Bilioni 240+ Zatolewa kwa Wananchi Kupitia Mikopo ya asilimia 10– Je, Wewe Umewahi Kunufaika?

Bilioni 240+ Zatolewa kwa Wananchi Kupitia Mikopo ya asilimia 10– Je, Wewe Umewahi Kunufaika?

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,441
Reaction score
1,050
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa kipaumbele kwa maendeleo ya wananchi kwa vitendo, hususan kwa kuwainua kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri isiyo na riba.

Mikopo hii imetolewa kwa makundi maalumu ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020–2025.

Kupitia mpango huu, serikali imefanikiwa kutoa mikopo yenye jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 240.9, ikigawanywa kama ifuatavyo:

👩‍🦰 Wanawake – Shilingi bilioni 99.5

👨‍🦱 Vijana – Shilingi bilioni 96.3

♿ Watu wenye ulemavu – Shilingi bilioni 45.1

Mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba ni moja ya mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kutekeleza Ilani ya CCM 2020–2025. Kwa kuwapa wananchi mtaji bila riba, serikali imeweka msingi imara wa maendeleo jumuishi na ya kweli. Hii ni hatua ya kuendelea kujenga taifa la uchumi imara, unaojikita kwenye uzalishaji na ushirikishwaji wa wananchi wote – bila kumwacha mtu nyuma.

#MamaAnafanikisha
 
Tatizo sio kuzitoa Tatizo je zinapotolewa kuna ufuatilaji wa kina ili kuwafikia walengwa au ni mishe za kufinyiana pande tu?🤔
 
Tulijaza form toka mwaka jana mwezi wa 8 mpaka leo kimya, na acount tulishafungua...
Watu wamejikatia tamaa wanafanya mambo mengne
 
Hawara yangu aliomba ..intro kwanza usiasa kibao,, Yan vinavyoitajika ni vingi kuliko, Bado usumbuliwe, vyote wakakamilisha na mashosti wenzake mwisho wa siku wanaambiwa eti hawajakidhi vigezo , na waliokuja kukataa ni ngazi ya mkoa ..huku chini utapitapita ila kwa tabu na mateso , unakuja kuishia ngazi ya wilaya /mkoa ...wanaopata ni kutokana na urasimu tu na rushwa ..Kuna mengine siwez sema..
 
Hahaha hizi hesabu za jumla jumla we jiulize nani kazipata?

Labda jeshi la mama uwt na uvcc.
 
Back
Top Bottom