Bilionea wa China, Jack Ma adaiwa kutojulikani alipo kwa zaidi ya miezi miwili tangu alipoikosoa Serikali na Chama Tawala

Bilionea wa China, Jack Ma adaiwa kutojulikani alipo kwa zaidi ya miezi miwili tangu alipoikosoa Serikali na Chama Tawala

Kampuni yake imelaumiwa na serikali hivi karibuni kua inahujumu makampuni mengine kwa kuweka masharti tofauti kwa wateja wanaotumia mtandao wake: Pengine anahojiwa...[emoji848]
Nahisi atakuwa alikataa kuireplace huduma yake ya Alipay kwa digital yuan kama serikali ya Beijing inavyotaka
 
BILIONEA wa China, Jack Ma inasemekana hajulikani alipo baada ya kutoonekana hadharani kwa zaidi ya miezi miwili.

Aidha, alishindwa kuhudhuria onyesho lake la ‘Africa’s Business Heroes,’ Novemba 2020, na aliwakilishwa na mmoja wa wakurugezi wa kampuni la Alibaba Group.

Kutoonekana kwake kunakuja wakati serikali ya China inazidi kuzibana biashara zake, baada ya bilionea huyo kuukosoa mfumo wa serikali katika kudhibiti biashara.

Kati ya mwaka 2016 na 2017, wakati wa zoezi la kuupiga vita ufisadi nchini China, mabilionea kadhaa walipotea, ambapo wengine walikuja kuonekana wakisema walikuwa ‘wakiisaidia serikali’ ambapo wengine kamwe hawakurejea.

============================

Hong Kong: Billionaire Ant Group Co. co-founder Jack Ma skipped a recent taping of an African TV program he created, spurring speculation online about his whereabouts and the outcome of an investigation into his internet empire.

Ma hasn’t been seen in public since Chinese regulators torpedoed Ant’s $35 billion IPO, then tightened fintech regulations and launched an antitrust probe into Alibaba Group Holding Ltd. — all in a span of days. The Financial Times on Friday reported that the showrunners of the Shark Tank-like “Africa’s Business Heroes” replaced him as a judge in a November telecast and removed his photo from the show’s website, around the same time Ma delivered his now-infamous rebuke of the “pawnshop” mentalities of government overseers.

The flamboyant Ma — long a fixture on the international conference circuit — all but vanished from public view thereafter. As of early December, the man most closely identified with the meteoric rise of China Inc. was advised by the government to stay in the country, a person familiar with the matter has said. An Alibaba spokesperson said Ma couldn’t attend due to scheduling conflicts, declining to comment specifically on the executive’s whereabouts.

Ma may have his hands full dealing with escalating scrutiny. The crackdown on Ma’s companies has set in motion a string of regulatory decrees that threaten to reshape the landscape for China’s online operators. Regulators are now studying plans to force Ant to divest equity investments in some financial companies, curbing the company’s influence over the sector, a person familiar with the matter has said. –Bloomberg
 
Kampuni yake imelaumiwa na serikali hivi karibuni kua inahujumu makampuni mengine kwa kuweka masharti tofauti kwa wateja wanaotumia mtandao wake: Pengine anahojiwa...[emoji848]
wewe sasa ndio uko sahihi juzi kati serikali ya china ilikua inalalamika kuwa jack anaikosoa sana watakua wameishampoteza kama waliweza kum fix bo xilai hawawezi kumshindwa huyu bo xi lai ndio alitakiwa aje kuwa rais wa China badala ya huyu xi ji ping
 
Kama bilionea wa nchi anaweza kupotea miezi kadhaa na kusiwe na taarifa yeyote ile kutoka mamlaka husika kuhusu usalama wake, basi ni hatari sana na ni doa kubwa kwa serikali kuhusu usalama wa kibiashara na uwekezaji katika nchi husika.

Jaribu kufikiri, Marekani: Jeff Bezos wa Amazon ama Zuckerberg wa Facebook asijulikane alipo kwa miezi kadhaa na kusiwe na taarifa kuhusu usalama ama juhudi za kuhakikisha usalama wake kwa kile kinachoelezwa kuwa ni baada ya kuikosoa serikali yake, hali ingekuwaje?

Maana yake ni kuwa, hakuna aliye salama!

Hili linatishia usalama wa sekta za uwekezaji sababu hakuna mwekezaji timamu anayeweza kuwekeza chochote katika mazingira ama nchi bila kuwa na uhakika wa usalama wake na usalama wa kile anachokifanya.
 
Ana angalia Movie Mpya imetoka inaitwa " KISS OF THE DRAGON 2"
 
1. Mwanzoni mwa mwaka jana,Serikali ya China ilichukuwa umiriki wa kampuni yake yote.

2. October 2020 akiwa kwenye maojiano na vyombo vya habari alitoa tuhuma kuwa Serikali ya China ina sera kandamizi zinazo leta vikwazo kwa wabunifu.

Baada ya hapo ajaonekana tena.
Yupo lupango tu,serikali ya Kikoministi ya China hairuhusu challenge. Kwa namna hiyo yuko chuo cha mafunzo(jela baridi), akifundishwa kutii mamlaka bila shurti.
Kama kampuni yake imechukuliwa na serikali,basi yeye atastaafu ,ndio China na labda serikali ndio ilikuwa nyuma ya ustawi wa kampuni hiyo Alibaba
 
Yupo lupango tu,serikali ya Kikoministi ya China hairuhusu challenge. Kwa namna hiyo yuko chuo cha mafunzo(jela baridi), akifundishwa kutii mamlaka bila shurti.
Kama kampuni yake imechukuliwa na serikali,basi yeye atastaafu ,ndio China na labda serikali ndio ilikuwa nyuma ya ustawi wa kampuni hiyo Alibaba
Source!???
 
Back
Top Bottom