Billboard yametoa orodha yao ya Rapa bora wa muda wote

Billboard yametoa orodha yao ya Rapa bora wa muda wote

Mbona inajulikana wazi kwamba jay z huwa anatoa hela nyingi sana kwa hizi platform hasa Billboard na Vibe hili aendelee kupewa promo na hata Grammy inasemekana jamaa anawatoa mamilioni ya dola wampe promo za kutosha ..ona kama hapo Wamemuweka Jay-Z katika 1, Kendrick Lamar katika 2, Nas 3, Tupac 4, Eminem katika 5 na Biggie katika 6 kwa ajili ya 50 bora Rappers of All Time List.

Kisha wakawa na ujasiri wa kuzungumza kuhusu Mapungufu ya 2pacs kama rapper lakini hawakuwahi kugusia ukweli kwamba marapa wengi kwenye orodha hii hawawezi kamwe kutengeneza ngoma kali kama Street Fame. Hawakutaka kumgusia Jay kuiba Rhymes nyingi za Biggie na nyimbo nzima kutoka kwa Ice T na 2Pac.

Hawakutaka kugusia kwamba Jay na Kendrick wamekuwa na career ya muda mrefu tofauti na miaka ambayo pac na biggie wamekuwa kwenye game na kufanya makubwa, Jay-Z amekuwa kwenye gemu tangu 1986 na kipindi chote hicho walipokuwa hai kina Biggie, Pac na Eazy-E hakuwahi hata kuwasogelea kwa ubora

Jay-Z kafanya mengi lakini tuseme ukweli, kulikuwa na gap kubwa kwenye mziki wa Rap baada ya kupoteza magwiji 3 miaka ya nyuma huko. Si hivyo zamani pia kulikuwa na battle ya Big L na Big Pun ambalo jay z hata hakulisogelea kwa ubora lakini halikwenda mbalo kwani wasanii wote wawili pia walifariki. Jay pia hakuwahi kupata Diamond plaque yoyote ktk mauzo ya kazi zake. Eminem ana 3 na Pac ana 2 huku Makaveli akiwa anafuata.
au tufanye kwamba Nas hakutoa albamu 4 mfululizo huku Jay akiweka mstari mmoja tu ktk battle yao ..Na tusifanye kama Nas hakushinda vita yake dhidi ya Jay na Ether. Billboard ni kituko sana. Pac is the greatest of all time
 
Iwe ni hot 100,award nomination,award winner....
Nkiwaona wapo 3 bora,jay z,kendrik lamar,tylor swift,beyonce,lil baby...huwa sifuatilii concert/event kabisa...
 
Back
Top Bottom