Bima ya Afya kwa wote inakuja na sheria kali

Wizara ya Afya Tanzania NHIFTZ najua mna nia ya dhati kabisa ila kuna vipengele hasa 9 na 10 vitaenda kuuwa Mifuko mingine ya Afya, chonde huu muswada ushirikishe wadau. Tunaenda kutengeneza tatizo kubwa sana bila kujua.

Huenda Actuarial valuation Report ya NHIF imetoa recommendations ili kunusuru Mfuko kupitia UHI Act, ila lazima wadau wote katika sekta ya Afya pamoja na mifumo ya Bima nchini washirikishwe.
 
Upumbavu tuu kama wameshindwa kuongoza mfuko wa bima ukiwa na wanachama wachache itakuaje tukiingia wengi.

Wao wametengeneza assumption kwamba watanzania wengi hawaumwi ila wanasahau watanzania wengi wanakimbia gharama za uchunguzi. Watanzania wanawai kuchukua dawa na kutibu ugonjwa kwa kukisia.

Tutarudi mule mule tuu.
 
Wamebuni namna nyingine ya kukwapua hela. Kwanini bima hii iwe lazima kwa kila mwananchi!?.

Wameua mifuko ya hifadhi ya jamii, wameua bima ya afya NHIF, wameona wabuni njia mpya ya kukomba hela za walala hoi.

Hii nchi bwana.
 
Hili la Bima ya Afya ni jambo jema. Laiti bila kishinikizo cha sheria na au Serikali- kulazimisha mwananchi kuingia kwenye pata potea, kwenye upatu inayoenda kuendeshwa na makampuni binafsi.

Kifungu cha 32 (a)(h) cha Muswada huo, itakuwa ni lazima kwa wananchi kuwa na bima ya afya kila wanapotafuta leseni ya udereva, bima ya magari na kudahili watoto kwa elimu ya juu ya sekondari au vyuo.
Kwa nini kwenye leseni ya udereva?
Mambo mengine nayo bora tuuzwe kwa ujumla....ndio maana yake.

Haiwezekani kulazimishwa upatu kwa kunyimwa kitambulisho. Kwa maoni Hii ni social research ya ajabu sana.
 
...sio hata kitu cha Kujadiliwa.

Mnatuuza Wananchi.!
 
TOZO ZIMEHAMIA KWENYE BIMA KWA NAMNA NYINGINE.

Hongera Mwigulu. Genge la msoga litatumaliza.
 
je ambao ofisi zetu zimetukatia bima katk mashirika binafsi itakuaje hapo??mwenye kufahamu tafadhali maana isije ikaleta balaa mtu umekatiwa bima nzuri then unalazimishwa kutumia NHIF ambayo baadhi ya hsptl nzuri hawaitaki kabisaaaaaa!
 
Mhhh
 
BAADA ya kutoonyesha msimamo Wake KWENYE vita ya urusi na Ukraine,ndipo Marekani itasitisha huduma za fedha kwa mfuko wa WHO NA NCHI ZETU ZITAATHIRIKA KWA KUKOSA DAWA AMBAZO TULILIPIWA BURE NA FEDHA HIZO KAMA CHANJO NA ARVS !Ndio maana serikali ikaamua kuiua NHIF na kuja na Kodi ya afya iitwayo BIMA ambayo ni lazima KWA kila Mtz kulipa Ili kufidia GHARAMA za afya ambazo tulikuwa tunapata Bure!!!


Ni nyakati chungu Sana za afya zinazokuja KWA NCHI yangu Tanzania!!

Tujiandae Tozo na kodi ya kichwa KWA kisingizio cha BIMA!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani Sasa iwe Katiba Mpya"
 
Hivi wasio na kipato au wasiojiweza kama maskini wazee na walemavu inakuwaje hapo tuna watz wengi mno wanaishi chini ya poverty line kupata mlo na mahitaji muhimu ni ishu wengine hata serikari inasaidia kupitia TASAF nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…