Bima ya Afya Tanzania: Kampuni bora na zenye changamoto katika kuhudumia wateja wake

Bima ya Afya Tanzania: Kampuni bora na zenye changamoto katika kuhudumia wateja wake

NHIF ijikite kutoa huduma na sio kufanya biashara hii. Kinachoendelea sasa ni kuweka rehani afya za waTz , mtu analipa 980,000 bado unamwambia baadhi ya huduma hawezi kupata is disturbing
 
NHIF ni janga kwakeli, haiwezekan Dr apsngiwe dawa na vipimo na jinsi ya kumtibu mgonjwa, sasa huko shuleni alienda kusomea nini?
 
Nilijua tuu wewe umetumwa na NHIF sio bure...yaan ukatwe 120,000 kwenye mshahara bado ulipie tena 50k kwa ajili ya mtoto huo ni wendawazimu
Na hiyo ya 50400 Ina a lot of restrictions...kuna huduma mteja hapatiwi.
 
Najua utakua ni mfanyakazi tu wa NHIF Sasa nina kero nyingi kuwahusu kwanza wafanyakaz wenu hawajui hta kuongea na wateja Kuna mmoja nilitaka nimzabe makofi kwa mdomo wake mchafu wakat mi nateketeza hela zangu huku nakosa huduma za muhimu
 
Hamna lolote. Dawa kibao zimeondolewa mfano mgonjwa wa kisukari ambaye dawa zingine zimeshindwa kumsaidia analazimishwa kutumia insulin wakati Kuna dawa Kama Galvas met ambayo mmeindoa kwa madai ni gharama.

Glucose test pia mmeindoa inabidi mtu anunue mwenyewe. Dawa nyingi mmeziondoa. Usitudanganye hatudanganyiki
 
NHIF kwa sasa ni dhuruma tupu. Nachangia 120,000 monthly toka mshahara. Kwenye nafasi tano za Dependants nilijaza mbili tu za watoto wangu . wamenitimia meseji ati December wanamuondoa mtoto wangu mmoja kwa vile atakua 18 years. That is daylight robbery. Something has to be done
Mtu mzima anaanzia 18 yrs, wako sahihi
 
Hamna lolote. Dawa kibao zimeondolewa mfano mgonjwa wa kisukari ambaye dawa zingine zimeshindwa kumsaidia analazimishwa kutumia insulin wakati Kuna dawa Kama Galvas met ambayo mmeindoa kwa madai ni gharama. Glucose test pia mmeindoa inabidi mtu anunue mwenyewe. Dawa nyingi mmeziondoa. Usitudanganye hatudanganyiki

Nilichokudanganya nini? Mimi nimesemea kwa upande wangu nimelipia 192,000 ila kuanzia February hadi sasa matibabu niliyotumia ni zaidi ya hiyo hela, tena imenisaidia sana.

Kilikua kipindi cha corona kila mtu hana ela, saa zingine naumwa sina hata mia naenda zangu hosp na bima yangu tu na hadi sasa naendelea kuitumia.

Kwa upande wangu BINAFSI imenisaidia kwenye matibabu yangu haswaaaa!! Hivi ningekuja kuomba msaada humu mngenipa zaidi ya kunichamba tu.
 
Najua utakua ni mfanyakaz tu wa NHIF Sasa nina kero nyingi kuwahusu kwanza wafanyakaz wenu hawajui hta kuongea na wateja Kuna mmoja nilitaka nimzabe makofi kwa mdomo wake mchafu wakat mi nateketeza hela zangu huku nakosa huduma za muhimu

Haya endelea kujua hivyo

Pole kwa yaliyokukuta
 
Umesafisha meno katika hospitali gani? Nahitaji na mimi nikapate huduma kwa kutumia kadi yangu
 
Nilichokudanganya nini? Mimi nimesemea kwa upande wangu nimelipia 192,000 ila kuanzia February hadi sasa matibabu niliyotumia ni zaidi ya hiyo hela, tena imenisaidia sana...
Hongera Mtumishi wa NHIF
 
Haya endelea kujua hivyo

Pole kwa yaliyokukuta
Hiyo list ya Dawa na maelekezo yake ni kweli kabisa na YASIPUUZWE kama walivyoandika hapo kukanusha. Barua hiyo ni usanii mtupu. Dawa namba 62 (DUPHASTON) dozi ni shilingi 84,000/= NHIF wanawalipa Pharmacy Tsh. 42,000/= Je pharmacy waingie hasara? Pharmacy zote hapa nilipo hazipokei Bima ya NHIF wamebakia na mabango ya NHIF lakini huduma hawatoi baadhi ya Pharmacy wamejitoa kabisa. Hayo yote nimeyajua baada ya kwenda Private Hospital na kuandikiwa dawa hiyo kisha kwenda Pharmacy niliambiwa dawa hiyo nitapewa kama nitaandikiwa na Hospital ya Rufaa ya Mkoa nikaenda huku.

