Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Naomba nitoe dukuduku langu na naamini katiba ya nchi hii inanipa uhuru huu kwa maana sivunji sheria yoyote.
Miaka ya hivi karibuni, serikali imeingilia sana uhuru wetu. Kuna wakati watu walikuwa wananyakuliwa kwa sababu tu wametoa maoni yao mitandaoni na wengi wao wakaenda kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi. Ni wazi kuwa serikali haiheshimu si tu uhuru wetu wa kutoa mawazo bali pia sheria za usiri tulizonazo. Uchaguzi Mkuu uliopita ulikumbwa na kiwango kikubwa sana cha uvunjifu wa haki za binadamu na sheria za uchaguzi, hilo lilipita na leo tuna viongozi bungeni na serikalini ambao hawana baraka za wananchi.
Hivi sasa kuna kampeni ya zoezi la kuhesabiwa linalokuja. Baadhi ya mambo uyakayoulizwa ni matumizi yako ya simu janga na laptop kama unavyo. Sijali hili zoezi linaenda kufanywa kwa malengo gani ila abuse ya power ambayo imeonyeshwa tena na tena haivumiliki.
Wametusumbua sana kupata vitambulisho vya NIDA wengine mpaka leo hawajapata, mitandao ya simu inapandisha gharama kila siku na kutuibia bando zetu, serikali haijali na hata kuyatetea haya makampuni. Zikaja tozo za miamala, yaani wizi kila sehemu na hakuna wa kututetea.
Huu ni mgomo wangu binafsi. Simshawishi mtu yoyote ajiunge nami katika hili ila binafsi sipo tayari kutoa taarifa zangu zozote zile.