu anapoteza muda tu huko msumbiji
Ruby ya Mz ipo juu kuliko Tzyani tani tano nilitegemea jamaa apewe hata tilion 50 hivi basi kitoabu anapoteza muda tu huko msumbiji
Kaombe ukoo kwa wamasai.Itabidi na mimi nibadili jina nijiite "KING LAIZER".
Hivi Marley Dollar na yeye si anachimba Ruby? Simsikii kabisa siku hizi.
Hahahaa ngoja niongee na rafiki yangu yero subai.Kaombe ukoo kwa wamasai.
Ile Range yangu ushaagiza au bado?