May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Miaka kadhaa nyuma nilihudhuria msiba wa aliyekuwa jirani yangu kabla, kwa bahati mbaya au nzuri walihamia nje ya mji.
Kwa wakati huo kulikuwa bado ni shambani hivyo hata miundo mbinu ya barabara haikuwa rafiki ,Bajaji na Bodaboda hazikuwepo bado, ilikuwa mwanzoni wa 2000.
Usiku saa mbili nikawasha Peugeot 505 (sijui kama wa kizazi kipya mnazijua hizi) ilikuwa tiamajitiamaji lakini nikajitia ujasiri kuwa nitafika msibani na kurudi...kweli msibani nilifika, ila sasa kurudi ngoma ikagoma kuwaka, piga piga na wewe saa tano kwenda sita usiku...nikapaniki kwani naingia kazini saa sita usiku.
Tukaisukuma Ndiga jirani na geti, nikaifunga vizuri nikaanza kuvizia lifti, Magari yalikuwa mengi kwani Mzee (baba wa marehemu)alikuwa Kigogo pale mjini. Nikawakuta kina Mama wawili watu wazima wanaongea, mmoja alikuwa Sister wa Katoliki..walikuwa kama wanaagana hivi, nikawasogelea nikawasalimia na kuuliza kama kuna anayeelekea mjini anisaidie lifti...hawakunijibu zaidi ya kuniangalia kama vile walinitaka niwaache wana maongezi.
Basi pale pale nikakumbuka Mwenzangu mmoja ofisini kwenye mastori aliwahi kuniambia "unaweza kupata tatizo mahali akapita Mtumishi wa Mungu akakuacha lakini ukaja kusaidiwa na Jambazi aliyetoka mahali kufanya tukio"...Nikawaza, pale naweza kwenda kwenye kona nikawakuta Masela 'wanalipuliza' na chupa zao za vimiminika pembeni, nikawaelezea tatizo wakaniambia "usiwaze Msela tunachomoka dakika sifuri...si unajua tena tunapooza hapa..Msela wetu G katangulia".
Ingawa baadae nikaja kupata lifti ya mmoja wa Wanafamilia alikuwa anaenda mjini, lakini nilibaki na jambo nimejifunza.
Kuna wakati unaweza kustaajabu pale ambapo yule Mtu unayemuamini na kumkubali, ukafika mahali ukaambiwa "huyu jamaa si Mtu mzuri" au kinyume chake kwa yule unayeamini ni katili na asiyejali basi ukaambiwa "huyu Jamaa ana roho nzuri sana".
Ninachoamini mimi kwa kuwa Binaadamu hatufahamiani, huwezi kumtambua aliyetoka kuuwa sasa hivi au aliyetoka kumsaidia chakula Bibi kikongwe wa nyumba jirani aliyetelekezwa na Wanafamilia wake...kwa wakati huo pale wote mpo sawa, mpaka pale utakaposikia au kuambiwa au kuona mwenyewe.
Swali ni je, Binaadamu ni kiumbe anayelazimika kupitia haya mabadiliko kutokana na mazingira anayokuwepo?, kwamba kila Binaadamu anabeba vinasaba vyote...vya wema na ubaya...na kinachosubiriwa ni kianzisho tu?.
Hivyo hali zote kwake si za kudumu bali hutegemea tu na alipo kwa wakati huo...Hivyo kamwe usimuwekee Binaadamu mwenzako mdhamana kwa hali unayomkuta nayo wakati huo.