Bima ya afya kutoka jubilee

Bima ya afya kutoka jubilee

Sababu nimejaribu angalia outpatient ni ndogo sana 1.5mil max kwa mwaka ni ndogo sana.

NHIF nikilipa kifurushi kikubwa cha 576,000
Natibiwa bila kusumbuliwa hapo naepuka Agakhan pekee ila hosptal zote naenda....

Jaribuni weka ukweli ili mtu asijekata afu akaingia gharama
Mpaka kuweka hizo gharama hawajakurupuka mkuu, zinatosha kabisa na unapata full dozi Bila ya kuongeza kiasi chochote ni vile mtu anaichukulia hiyo hela kijujuu tu lkn nakwambia hakuna mtu aliyewahi kuambiwa outpatient ama huduma nyingine imekataa katikati ya mwezi hivo hawezi kutibiwa .

Kwanza tunamadaktari ambao Huwa wanacontrol hizo bima kwa mteja ili asije akaongezewa gharama ambazo si halisi na anachoumwa maana ukumbuke hosp Nazo zinahitaji kufanya biashara unaweza enda na kadi inapimwa malaria mwisho wasiku wanakata dawa za maradhi mengi mgonjwa unakuwa hufahamu ,
Ila sie tunautaratibu wa kufuatalia Hali ya mgonjwa Hadi pale anapokamilisha matibabu

Na unaweza kufuatalia statement yako kila mwezi ili kuona muenendo wa kadi yako kama unahitaji na ndio maana ninasema ni wewe kuangalia wapi unapata huduma nzuri na kwa kiwango Bora zaidi



Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Mi ningetaka just kuuza wala nisingekushauri kwanza maana tunazo Hadi za laki mbili na elfu 61 ambayo ndio gharama ya chini kabisa.

Lkn nakuelewesha wewe mwenyewe ndio ujipime wapi ni Bora zaidi tena nakupa na lists ya hosp kwanza uangalie kwahyo unaangalia na eneo lako wapi utaweza kupata huduma kwa urahisi zaidi Bila ya usumbufu na kwa ubora wa Hali ya juu.



Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Upigiwe tena!!?

Futa haya maneno sasa "Karibuni sana, kwa anayehitaji maelezo zaidi unakaribishwa kuuliza na nipo hapa kwaajili ya kuwajibu wote."
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]dah madogo wa bongo kwa kuhoji nimewavulia kofia. CCM wajiandae kutolewa madarakani. Hiki kizazi kinahoji balaa na wanamaswali ya kinoko balaa.
 
Bima yenu unatibiwa Agakhan Hospital au ni kwenye hospital za michongo?

Kama Baba+Mama+watoto wawili ni 1.09m ,je ukiongeza mtoto mmoja inabidi uongeze 440k? Mbona watoto mmeweka wachache sana wakati mnajua familia za kiafrica hamna hamna mkono(watoto wa 5).
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ungeweka kila kitu wazi ili usijieleze sana...

Mf 440,000
Nitatibiwa hadi kiasi gani kwa mwaka kwa outpatient?
MRI, CT Scan, Operation
Dental, Optometry etc

Nina hakika huwa mna bronchures zinazoelezea kila kitu...

Usipende pigiwa simu wakati uwezo wa kueleza upo
Watoa huduma wetu especially dawati la mteja huwa hawapo tayari kisaikolojia kwa kazi yao.

Huwa wanaona ni kazi rahisi tu ya kuongea na mteja ila kuna ule muda wakigongwa maswali ya ugoko utaona wananuna.
 
Ili uweze kutibiwa hospitali ya aghakan unatakiwa ukate bima kubwa zaidi ya hiyo ambayo inaanzia mil 1 na kuendelea mkuu,

Ila hiyo huwezi na ndio maana nimejaribu kufafanua kila mahali.

Bima zetu zipo kwa ajili ya kucover watu wote wenye kipato cha juu, kati na cha kawaida na ndio maana mteja kabla hujakata bima Huwa napenda nikushauri kwanza.

Halafu wewe mwenyewe ndio utafanya maamuzi kulingana na bajeti yako.

Hapo umenielewa nafikiri

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Watoa huduma wetu especially dawati la mteja huwa hawapo tayari kisaikolojia kwa kazi yao.

Huwa wanaona ni kazi rahisi tu ya kuongea na mteja ila kuna ule muda wakigongwa maswali ya ugoko utaona wananuna.
Karibu upate huduma Bora kiongozi, na usisite kuuliza pale unapohitaji ufafanuzi nipo hapa kwaajili ya kujibu mashaka yote.

Karibu sana

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Hapo utachagua Moja wapo. Daraja la kwanza na la pili nje ya nchi za Africa, la tatu na nne ndani ya nchi zote za Africa Mashariki.
Vipi kwa familia hii?
Baba miaka 45
Mama miaka 31
Watoto wawili: Miaka 6 na wa mwisho miezi 7: Leta bei ya jumla kwa Premier, Executive and Royal
 
Mkuu unahitaji documents gani? Na je inachukua siku ngapi hadi kupata kadi ya bima?
 
Back
Top Bottom