Bimmer na Landcruiser V8

Gari yenye 320hp na uzito wa 1800kg haiwezi lingana na gari ya 380hp ina uzito wa 3000kg. Hp/kg ndo uchawi ulipo.

Ndo maana acceleration zinatofautiana.

Hapo ukiwaambia wanakwamba hiyo 340i haifui dafu kwa vxr.
 
Aisee hizo Landcruiser zinaharibika pia.. Ishu ni gari za serikalini.. Kuna taasisi kadhaa zimeshindwa kuzimaintain gari.. Zimepaki nyingi tuu.. Fanya kutafuta Landcruiser za serikali zilizokuja brand new 2014 mpaka leo ngapi bado zipo barabarani..
Dereva wa serikali hajali hata akiitupa mtaroni anajua kesho Nduvini atalipwa na kodi zetu gari inarudi road.

Ndo maana huku mtu anakwambia VXR inafukia matuta hata ikiwa 180kph. Nenda kapige yako uletewe mkeka wake ndo utajua kwanini hujui.

Hizo gari ni delicate tu kama hizi za wajerumani, simply zinamilikiwa na serikali na wanavyoziendesha hovyo mnadhani ikiwa yako utaibamiza kama ilivyo.

Zile mkonga ndo unaweza zipiga utakavyo ila sio haya mayai.
 
Sure.. Wafanyakazi wa Uma wanaharibu sana funds za wananchi..!
Landcruiser iliyokuja 2014 brand new leo hii haitazamiki..!

Yes kabisa.. Landcruiser zipo Off road oriented na Comfort Oriented..
LC200 sio off-road..front axle haina na ni kitu muhimu kwa off roader.. Sema sababu vitu vya serikali nani atauliza..
Ukikutana na LC200 private barabarani utaona tofauti ya uendeshaji.. Labda iwe ya mwarabu au mhindi..!
 
Hata wakandarasi nawaelewa kutumia hizo Lc 200.

Hata akiwa Mpanda au Nkasi, anajua kitu kikizingua atatumwa mtu mwanza au mbeya akalete spare, inafungwa kitu kinaamka tena.

Sasa wewe na benzi yako ipasue kitu, mpaka ije cfao kazi imeshalala.

Convenience ya garage na spare availability ndo toyota alipowapiga bao hao wajerumani huku tanzania. Ila ule udelicate wa gari upo palepale.
 
Sure aisee.. Pia ni fursa hiyo kuleta spares za Wazungu .. Ufundi pia ni fursa nyingine.. Kutengeneza gari nje ya Mjapani..!
 
Duu hiyo range rover ya kushindwa na hz itakuwa ni ile yenye engine ya tdi labda lakini sio ile v8 ya zamani iliyotumiwa sana na wahindi kama racing car,70 series niliyowahi iona ktk racing ni 1GR V6 pekee!
 
Hahaha aisee usisahau Range Rover zilikuwa hairuhusiwi kupaki benki (stori za kale).. Walikuwa na hii engine 4.2EFI.. Landcruiser haiwezi.. Na wakati huo mafuta tsh 400..haikuwa ishu kuipush..
Plus P38 zimekuja Era hiyo hiyo ya 90's..Landcruiser hajawahi kuwa mkali wa spidi.. Ni vile enzi hizo gari nyingi za Toyota engine 3L.. Kwahiyo 1HZ ilionekana ndio kila kitu..
 
Diesel haiwezi kuwa moto hata siku moja.

Engine ya diesel imetengenezwa kuwa na torque kubwa na siyo horsepower kubwa.
Mzee kuna haya mabalaa!

1. Audi SQ7 4.0 TDI V8 Tiptronic quattro, diesel engine. Hii ina engine power ya 430 bhp na engine torque ya 664 lbs/ft. 0-62mph in 4.9 seconds

2. BMW X5 3.0 M50d Auto xDrive. Engine power ni 376 bhp, engine torque ni 545 lbs/ft. Na 0-62mph in 5.3 seconds

3. Porsche Cayenne 4.2 TD S Tiptronic S 4WD. Engine power ni 380 bhp, engine torque ni 627 lbs/ft. 0-62mph in 5.4 seconds

Sasa hapo hakuna moto?

Sema tu TRA kanyoosha goti kwenye mabalaa!
 
Tsh. 400 kipindi hicho unaona ilikua ndogo?.miaka 20 kutoka Sasa madogo wakija kusikia petrol enzi Lita 1 ilikua kwny buku 2 watashangaa kichizi nakuona baba zao walikua wazembe kuto ku-push ndinga zenye 6.2l huko,maana hio pesa itakua Ni ndogo sana.
 
Haya ni mawazo ya kimaskini sana
 
Mkeka wa ist mpya😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…