Mkuu hili wala sidhani kama litakuwa na mjadala mrefu.
Ukiona gari imeandikwa 180 na imefungwa saizi ya tairi sahihi basi hiyo gari haiwezi kuvuka 180.
Ukiona gari imeandikwa 180 na inavuka 180 basi kuna mawili. Moja gari imefungwa tairi za saizi kubwa kuliko zinazotakiwa, mbili gari imekuwa tuned ikaondolewa speed limiter.
Speaking from experience, last week tulikuwa tunapeleka gari Toyota Premio Tanga mjini. Kama kumbukumbu zangu zipo sawa ile gari tairi zilizofungwa ni 175/70R14 na ukisoma kile kibati cha pale mlangoni tairi zinazotakiwa ni 185/70R14.
Ile gari tukisoma speed kwenye google map ilikuwa inatuletea speed ndogo kuliko speed inayoonesha kwenye dashboad. Around 55Km/h kulikuwa na difference ya 4Km/h.
Speaking of Passo na Bus aiseee hizi ni story za vijiweni. Speed ni universal.
Basi na passo zote zikianza at point A na zikaaccelerate kwa 100Km/h wote watafika point B at the same time.
Asikudanganye mtu eti 100 ya Basi ni kubwa kuliko 100 ya Passo.
Huo ni uongo wa mchana kweupe.