Katika jambo mojawapo la upotoshi mkuu ambao dini umeweza kufanya ni kuwaaminisha binadamu kwamba wa ndio kitovu cha ulimwengu (the center of the universe), kwamba kila kitu kimeumbwa kuwazunguka wao.
Kwamba wanyama, miti, Samaki, ndege na viumbe wengine wote vimewekwa kwa ajili yao, huu ni uongo mkubwa sana. Hapo ndipo mtu anamshukuru mungu wake kwa uhai wake kisha anaenda kuchinja kuku au ng'ombe na jumla! Anashukuru kwa uhai wake kisha anaenda kutoa uhai wa viumbe vingine!
Binadamu sio kitovu cha ulimwengu (center of the universe). Imetokea tu binadamu kuwepo kwenye sayari mojawapo ndogo kama vile viumbe wengine wote katika ulimwengu wenye mabilioni ya Galaxy na matrilioni ya Sayari.