Bima ya Afya

Bima ya Afya

Mkuu hapo Mwanza bila shaka wana ofisi za kanda ngoja waje wataokutajia zilipo ofisi ukifanikiwa kuwaona utapata kuhudumiwa.
 
Nenda kwa ofisi zao utapata maelezo yakutosha, ill inawezekana ukajiunga...
 
ni insurance gani nzuri ya private?
mwenye kujua anijuze
 
wazo zuri ngoja na mimi niangalie mchakato wa kufungua hii bima.
Nalog off
 
ni insurance gani nzuri ya private?
mwenye kujua anijuze

Bima zote ni nzuri lakini zinatofautiana kwa sifa na manufaa kwa mkata bima. Bima za Private kwa ufahamu wangu, ili kujiunga unatakuwa kwanza upimwe afya yako, wajue umri wako ndipo wakupangie "premium" ambayo itategemea afya yako na umri wako. Malipo yao nasikia ni makubwa kidogo ambayo mimi mmachinga au mkulima si rahisi kuyamudu. Bima za Taasisi za Umma kama vile NHIF, CHF,(ambazo mimi nazifahamu inawezekana zipo nyingine) ni wazi kwa kila Mtanzania.

Maelezo mazuri yanapatikana kwenye Ofisi zao za Mikoa kwani nasikia karibu kila Mkoa una ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (ambao nasikia wanasimamia pia Mfuko wa Afya ya Jamii CHF). Mimi nina kadi ya Bima ya Afya kupitia mwanangu ambaye ni mfanyakazi wa Taasisi ya Uma na ni Mwanachama wa NHIF. Kwa kweli bima hiyo ni nzuri sana kwetu walalahoi, kwani uinatibiwa popote utakapokuwa ili mradi pawe na hospitali iliyosajiliwa na NHIF.

Nakushauri uulizie Ofisi ya Mwanza ilipo ili wakuelimishe namna ya kujiunga ndugu yangu. Nakutakia kila la heri.
 
Aiseee utoaji wa dawa ni kituo cha afya sio bima ila miwani tu ndio tatizo hawagharimii kila aina ya miwani
 
Jamani naombwa kujuzwa kuhusu bima ya afya inayotolewa na NSSF,je inahitaji vigezo gani ili kujiunga?
 
ndugu wana jf.uko wapi umuhimu wa kuwa na bima ya afya?
Nauliza hili nikiwa nimekwazika na huduma tunayopewa na hospitali nyingi hapa nchini.ukiwa na bima ya afya nijuavyo mimi unatakiwa upate vipimo, upewe dawa pale hospitalini.
Lakini hospitali nyingi unaweza ukapimwa na ukaambiwa nenda dukani kanunue dawa sisi hapa hospitali hatuna.

Na hizi ndizo hospitali nilizoambiwa majibu hayo. Hospitali ya mkoa RUVUMA. Hospitali ya PERAMIHO. Hospitali ya mwananyamala. Hospitali ya IFAKARA KATOLIKI. Hospitali ya wilaya ULANGA.

Kisha naomba munijuze je ninaumuhimu wakuendeelea kukatunza haka kakadi ka bima ya afya wakati hakanisaidii?
 
Yale maduka binafsi yanakapenda sana hako ka kadi kako ka bima ya afya, Nenda nako!
 
Matibabu kwa bima ya afya ni adhabu, kwanini bima ya afya hawataki kuitisha mikutano na wadau ili tuwape kero zetu, kwavyovyote vile kuna jambo wananufaika wao binafsi na si kama mfuko
 
System ya bima ya afya ni nzuri kama kweli inakua implemented inavyostahili,kuna wadau kadhaa wanahusika,service providers(vituo vya afya,mahospitali),policy ambayo inasimamia mfumo mzima na watumia huduma,hawa wote wana nafasi ktk kuendelea kwa mfumo huu.

Shida inakuja kua serikali yenyewe haitoi kipaumbele kwenye sekta ya afya,ruzuku hazitoki ipasavyo vituo vya afya havijaboreshwa,mfumo hasi wa kuamini matumizi ya taslimu nk,tunaona hata bajeti ya wizara ya afya inadidimia kila mwaka wa fedha,huwezi kusonga mbele.
 
Matibabu kwa bima ya afya ni adhabu, kwanini bima ya afya hawataki kuitisha mikutano na wadau ili tuwape kero zetu, kwavyovyote vile kuna jambo wananufaika wao binafsi na si kama mfuko

Unapo kuwa kwenye foreni na kabima kako wakati wenzako wanakeshi unaambiwa subili kwanza wakati mwenye fedha keshi mkononi anapata huduma.huu sio mfumo bora
 
Naamini ni mpango mzuri sana, kwa nchi yenye mfumo mbovu lazima uface hizo challenges. Dawa utapata maduka binafsi ambayo yako registered. Pole pole mkuu
 
Kweli hili jambo limekua kero kuna hospitari zingine za serikali wakiona vipimo vyako vya gharama wanakwambia mashine imearibika labda uende hospitari fulani
 
Kweli hili jambo limekua kero kuna hospitari zingine za serikali wakiona vipimo vyako vya gharama wanakwambia mashine imearibika labda uende hospitari fulani

Hilo nalo lipo nilienda hospitali kuangalia afya yangu.daktari aliniuliza unaumwa nini?nikamwambia siumwi chochote ila nataka nipime choo ndogo na choo kubwa na damu.akaniambia kama hujihisi homa yoyote ludi tu nyumbani tunaupungufu wa vifaa tiba.hakika hii ndio tanzania yetu
 
ndugu wana jf.uko wapi umuhimu wa kuwa na bima ya afya?
Nauliza hili nikiwa nimekwazika na huduma tunayopewa na hospitali nyingi hapa nchini.ukiwa na bima ya afya nijuavyo mimi unatakiwa upate vipimo,upewe dawa pale hospitalini.
Lakini hospitali nyingi unaweza ukapimwa na ukaambiwa nenda dukani kanunue dawa sisi hapa hospitali hatuna.
Na hizi ndizo hospitali nilizoambiwa majibu hayo.
Hospitali ya mkoa RUVUMA. Hospitali ya PERAMIHO. Hospitali ya mwananyamala. Hospitali ya IFAKARA KATOLIKI. Hospitali ya wilaya ULANGA.
Kisha naomba munijuze je ninaumuhimu wakuendeelea kukatunza haka kakadi ka bima ya afya wakati hakanisaidii?


Ukiambiwa kununua pia unatakiwa ukanunue kwenye duka ambalo linapokea huduma ya bima siyo kulipa cash.
 
Matibabu kwa bima ya afya ni adhabu, kwanini bima ya afya hawataki kuitisha mikutano na wadau ili tuwape kero zetu, kwavyovyote vile kuna jambo wananufaika wao binafsi na si kama mfuko

it is true mi mwenyewe siku hizi nimeamua kujilipia cash japo nina hiyo bima ya afya...ukweli ni kero kubwa sana kutumia hii huduma, mi nilishaamua kujilipiaga tu, japo naumia mara mbili
 
Back
Top Bottom