Binadamu tunaishi ili iweje? Au tupo duniani kufanya nini? Why Do We Live?

Binadamu tunaishi ili iweje? Au tupo duniani kufanya nini? Why Do We Live?

Tafuta kusudi lako ndo utajua unaishi kufanya nn humu dunian
 
Kuna sababu za msingi zilizomleta kila mmoja wetu hapa duniani. Tatizo ni kujua kilichokuleta. Na kama utaishi bila kujua
kilichokuleta, wengine watakutumia ili wakamilishe mipango iliyowaleta.

Mfano :

Kijana anapenda kuwa mhandisi wa mawasiliano lakini kwa sababu amepata alama fulani chuo kinamwambia huko
unakotaka kumejaa labda usome kemia na kijana hana uwezo wa kifedha. Huyu kijana anenda kusoma kemia na anamaliza stashahada au shahada, anaanza kufanya kazi kama mkemia. Lakini kumbe laiti kama angesomea mambo ya mawasiliano angeweza kufanya maajabu katika taaluma hiyo na dunia ikatambua uwepo wake. Vivo hivyo unakuta kijana kapata daraja la kwanza na pointi tatu katika kidato cha sita. Anataka kusoma uhandisi fulani na anakipaji cha hali ya juu katika hilo ila tu kwa sababu wanaofaulu sana huwa wanaenda kusoma kozi fulani na ye anafuata mkumbo na kuishia kutafuta mkate wake wa kila siku na utaalamu huo.

Wapo watu wamekuja hapa duniani kama mitihani kwa wengine, wapo waliokuja kutuachia teknolojia fulani, wapo waliokuja kutuonyesha mambo ambayo tulidhani hayawezekani kwenye michezo, siasa, biashara, sayansi, n.k.
Na vipi mtu mwenye matatizo ya akili kama mtindio wa ubongo anajuaje lengo lake hapa duniani ikiwa hawezi hata kujua jina lake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I have not found one argument against existential nihilism.

Life must have a meaning, for there to be a purpose.

Kila mmoja wetu ana maana yake ya maisha na hivyo kila mmoja wetu ana "purpose" yake ya kuishi.

Tatizo ni pale kunapokuwa na mila, desturi na imani. Kwamba katika maisha lazima uamini mungu, uende shule, uwe na kazi, uoe/uolewe, uwe na watoto etc. Hivyo vitu kama hivyo vinabebwa na jamii na kufanywa "purpose" ya maisha kwa wote.

Lakini si kweli kwa sababu si kila mtu ana maana moja ya maisha. Mwingine anaweza kusema maisha haya ni a one time shot that's never coming back. Kwa mfano mtu anaweza kuamua kusema hakuna purpose yoyote ya kuishi na kuamua kujiua, mwingine anaweza sema maisha yangu nitasafiri dunia nzima, mwingine nitasoma as much as I can na kuamua kuishi bookstores, etc etc..

So bottom line, life has no objective meaning, it's what you make it.

Hakuna sehemu inayosema binadamu tupo hapa ku-achieve something. So you decide what you want out of this life.
Hii deep sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo swali lako lipo ki-imani zaid..kma wwe ni mkristo refer kwnye bible ama muulze pastor wako but kma ni muslim jbu ni simple tu coz uki-refer kwnye Qur-an Mungu anasema ,"nimeumba majini na b/damu ili tu wapate kuniabudu"..kwa mana hyo atakaefuata hayo maamrisho bhas atapata makaz mema akishakufa but kinyume na hayo utachomwa moto wa jehanamu
Ukijitahidi kufikiria nje ya vitabu ,Kuna jibu halisi lipo kichwan kwako mwenyewe Bila vitabu,na kama hupati jibu nje ya vitabu(yaani Kwa kufikiria) basi upo kwenye kifungo ambacho huwezi toka, na hayo ndo maisha yako halisi yaliyokuleta hapa duniani
 
Mimi huwa nashangaa washika dini wanavyoogopa kifo wakati ndio wanasisitiza huko mbinguni ni kuzuri kuliko duniani.
Mtu kwenye ajali utasikia Yesu niokoe, Allah niepushe, sasa ya nini yote hio wakati mnaenda kuwa karibu na muumba sehemu yenye maziwa na asali na mabikra kadhaa?

Ingetakiwa muwe mna encourage kufa kama kweli mnaamini mbinguni kupo na ni kuzuri kuliko hapa.

Kwetu pazuri, nimepakumbuka... la mkifa vilioo!!
😆😆😆😆😆 nimecheka sana
 
Tunaishi ili kuchunguza uumbaji. Na hili ndilo lengo halisi la uwepo wetu hapa duniani na ndiyo ibada ya kweli, maana unapochunguza uumbaji Ni lazima utasifu tu eidha kimoyomoyo au kwa sauti. Hivyo basi utaendelea kusifu Hadi ukomo wa umri wako na ukifa watazaliwa wengine kwa fikra mpya za kusifu uumbaji.
 
Dunia Ni Banda binadamu nimifugo na mfugaji hajulikani Ni Nani ila yupo

Yupo kwasababu Banda haliji jengi linajengwa

So tunafugwa tunaliwa na tuna chaguliwa yupi wa kuliwa leo yupi aachwe Kama tunavyo chagua kuku bandani

Duniani hatupo peke yetu Kuna viumbe vinatu chunga vinatulinda na kututafuna japo hatuvioni na kibaya zaidi tuna amini katika vyenyewe kuwa ndivyo walinzi wetu

Kama vile kuku aaminivyo kwamba sehemu sarama ya kuishi Ni nyumbani kwa mfugaji wake

lakini huku asijue huyo huyo mfugaji wake ndiye adui namba moja wa vizazi na vizazi vyake

Mwisho nikukumbushe kwamba dunia Haina 7 continents Kuna dunia nyingine nyuma ya zile ice walls na Kuna viumbe wanaishi

Sasa hatujui viumbe hao chakula vyao pendwa Ni vipi
 



Bila-shaka hakuna swali lisilo na jibu japokuwa kila jibu litolewalo si lazima liwe sahihi. Waulize swali moja wanafunzi wa chekeachea, shule ya msingi, sekondari na vyuo kwa nini unasoma shule?

Majibu mengi yaliyotolewa yalikuwa majibu ya kunakili kutoka kwa wazazi au walezi wa hao watoto. Wangi wao walisema wanasoma hili maisha yao ya baadaye yawe mazuri. Nilipowauliza nini maana ya maisha mazuri?

Nilipokuwa nasoma chekechea ak.a kindergarten mwalimu alinifundisha kuwa moja toa mbili jibu lake ni haiwezekani. Nilipoingia darasa la kwanza mwalimu huyo huyo wa chekechea akanifundisha kuwa moja toa mbili jibu lake ni (-) hasi moja. Swali moja majibu mawili tofauti lakini yote ni sahihi.

Baada ya maelezo hayo machache nikukaribisheni mtoe maoni yenu katika kujibu swali hilo hapo juu.
.
 
Back
Top Bottom