Bimmer na Landcruiser V8

Bimmer na Landcruiser V8

V8 achana nalo akikaa dreva sahihi huwezi muacha kizembe. Utabisha tu ila ndo uhalisia.

Mwenyewe nina mjerumani ila ukileta mambo ya kushindana na huyo mjapan kwenye hizi barabara zetu na dreva akiwa vizuri hutoboi.

Kwanza ile gari kwenye bamsi anafukia tu wakati lets say una x5 new generation huwezi fukia bamsi kubwa utaogopa sensa zisidondoke.
Hilo moto wake sio mchezo! Halijali bumps wala rasta linakatiza tu. Shock ups zake zipo Poa sana
 
😄 kwa hiyo kile kibati pale kimeandikwa 180 ndicho mwamuzi siyo? Fanya tena uchunguzi anza na basi lenye 160 vs Passo 180.

Mkuu hili wala sidhani kama litakuwa na mjadala mrefu.

Ukiona gari imeandikwa 180 na imefungwa saizi ya tairi sahihi basi hiyo gari haiwezi kuvuka 180.

Ukiona gari imeandikwa 180 na inavuka 180 basi kuna mawili. Moja gari imefungwa tairi za saizi kubwa kuliko zinazotakiwa, mbili gari imekuwa tuned ikaondolewa speed limiter.

Speaking from experience, last week tulikuwa tunapeleka gari Toyota Premio Tanga mjini. Kama kumbukumbu zangu zipo sawa ile gari tairi zilizofungwa ni 175/70R14 na ukisoma kile kibati cha pale mlangoni tairi zinazotakiwa ni 185/70R14.

Ile gari tukisoma speed kwenye google map ilikuwa inatuletea speed ndogo kuliko speed inayoonesha kwenye dashboad. Around 55Km/h kulikuwa na difference ya 4Km/h.

Speaking of Passo na Bus aiseee hizi ni story za vijiweni. Speed ni universal.

Basi na passo zote zikianza at point A na zikaaccelerate kwa 100Km/h wote watafika point B at the same time.

Asikudanganye mtu eti 100 ya Basi ni kubwa kuliko 100 ya Passo.

Huo ni uongo wa mchana kweupe.
 
V8 achana nalo akikaa dreva sahihi huwezi muacha kizembe. Utabisha tu ila ndo uhalisia.

Mwenyewe nina mjerumani ila ukileta mambo ya kushindana na huyo mjapan kwenye hizi barabara zetu na dreva akiwa vizuri hutoboi.

Kwanza ile gari kwenye bamsi anafukia tu wakati lets say una x5 new generation huwezi fukia bamsi kubwa utaogopa sensa zisidondoke.
Hahahha ndio maana namwambia huyo chalii hio GX V8 ni kama Tank! Yani inafukia rasta na ma bumps kama utani vile 😅

Wakati wewe unarudi 30KPH kuruka bumps mwenzio analipanda na 100KPH gari inanepa tu na kutembea 😅
 
Labda Bumps kubwa na zipe Humps...

Ila Rasta hata Mjerumani anapita kwa speed kubwa.

Af Bumps kubwa hata huyo Mjep lazima arudi 30 otherwise lazima apae....
Sawa utapita kwa speed kubwa kwenye rasta lakini baada ya week utaenda clinic kuuguza majeraha 🤣🤣 maana huko chini kutaanza kugonga balaa
 
Aisee mambo ya bumps tena..!!Rough road..!!Huko hata 1HZ inaweza kukupita..
Hapo ni highway.. Stretch ndefu tuu hakuna bumps na ni lami tupu..
Unaweza ukawa na mjerumani ila ukashindwa kumtumia.. Tupunguze kutengeneza mazingira ya visingizio..
Hapo sijatoa facts gari yangu ni ya zamani.. Model ya 1992.. Imeingia Tanzania wakati wa namba TZ*.. Ina registration ya namba AB za mwanzoni.. Lakini hata leo hii hizo V8.. Kama sio VX.. VXR.. Lazima nikuvute shati..!