Hospital ya Rufaa ndio ikawa balaa niliambiwa Duka la dawa la MSD hawana hiyo dawa, kipimo nilichotakiwa nipimwe kwenye Hospital ya Rufaa niliambiwa kipo ila NHIF hailipi hiyo niwe na Cash nitapimwa kwa Bima Hapana. Hiyo ilishauriwa niende Private Hospital kupata hicho kipimo kwa Bima.

Swali Je kama Hospital ya Rufaa hawapokei Bima vipi kuhusu Private Hospital? Waliniandikia dawa namba 62 nikanunue kwenye Pharmacy, nami nikarudi kwenye Pharmacy ile ile. Wakaniambia Dawa hiyo haipo, wakati naondoka kuna MTU aliniita pembeni akaniambia Dawa ipo ila BIMA inalipa nusu hivyo wao wanaingia hasara.

Juzi tu mwanangu aliandikiwa mseto was watoto kwenye Pharmacy na Hospital Sh. 3,000/= lakini Bima wakija wanawalipa Sh. 1,500/=. Pamoja na kusifia kote huko SISI WATUMIAJE tunaujua UKWELI. NHIF wanauwa watu indirect, dhambi itabaki kuwa dhambi tu. BIMA inayoshindwa kulipa Elfu tatu (3,000) au shilingi 84,000/= mhh ipo siku BOMU litalipuka. TIME WILL TELL. You can fool all people sometime, but you can't fool all people All the time.

EhF0HkbWoAQMZRl.jpg
View attachment 1614785
 
NHIF wanafanya Wizi..

Mwezi February nimelipia kile kifurushi cha kikubwa TIMIZA AFYA kabisa kwa mwaka mzima.

Kuna baadhi ya huduma maabara kama sijui X-Ray , ECHO , EEG wanatoa ila huduma kama MRI na CT scan ni hadi mwaka wa pili wa uchangiaji.. Nikaona pouwa tuu.

Kuna baadhi ya mambo ambayo bima hawaweki wazi kwa wateja wao

Mfano: Baada ya kupata bima, kuna siku nilienda hospitali moja (Dsm) kufika pale hospitalini wakadai kwa bima yangu hawezi kunihudumia..hadi niwe na Rufaa kutoka hospitali ngazi za chini ( nafikirini ni Zahanati)..

Swali; Ni kwanini nipate huduma kwanza kwenye hospitali za vichochoroni, then ndio niwe refered hospitali kubwa kama Muhimbili, selian, kairuki, TMJ and etc.

Kwanini hayo maelezo yasiwepo toka mwanzoni wakati nafanya application ya Bima?

Nafikiria huu ni aina ya wizi nao, kama shirika la bima tena linategemewa na watu wa kipato cha kawaida lazima lijiangalie upya..

Na bima yao nilitupa huko, nikiumwa tena nitajikongoja tuu nikatibiwe mahali pengine kuliko masharti yao ya kijinga..


View attachment 1614855
20201028_163211.jpg
 
Hivi karibuni kuna iwezekano nitapata kazi nyingine as a consultant ikimaanisha kwamba sitatambulika kama muajiriwa na nitahitaji kuprocess bima ya afya yangu mwenyewe binafsi. Nahisi NHIF ina unafuu wa bei, ila sijafanikiwa kupata gharama za vifurushi za BIMA nyingine kama Strategis, AAR, etc. ninachouliza nii:

1. Huduma zinazopatikana na hizi bima za makampuni binsafsi ni bora zaidi kuliko NHIF.

2. Je, gharama zake ni kubwa zaidi? au kiasi tu?

3. Kama ni gharama zaidi. Je, is it value for money?

Asante
 
Back
Top Bottom