Kwa sisi tuliopita kwenye machimbo ya Ruby kule Montpuez kwa mzee Filipe Jacinto Nyusi in the Republica de Mozambique hili swala kidogo tunaweza lidadavua.
Tuanzie kwanza bei ya Ruby
Bei ya ruby ina range kuanzia $10 mpaka $12,000 kwa carat au inaweza ikashuka mpaka kufikia $ 50/kg
,na hapa inategemea na hiyo ruby imechimbwa nchi gani maana kuna nchi ukichimba ruby ukapeleka kwenye world market hauwezi kuuza kabisa yaani ni priceless japo ni ruby hii kitu kwa sisi watu wa madini tunawezaita "blood mineral " pia tunaweza kuita "blood ruby" katika kesi yetu japo mara nyingi neno blood limekuwa ikitumika kwa kesi ya diamond kama tulivyoona "blood diamond" za kule Seara Leone ambako kulikuwa na machafuko but always this blood minerals are priceless sababu inatoka kwenye migodi iliyomwaga damu na nchi zenye umwagaji damu,au nchi zinazofadhiri vikundi vya wahasi.
Na wazungu walivyo wafitini hawa mabeberu wamezigawa ruby kwenye madaraja ya thamani kutokana na nchi zinazochimbwa kama ifuatavyo.
1.Burma au Myamar
2.Thailand ,Cambodia
3.Mozambique ,Madagascar
4.Kenya,Tanzania
5.Afganstan and Parkistan
Kwa vigezo vya ubora ,usambazaji na uchimbaji,na brand.
Na hii ndio iliyopelekea wabongo wengi kukimbilia machilbo ya ruby kule Montpuez Msumbiji japo Tz kuna ruby deposit nyingi,ila kuna kautofauti kidogo ka thamani ya ruby zinazochimbwa nchi hizi mbili tofauti katika same condition.
Ila vigezo vingine vinavyotumika kupima bei ya ruby kitaaramu tunaita 4C's +OT
1.Clarity-uangavu
2.Color-rangi hapa nyekundu inakuwa ghari (expensive)kuliko purpish red,orangish red,pinkish red
3.Carat weight-huu ni uzito na 1kg inakuwa sawa na 5000carat
4.Cut-hii ni shape baada ya ruby kukatwa zenye shape ya pembe kumi,duara,mraba,n.k hizi zenye shape ya pembe kumi ,duara,na mraba zinakuwa ghari sana
5.Origin - hapa tunazaungumza asili ya hiyo ruby imechimbwa wapi,mgodi gani,kampuni gani n.k.
6.Treatment level-hapa tuna refer njia zilizotulika katika uchenjuaji mpaka kupata refined ruby.
Pia kuna mambo kibao kama inclusions n.k ila ukibahatika kupata kitu inaitwa " pigeon blood ruby" wewe ni mtu mwengine kwenye hii dunia,ruby hizi zina bei kuliko hata diamonds unazozijua ww hizi ndio zile watoto wa uswazi wanaziita ruby birihani au ruby VPN yani hazina chenga pesa nje nje.
Twende kwenye point sasa
Bei ya ruby inaanzia $10 mpaka $12,000 kwa carat kwa kuzingatia vigezo tajwa hapo juu,pia inaweza ikawa $50 /kg .
Kumbuka 1kg ni sawa na 5000 carat .
Tukizingatia vigezo hivi hiyo 1.7Bilion inaweza ikawa ndio halali yake ,maana kuna makato ya kodi n.k.