Na hizi challange zimeanza siku hizi gari imepungua moto.. Kipindi hicho cha late 90s gari bado mbichi ilikuwa haishikiki..!
 
Gari mpaka iue wishbone we utakuwa uneigeuza Off road af unapita juu ya mawe kwa
Gari mpaka iue wishbone we utakuwa uneigeuza Off road af unapita juu ya mawe kwa speed kali.
shida ya hizi highway zetu unakutana na mashimo ya kushtukiza inabidi ufukie tu maana ukikwepa unaweza kupata ajali. Ukiwa na kilimo kwanza unapiga shimo bila hofu ila sasa uje kwenye haya magari ya kizungu utajuta. Unaweza kuacha sample barabarani
 
Mkuu hili wala sidhani kama litakuwa na mjadala mrefu.

Ukiona gari imeandikwa 180 na imefungwa saizi ya tairi sahihi basi hiyo gari haiwezi kuvuka 180.

Ukiona gari imeandikwa 180 na inavuka 180 basi kuna mawili. Moja gari imefungwa tairi za saizi kubwa kuliko zinazotakiwa, mbili gari imekuwa tuned ikaondolewa speed limiter.

Speaking from experience, last week tulikuwa tunapeleka gari Toyota Premio Tanga mjini. Kama kumbukumbu zangu zipo sawa ile gari tairi zilizofungwa ni 175/70R14 na ukisoma kile kibati cha pale mlangoni tairi zinazotakiwa ni 185/70R14.

Ile gari tukisoma speed kwenye google map ilikuwa inatuletea speed ndogo kuliko speed inayoonesha kwenye dashboad. Around 55Km/h kulikuwa na difference ya 4Km/h.

Speaking of Passo na Bus aiseee hizi ni story za vijiweni. Speed ni universal.

Basi na passo zote zikianza at point A na zikaaccelerate kwa 100Km/h wote watafika point B at the same time.

Asikudanganye mtu eti 100 ya Basi ni kubwa kuliko 100 ya Passo.

Huo ni uongo wa mchana kweupe.

Hapana hapo kwenye maelezo yako umeaply ceteris paribus theory.

Halafu, Nakuquote:
"Asikudanganye mtu eti 100 ya Basi ni kubwa kuliko 100 ya Passo".

Hakuna mtu aliye na elimu asiyejua hili ila hapa tunazungumzia vyombo viwili kushindana katika hizo km/hr zilizopo na sio utofauti wa km/hour 🤣.

Ukirudi kwenye uhalisia katika km hizo za kushindania Kuna engine performance, kuna tyre size, kuna road condition na mambo mengi.

KWA UFUPI, KATIKA KUSHINDANA SPEED METR NI SEHEMU NDOGO TU INAYOAMUA NANI ATASHINDA, MAMBO NI MENGI MNO YANAYOAMUA NANI AWE MSHINDI. Otherwise kama kila kitu ni sawa kusingekaa kukapatikana mshindi. Ingekuwa ni sare sare maua.
 
Nna experience ya BMW X3. Nilikua nalibembeleza kwenye rasta maana najua gharama zake kwenye kubadili bush na wishbone. Ila ukikuta lami nzuri na haina bumps za hapa na pale utatembea mpaka uchoke
Hahahahahahahah ukiwaza ile 800K ya bushing na wishbone unakuwa mpole🤣 unatembea mwendo wa kobe kwenye matuta!
 
Hahahha ndio maana namwambia huyo chalii hio GX V8 ni kama Tank! Yani inafukia rasta na ma bumps kama utani vile 😅

Wakati wewe unarudi 30KPH kuruka bumps mwenzio analipanda na 100KPH gari inanepa tu na kutembea 😅
Kabisa. Halafu hapo hajakutana na kibao cha men at work kisha kipande cha barabara kimefungwa unatakiwa uchepuke kwenye barabara yenye mawe kama m300 hivi 😂.

Hapo Bima inaenda mwendo wa guta wakati mwenzake atawatimulia vumbi hao men at work.
 
Back
Top Bottom