Binadamu kuishi milele - Kama zoezi la kuunganisha ubongo na mfumo wa komputa litakamilika

Binadamu kuishi milele - Kama zoezi la kuunganisha ubongo na mfumo wa komputa litakamilika

Nimekupata ndugu,lakini kumbuka mwanadamu anamwisho wake Kwa kila afanyacho,pia ili iwepo tofauti kati yake na Mungu,ni lazima kuwe na vitu vinavyowatofautisha.
...hiyo biblia unafikiri kila MTU anaiamini ?
 
Kina baadhi ya vitu ambavyo mwanadamu hatoweza kuvivumbua,mfano,siri ya kifo.Vitu hivyo ni siri ya Mungu pekee
Biblia inasema"kila mwanadamu ni lazima age,na baada ya kifo ni hukumu"

Mmeshaanza kila kitu ni biblia,Kwani biblia ni nini?

Embu jaribu kufungua mawazo yako na kutafakari vitu pasipo na hiyo biblia tazama dunia kwa upande mwingine usikariri kila kitu ni biblia
 
Jambo hili haliwezekani.

Wafanye mengine tu.

Anyway, wakifanikiwa mtanitag wakuu
Linawezekana in theory lakin practical bado hajawa implemented. Anacho jaribu kukisema elon musk ni kutransfer human conciousness kwenda kwenye computer.

Kuhusu suala la kuzeeka hapo ndio itakuwa ngumu zaidi. Maana ni dna na protein maalum ndio huzeesha mwili. Labda acheleweshe aging process.
Lakin pina kuna possibility kukawa na artificial body ambayo inaweza kuwa ni robot na ikawekewa ubongo wa binadam.

Angalia movie moja inaitwa "ghost in the shell"
Utaelewa hii concept
 
Waafrica Wata oa wataacha watakuwa na watoto kijiji kizima. Si akuna kufa akuna kuzeeka
 
sifa moja kuu ambayo ubongo inayo ni kuwa ubongo unasifa ya kufikiri.. kwa kutumia kumbukumbu,maarifa,mazingira na ujazo wa ufahamu wake binadamu hufikiri na kutoa majibu,swali ni je,sifa hiyo itarithishwa..?
 
Kina baadhi ya vitu ambavyo mwanadamu hatoweza kuvivumbua,mfano,siri ya kifo.Vitu hivyo ni siri ya Mungu pekee
Biblia inasema"kila mwanadamu ni lazima age,na baada ya kifo ni hukumu"

Never say never mkuu. Maandiko matakatifu yapo imara kwenye masuala fulani fulani tu ila kisayansi huwa yanachemka sana.

Mfano hai ni pale kitabu fulani kilivyochemka kuhusu umbile la dunia enzi hizo.
 
Hizi projects nyingine mbona zina utata???
 
Ubongo wa binadam ni zaidi ya molecular chemical reactions.Kuna Swali la Roho.Huyo aliyeunganishwa na computer anaeishi si yule original aliyekufa.
 
Never say never mkuu. Maandiko matakatifu yapo imara kwenye masuala fulani fulani tu ila kisayansi huwa yanachemka sana.

Mfano hai ni pale kitabu fulani kilivyochemka kuhusu umbile la dunia enzi hizo.
Havikuchemsha mkuu.kutoka hapo ulipo unaweza kwenda kushoto,kulia,kasakazini au kusini.pengine pote ni sehemu ya hizo Major au Cardinal headings hizo nne.
 
Tena uzinduzi wa matundu ya vyoo siku ukifanyika unachukua nafasi ya kwanza kwenye taarifa za habari za vituo vya redio na televisheni kwa siku hiyo, na hufanywa na viongozi wa kitaifa
Yani mkuu Haya mambo wenzetu walifanyaga karne ya 18 uko lakini sisi ndo tunakomaa nayo karne hii ya 21..
 
Back
Top Bottom