Napenda nikubaliane na points ambazo Alola ameweka kwenye mchango wake. Lakni nadhani kujarbu kujua ni kwa nini wewe upo hapa duniani ni swali ambalo hakuna mwanadamu anayeweza kulijibu. Ni sawa na kujibu kwa nini Mungu ameumba nyota nyingi kiasi hicho? (Uki-google 'galaxies' utapata maelezo kwamba 'a gallaxy is a collection of stars. It is estimated that there are 50 billion galaxies and each galaxy has about 50 billion stars). Ukijiuliza ni kwa nini Mungu ameumba nyota nyingi namna hiyo utapata jibu? Never! Au ukijiuliza kwa nini kila mtu ana alama ya kidole gumba au DNA tofauti na ya binadamu mwingine yeyote unadhani utapata jibu? Hupati !
LAKINI: Hilo halina maana kwamba Mungu hakumpa kila mtu jukumu lake. KILA MTU ana jukumu ambalo Mungu kampa. Tatizo kubwa ni kwamba wengi wetu sisi hatujui wala hatutafuti kujua mpango wa Mungu kwenye maisha yetu. Kwa wale wanaosoma Biblia, ukienda kwenye kitabu cha Wakolosai utaona namna Mtume Paulo alisema anawaombea Wakolosai ILI WAPATE MAARIFA YA KUJUA MAPENZI YA MUNGU KWAO ni yapi. Lakini bila hata kwenda kwenye kitabu chochote cha dini, sote tunajua kwamba kuna mtu ambaye Mungu anamweka awe mkuu wa nchi (hata kama watu wengine hawataki), na huyo huyo lazima apate mpishi wa kumpikia na dobi wa kumfulia n.k. Mungu anataka mwingine awe daktari, mwingine ajenge barabara, mwingine afundishe watoto wetu, mwingine alime tupate chakula n.k. Kila mtu ana kusudi ambalo Mungu amempa.
Kwa hivyo, wewe usiulize ni kwa nini upo hapa duniani. Kuna jukumu ambalo Mungu amekuwekea la kufanya. TENA UJUE: UKIWEZA KUJUA KUSUDI AMBALO MUNGU AMEKUWEKEA, UKILIFANYA UTAFANIKIWA MAISHANI.