mkuu,nilivyomuelewa Yericko,ni kwamba binadamu ndiye mungu kwa sababu unapompa title ya muumbaji maana yake nini?hii ni imani ya New Age,kwamba Mungu mkuu anayetawala vyote hayupo zaidi ya binadamu mwenyewe kuwa mungu na umoja wa binadamu wote huleta nguvu kuu sana.Ndio wameijaza dunia na haya mafundisho ya "discovering yourself".Actually ni kweli kuna sehemu ya powers za binadamu hasa spiritual part ambazo kizazi cha leo tumekuwa mbumbumbu sana kuzijua,sasa New age wanakuja na elimu kuhusu nguvu hizi(na mengineyo ni chumvi tu) huku wakipotosha kwa kusema nguvu hizi zinadhihirisha uwezo wa kiungu ulio ndani ya binadamu na huku wakiutukuza uwezo huu kuwa independent ilhali ukweli ni kwamba uwezo huu una mahusiano na Muumba wanayekataa existence yake.Hawa New age wana imani ya meditation wanayodai inawaunganisha na viumbe fulani toka kwenye invisible realm(4th dimension nadhani) ambao wanawaita masters.Wanadai kila mtu ana master anayemwezesha kujitambua na kumsaidia hadi kufikia "uungu" wake,hivyo imani yao inatakiwa kusambazwa ili watu wajenge mahusiano na masters wao kwa ajili ya kukuzwa kiuwezo hadi wafikie uwezo wa "kiungu" ulio ndani yao ambao utawafanya watende lolote watakalo.Ukitazama hapo utaona contradictions nyingi tu za kinadharia ambazo kwa mtu aliyetuliza kichwa ataziona.Hao masters ni nani, wanatoka wapi na nani kawaumba?wanasema binadamu mungu ni lini aliumba dunia na how comes leo hii anashindwa kutumia huo uwezo wake hadi asaidiwe na masters?hizi ndizo zile roho za uchafu zilizofanana na vyura kwenye revelation nadhani!beware!majini yanatafuta namna ya kufit kwenye dunia yetu,waje kuishi nasi kama wenzetu ili watumie intelligence yao kubwa kututawala na kutukusanya kwa vita ile iliyo kuu against the most high,the holy God,the creator,the merciful pale Harmagedon!Haya ni majeshi ya Dajjal!ndio maana nasema lazima tuwe wakali na mafundisho haya.Si ya kukalia kimya.Ndugu zetu wengi wanayabeba haya mazima mazima bila kujua kilicho nyuma ya pazia na kwa vile yanagusia baadhi ya uwezo wa kibinadamu ambao kweli anao,na vile watu walivyo na hamu ya kujitambua,watu wengi sana wanatekwa.So,so,so many!