Mimi ni mwanachama na nimekuwa nikifaidika na Bima ya Afya Tangu mwaka 2002 na nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa mafao ya hawa jamaa. Kitaalamu NHIF au Bima ya afya wanatumia system inayoitwa FEE FOR SERVICE ambayo hakuna kikomo cha gharama kwenye matibabu na unaweza kupata huduma wewe na wategemezi wako watano kwa maana ya wewe,mwenzi wako wa ndoa,watoto wako na wazazi wakoau hata wakwe zake na kuwa na jumla ya wanufaika sita na wote mnapewa vitambulisho ambavyo unaweza kupata huduma popote Tanzania kwenye hospitali zote za serikali,mashirika ya dini,za watu binafsi na na pia wamesajiri pharmacy ili ukienda na kukosa dawa kwenye hospital unapewa form ya kwenda kuchukua dawa. Na gharama ya kujiunga kwa mtu binafsi ni Tshs 964,800 na unapaswa tu kuandika barua kwao na kuwa na wadhamini wawili ambao ni wanachama wa NHIF. Hao wanaokushauri kwenda Private Insurance ni kwamba wao wana tumia capitation Method ambayo ina ceiling limit ya cost za matibabu na wana pima Health status ya wanachama wake na especially kama una mtu mwenye clonic desease wanamkataa hasa kansa,kisukari,figo wakati bima ya afya wao wanasema Organisation yao haiku katika misingi ya kibiashara wala lengo la kutengeneza faida bali kutoa huduma. kwa Dar ofisi zao ziko Makao Makuu ni Kurasini Bendera tatu jirani na makao makuu ya Bandari,Temeke jirani na Hospitali ya Temeke,Kinondoni wako Mwenge njia ya cocacola JOSAM House na Ilala wako Ocean Road hospital au watafute kwenye
www.nhif.or.tz au wa email
info@nhif.or.tz