Bima ya Afya kwa wote wataalamu msizunguke mbuyu utekelezaji uanze mara moja!!

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Salamu!

Mimi ni muumini na mdau kindakindaki wa huduma endelevu za afya chini ya uwekezaji wa Watanzania wenyewe. Nimesimama na hoja hii kwa muda mrefu na nitasimama nayo hadi kieleweke.

Tanzania kama nchi lazima tukamilishe uhuru kamili kwa kuhakikisha masuala ya msingi, hususani huduma za watu wetu, zinapatikana kutokana na mapato yetu na si utegemezi wenye masharti na wa msimu kutoka kwa walami, wakoloni wa zamani na wakoloni mamboleo.

Kwa miaka kadhaa takribani 20+, huduma za afya zimekuwa zikitegemea hisani ya Wamarekani na walami wengine. Kwa miaka mingi, tumeshuhudia huduma za afya zikiwa ni chaka la kupitishia misaada halali na haramu kwa kisingizio cha misaada ya kijamii.

Chaka hili pia limetumika kama mwiba kwa serikali hasa nyakati za uchaguzi na nyakati za kufanya maamuzi ya kitaifa.

Taasisi mbalimbali, ikiwemo za dini na mashirika yasiyo ya kiserikali, yamejizolea umaarufu na kuiweka serikali kikaangoni kwa kuwa wanapokea misaada hii. Kwa muktadha huu, serikali haina budi kukatisha utegemezi huu unaoendelezwa kwa maslahi ya wazawa wachache na walami pia.

Uwepo wa njia mbadala na endelevu katika huduma za afya ni mojawapo ya mkakati muhimu katika kulifanya Taifa letu kuwa na uhuru kamili.

Isitoshe, kila mmoja wetu ataungana nami na kauli zilizowahi kutolewa hapo awali juu ya vita dhidi ya maadui watatu—ujinga, maradhi, na umasikini. Kamwe maadui hawa hawataondolewa kwa msaada wa wakoloni wa zamani na wakoloni mamboleo wanaokuja kwa njia mpya kila siku.

Nimewahi kuulizia, kushawishi, kushinikiza, kukosoa na kupendekeza juu ya namna bora ya kuondokana na hili dubwana la muda mrefu...na inawezekana kabisa.

Nimekumbusha mara nyingi na sitaacha kufanya hivyo juu ya kufanya maamuzi magumu ya kimkakati, kisera, na kiutekelezaji katika kuhakikisha huduma za afya zinakuwa endelevu, nafuu, na mafaa kwa Watanzania wa hali ya chini.

Mtafaruku ninaouona ni uelewa, utayari na uwajibikaji wa wataalamu wa afya katika kuchakata na kuhitimisha suala hili.

Nimshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuelewa dhima ya bima ya afya kwa wote na hatimaye kuruhusu mjadala na baadaye kupitishwa kwa muswada wa bima ya afya kwa wote. Hii ni legacy ya kipekee ambayo tunapaswa kumbuka nayo.

Kinachonihuzunisha ni baadhi ya wataalamu kukwamisha mchakato huu ambao tayari umepata ridhaa ya kisiasa.

Inanishangaza kwa nini wataalamu wanaotakiwa kutekeleza wanafungua mijadala isiyo na tija wakati walipaswa kuelekea kwenye utekelezaji?

Hapa naanza kujiuliza ni nani mnufaika wa mfumo wa sasa anayewabana? Najiuliza zaidi...je, ni nani anayehujumu hatua hii muhimu ya kimaendeleo? Je, wanufaika wa misaada ndio wanatukwamisha kwa maslahi yao binafsi?

WITO KWA WAZIRI WA AFYA

Pokea maoni kwa wadau waliopo ngazi ya utekelezaji na kamwe usidanganywe na baadhi ya wataalamu ambao hawajawahi kuishi katika huduma za afya kwenye ngazi ya kata na mitaa. Kamilisha suala hili na kamwe usitishwe na wanajifichia kwenye maswala ya uchaguzi.

Bima ya afya kwa wote imepitia michakato yote na imepitishwa na wawakilishi wa wananchi...anayezuia na anayetafuta maoni mapya ni nani?

Tumpe zawadi yake na legacy yake Rais Samia kwa kukamilisha mchakato huu wa kihistoria.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Sera hii ni lazima itekelezwe no matter what
 
Hii inqtakiwa kuqnza kidogo kidogo

Kumbuka CHF imekufa na NHIF ipo hoi
 
Hongera sana na hongera tena Mhe Rais Samia kwa kutuletea sheria ya bima ya afya kwa wote
 
Back
Top Bottom