Mkuu, Unaweza kuishi bila pesa kweli, au una maanisha utajiri??Haya maisha ukifanikiwa kujiweka mbali na tamaa ya pesa utaishi kwa amani sana, bahati mbaya maskini wengi hatuwezi kuishi hivyo, kwetu kila siku ni mitihani inayohitaji pesa.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Msimpangie cha kufanya, hizo ni pesa zake, maskini wa Africa wanatamani hizo pesa, tafuteni pesa zenuππ, Pesa mwana haramu,,, anasubili mpaka akate moto kwanza.
Kabisa mkuu.Msimpangie cha kufanya, hizo ni pesa zake, maskini wa Africa wanatamani hizo pesa, tafuteni pesa zenu
Hili nalo neno...Kwanini asiwape mwenyewe kabla hajafa?
πππβ πWewe pia si uko hai?
Kwa nini hugawi mali zako kwa maskini?
Huwezi kumpangia mtu namna ya kutumia hela zake.
Acha akili za kimaskini, nini maana ya urithi?Ni unafiki tu..kwann asiwape sasa hivi
Acha akili za kimaskini, nini maana ya urithi?Kwanini asiwape mwenyewe kabla hajafa?
Acha akili za kimaskini, nini maana ya urithi?Hili nalo neno...
Zina masharti pesa[emoji1787]
πAfrica hakuna tajiri, matajiri wa Africa wamezishikia Bank hela.
Kwa nini?Ni kweli, lakini hata tuwe na hela nyingi, hatuwezi fikia hatua hiyo..
Hasaa BurundiKwani hana mke, watoto na ndugu wa kugawiwa hizo mali mpaka atake zitapanywe akifa? Kama vipi atafute nchi moja afrika iliyo masikini na wale masikini kabisa hohahe wagawiwe huo utajiri wake.
Sasa povu la nini, stress tu zinakusumbua...Acha akili za kimaskini, nini maana ya urithi?
wenye haki ya kurithi hizo mali ni familia yake Warren kwanini hawapi kabla hajafa?
babaako anaeza kukuachia nyumba kabla hajafa? jinsi babaako alivyo na uchungu na hiyo nyumba anavyoiona hiyo nyumba ndo utambulisho wake akiwa hai ndio maana hawezi kukurithisha kabla hajafa, labda kwenye makaratasi tu lakini kuimiliki ni mpaka afe.
the same kwa Warren hizo ni mali alizitafuta kwa jasho lake ana uchungu nazo na ndio utambulisho wake mpaka kufa
mtu kaamua nikifa urithi wangu wagaiwe wenye uhitaji mmatumbi mmoja anaita unafki, shwain
Kwa sababu ya kauli yako, "...tupo radhi...", nakushauri uachane na hiyo tabia mkuu. Wewe ukiacha, na wengine watafuatia. (Nimekutania kwa sababu naamini huna tabia hiyo).AFRICA Ni wachoyo sana, tupo radhi kuchangia msiba, kuliko akiwa bado yupo hai anaumwa
πππβ πππWazungu kuwa nao sawa ni mbingu na ardhi
Wao kwanza ni waaminifu na wamejifunza katika maisha haya haya waafrika tunayoishi
Mfumo wa maisha ni tofauti kabisa
Mwafrika anapeleka fungu la mshahara kanisani wakati mzungu anahakikisha wana Charities nyingi sana kutoka taasisi mbali mbali na wanachangia kila mwezi au kila wakati wanapoona tangazo na hela zinaenda kwa walengwa
Kwa mfano Charities za Cancer research mpaka maduka ya mitumba wanayo na wanaopeleka madukani ni wananchi hata mimi nimepeleka sana
Pia wanasaidia kila kitu usione wana kila kitu sio yote wanapata kutoka serikalini hasha
Vingine wanajitolea sana tena sana mpaka Africa misaada inayokuja sio ya serikali tu bali wananchi wanachanga sana
Wakisikia punda wanateswa wa kwanza kuchangia ni wao
Miradi kama WaterAid ni hela wanazochanga hata Red cross inafadhiliwa na watu kwa kutoa
Sasa mwafrika hela za kufa na kuzikana mmepitia, za pensions mmepitia
Shule inapigwa picha imekandikwa na matope juu nyasi na watoto hawana hata madaftari
Hapa nikisema tuchangie na mimi naanza na laki 5 utasikia unaambiwa hiyo sio kazi yetu ni kazi ya serikali
Sasa lini mtajua charity starts at home
Kwanza tujue kujisaidia wenyewe bila kusubiri kila kitu serikali wakati sisi ndio nchi yetu
Maendeleo ya wazungu ni hizo Charities pia maana ina misaada mikubwa sana kwa watu
Leo nikikosa pa kulala naweza kwenda mahali nikapata pa kulala kiasi serikali inanitafutia sehemu tena bure
Majuzi mmoja kasema uchafu umejaa sehemu anayoishi eti wanasubiri waondolewe
Mkuu suala hili ni Kwa watu weusi, na imekua kama desturi hapa Tanzania, Mwenyezi mungu atuepushe na kikombe hiki.Kwa sababu ya kauli yako, "...tupo radhi...", nakushauri uachane na hiyo tabia mkuu. Wewe ukiacha, na wengine watafuatia. (Nimekutania kwa sababu naamini huna tabia hiyo).
Ni ubinafsi mkubwa sana. Mtu anaweza akaomba asaidiwe hela ya matibabu asipate, ila mtu huyo huyo akifa, hufanyiwa mazishi ya kifahari.
Watu wenye tabia kama hiyo hawana tofauti na "wachawi!"