Bilioni 650 za DP World Zamkuna Makala. Zaongeza Ufanisi wa Bandari ya Dar kutoka Makasha 7,000 Hadi Makasha 20,000

..ndio nimekwambia SHERIA imekiukwa.

..kulipaswa kuwe na Zabuni, halafu makampuni yatie nia, na mshindi apatikane baada ya mchakato.

..sasa hivi tulivyofanya tuna uhakika gani kama Adani, au Dp, wametupa offer nzuri kuliko wote?
Abani alitangazwa mpaka kupatikana kwake, kwenye magazeti ya serikali lilikuwepo tangazo lake. DPW nimekwambia mara elfu moja sasa, kwamba nature ya biashara anayoifanya ilimpa yeye moja kwa moja nafasi ya uwekezaji.

DPW ana miliki bandari za UK na India nitafutie kampuni nyingine ya hadhi yake katika ulimwengu mzima wa biashara za shipping kwa sasa.
 
Mnajadili haya mambo kihisia na wote hamjui hata mnachojadili. Nani nawaambia tender ya kuendesha ghati namba 8-11 haikutangazwa?
Nguvu ya kujadili msichokijua mnaitoa wapi?

..kuna madai kwamba Adani alianza kazi kabla ya zabuni kutangazwa.

..yaani hiyo zabuni imetangazwa kihuni wakati anayetakiwa anajulikana.

..vilevile kama Adani alipata kazi kupitia zabuni kwanini Dpw yeye kupewa mkataba kibabe?

Cc Steven Joel Ntamusano
 
Mhh Kama ni mwanahalisi (gazeti) wameandika hivo then tuna waandishi bogus kabisa! Wameshindwa hata kuingia kwa website ya TPA na kuona meli zinasubiri kwa muda gani ili kushusha mzigo?😭😳😳😳
Hii hapa chini( attached) ni ratiba ya meli zinazosubiri kushusha mzigo, utaona kuna meli ina siku thelathini (30) na bado haijaingia/kupata nafasi ya kushusha mzigo
 

Attachments

  • IMG_0076.png
    442.4 KB · Views: 1
Asante kwa kunisahihisha. Nilichukulia ni sawa na ile ya magati namba 3-7 aliyopewa DPW.
Sawa mkuu, lakini mbona bado unakosea? Maghati 3-7???
Sijui kama unaelewa kweli hili jambo, lakini bado nauliza kwa nn unajadili Jambo ambalo linaonyesha pengine hulifahamu?
 
Mbona mnahangaika sana bila sababu za msingi?

Nimesema DP World ameingia Kwa mtindo wa Serikali Kwa Serikali kusaini MoU na hivyo Kuna preferential treatments Kwa sababu za kimahusiano baina ya Nchi kama tuu Arab Contractors wa Bwawa la Nyerere.

Huyo mwingine Tanzania na India Hazina kubaliana rasmi so alitumia open tendering.

Mwisho Cha muhimu ni matokeo au mchakato?
 
Kwanza mm nimewarekebisha mliposema haikutangazwa. Ukweli ilitangazwa

Kwa nini DP haikutangazwa, hiyo sijui ndio maana sikuigusa.
 
DP world ghati namba 8-11??

Sema huu mjadala wenu mmechanganya mambo hadi basi aisee
 
wajinga ndio wataamini uekezaji ndio uongeze makasha?hao wateja wametokea wapi... walikuwa wateja wa bandari gani wa kaopt kushushia dar..unaweza kuta wateja wa holili ,tanga na mtwara wamelazimishwa kushushia dar kontena zao....maana mmiliki ni mjomba....niishie hapo
 
Akili huna wewe usiyefuatilia habari za maana. Kesi ya kupinga DPW asipewe uendeshaji kule Mbeya, Mwabukusi na wenzake waliangukia pua ndio SSH akaamuru mchakato wa kumkabidhi hayo magati namna 8-11 uanze mara moja.
Haya mnaandika kwa confidence huwa mnayatoa hewani? Dp world ghati 8-11????

Huu mjadala wenu kiboko aisee
 
DP world ghati namba 8-11??

Sema huu mjadala wenu mmechanganya mambo hadi basi aisee

..wanaotetea uchafu ndio wanachanganya mambo.

..sasa sio tunaowapinga tunaonekana tunashiriki kuwachanganya wasomaji.

..kuna kipindi tulikuwa tunadanganywa kwamba Dpw wameletwa kuwa-replace Ticts.
 
Kampuni zingine zenye hadhi kama DP? Mbona zipo nyingi.
PSA
Hutchison ports
Cosco
China merchants ports. (Hawa ndio walitaka kuja kujenga bagamoyo port kwa trillioni 20)

Mkuu Kuna sababu nzuri ya serikali yetu kuwapa DP world.
Bado nasisitiza tusiandike kitu hatukijui vizuri hasa kwenye vitu technical
 
..wanaotetea uchafu ndio wanachanganya mambo.

..sasa sio tunaowapinga tunaonekana tunashiriki kuwachanganya wasomaji.

..kuna kipindi tulikuwa tunadanganywa kwamba Dpw wameletwa kuwa-replace Ticts.
Sio kweli, DP world hajareplace ticts. Mara nyingi huwa nakuambia choice variables awe anaandika vitu ambavyo anavijua, sababu anachoandika haandikii watu wajinga

Pia ni jambo la ajabu kuandika na kuzungumza vitu technical ambavyo mtu huvijui kabisa
 
Sio kweli, DP world hajareplace ticts. Mara nyingi huwa nakuambia choice variables awe anaandika vitu ambavyo anavijua, sababu anachoandika haandikii watu wajinga

Pia ni jambo la ajabu kuandika na kuzungumza vitu technical ambavyo mtu huvijui kabisa

..wanaotetea huo uchafu huwa wanakuja na mambo mengi.

..kuna watu wako hapo kwa malengo maalum ya kupotosha, na kuharibu mijadala yetu.
 
..hoja zako zinaweza kuungwa mkono au kupingwa bila kujali kama umekosea namba za gati zinazozungumziwa huko bandarini.
Bila kujua dp world ana operate wapi sasa yote mtajadili si itakua ni hisia?
Hujui mchezaji anacheza namba gani, lakini unataka kumjaji? Si ndio itaanza kulalamika kwa nini bakari mwamnyeto hafungi magoli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…