Binafsi nakataa kuhesabiwa, kuna sheria yoyote ninavunja?

Cha kufanya hiyo wiki ya sensa hama kwako kabisa ili wasikuhesabu, mpaka wakishafunga mahesabu yao utarudi, sidhani kama kuna sheria inayokubana
Kuna namna mbili za kuendesha sensa: 'de facto', na 'de jure'. Kwa mtindo wa 'de facto' swali linaloulizwa ni kwamba watu wangapi walilala hapa nyumbani siku ya sensa? Kama ulilala nyumba ndogo, huhesabiwi nyumbani kwako bali huko kwenye nyumba ndogo. Kwa mtindo wa 'de jure' swali ni kwamba wangapi wanaoishi hapa nyumbani? Hivyo hata wewe uliyelala nyumba ndogo utahesabiwa nyumbani kwako na si kwenye nyumba ndogo. Kumbuka kwamba udadisi unafanywa nchi nzima wakati huo huo. Hivyo usijidanganye kuondoka nyumbani ili usihesabiwe. Utahesabiwa tu uwepo au usiwepo.

Siku ya sensa kunafanyika utaratibu hata stesheni au airport watu wanahesabiwa. Kwa hiyo takwimu zitapatikana watu wangapi walikuwa safarini siku ya sensa; wangapi kwenye nyumba za kawaida za kuishi; wangapi walikuwa kwenye nyumba za jumuia: kwa mfano jela, hospitali au hosteli ya wanafunzi; n.k.
 
Sidhani kama nahitaji kuhama au kuwakwepa kama sivunji sheria yoyote. Wakija nawaambia tu sitaki kutoa ushirikiano, waendelee tu na shughuli zao.
Kuna sheria ya Sensa katika kila nchi. Ukikataa kuhesabiwa ni miaka minne jela au faini au vyote kwa pamoja. Ujue sensa haina hiari ni lazima.
 
Kuna namna mbili za kuendesha sensa: 'de facto', na 'de jure'. Kwa mtindo wa 'de facto' swali linaloulizwa ni kwamba watu wangapi walilala hapa nyumbani siku ya sensa? Kama ulilala nyumba ndogo, huhesabiwi nyumbani kwako bali huko kwenye nyumba ndogo. Kwa mtindo wa 'de jure' swali ni kwamba wangapi wanaoishi hapa nyumbani? Hivyo hata wewe uliyelala nyumba ndogo utahesabiwa nyumbani kwako na si kwenye nyumba ndogo. Kumbuka kwamba udadisi unafanywa nchi nzima wakati huo huo. Hivyo usijidanganye kuondoka nyumbani ili usihesabiwe. Utahesabiwa tu uwepo au usiwepo.

Siku ya sensa kunafanyika utaratibu hata stesheni au airport watu wanahesabiwa. Kwa hiyo takwimu zitapatikana watu wangapi walikuwa safarini siku ya sensa; wangapi kwenye nyumba za kawaida za kuishi; wangapi walikuwa kwenye nyumba za jumuia: kwa mfano jela, hospitali au hosteli ya wanafunzi; n.k.
Shukrani mkuu tumepata elimu.

Nataka kuuliza, watatumia mtindo wa de facto ama de jure?
 
Naomba nitoe dukuduku langu na naamini katiba ya nchi hii inanipa uhuru huu kwa maana sivunji sheria yoyote.

Miaka ya hivi karibuni, serikali imeingilia sana uhuru wetu. Kuna wakati watu walikuwa wananyakuliwa kwa sababu tu wametoa maoni yao mitandaoni na wengi wao wakaenda kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi. Ni wazi kuwa serikali haiheshimu si tu uhuru wetu wa kutoa mawazo bali pia sheria za usiri tulizonazo. Uchaguzi Mkuu uliopita ulikumbwa na kiwango kikubwa sana cha uvunjifu wa haki za binadamu na sheria za uchaguzi, hilo lilipita na leo tuna viongozi bungeni na serikalini ambao hawana baraka za wananchi.

Hivi sasa kuna kampeni ya zoezi la kuhesabiwa linalokuja. Baadhi ya mambo uyakayoulizwa ni matumizi yako ya simu janga na laptop kama unavyo. Sijali hili zoezi linaenda kufanywa kwa malengo gani ila abuse ya power ambayo imeonyeshwa tena na tena haivumiliki.

Wametusumbua sana kupata vitambulisho vya NIDA wengine mpaka leo hawajapata, mitandao ya simu inapandisha gharama kila siku na kutuibia bando zetu, serikali haijali na hata kuyatetea haya makampuni. Zikaja tozo za miamala, yaani wizi kila sehemu na hakuna wa kututetea.

Huu ni mgomo wangu binafsi. Simshawishi mtu yoyote ajiunge nami katika hili ila binafsi sipo tayari kutoa taarifa zangu zozote zile.
Mkuu,

Kwa mjibu wa amri za rais ambazo hutekelezwa kwa mjibu wa sheria ukigoma wanao uwezo wa kukufunga kwa jaribio la kukataa huduma hivyo kuhatarisha maisha yako na wengine.

Zamani ilikuwepo sheria ya Takwimu ya mwaka 1961 ambayo iliitwa (The Statistics Ordinance Act, 1961, Cap 443 ambayo ilifutwa mwaka 2015 ikatengenzwa nyingine inayoendana na mahitaji ya Tanzania huru kupitia tangazo la serikali GN 491 ya 2015. Ilipotimu mwaka 2019 sheria ya Takwimu ya Taifa (The Nationa Bureau of Statistics Act, 2015) ikarejerewa mwaka 2019 na kuitwa The Statistics Act Cap 351 RE 2019.
Sheria hiyo inaanzihswa na amri ya rais katika kifungu 21 (1) & (2) ikakaziwa katika utekelezaji wake kwenye kifungu cha 24 (3) na 36 (1), (2) & (3) a-b
*ACHA WAKUHESABU TU KAMA WEWE NI MTANZANIA NA NI MWEMA MAANA HATA KABLA< WAKATI NA BAADA YA YESU SENSA ILIFANYIKAKUJUA IDADI YA WATU KWA KUPANGA MIPANGO WALIYOJIWEKEA KWA KULINGANA NA RASILIMALI ZILIZOPO.

Hitimisho: Sheria ipo inayokulazimisha ukikataa watakuzulia jambo ambalo hulijui kisha wanakubana
Reference: https://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/ACT/STATISTICS_ACT_CAP_351_(R.E 2019).pdf
 
Naomba nitoe dukuduku langu na naamini katiba ya nchi hii inanipa uhuru huu kwa maana sivunji sheria yoyote.

Miaka ya hivi karibuni, serikali imeingilia sana uhuru wetu. Kuna wakati watu walikuwa wananyakuliwa kwa sababu tu wametoa maoni yao mitandaoni na wengi wao wakaenda kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi. Ni wazi kuwa serikali haiheshimu si tu uhuru wetu wa kutoa mawazo bali pia sheria za usiri tulizonazo. Uchaguzi Mkuu uliopita ulikumbwa na kiwango kikubwa sana cha uvunjifu wa haki za binadamu na sheria za uchaguzi, hilo lilipita na leo tuna viongozi bungeni na serikalini ambao hawana baraka za wananchi.

Hivi sasa kuna kampeni ya zoezi la kuhesabiwa linalokuja. Baadhi ya mambo uyakayoulizwa ni matumizi yako ya simu janga na laptop kama unavyo. Sijali hili zoezi linaenda kufanywa kwa malengo gani ila abuse ya power ambayo imeonyeshwa tena na tena haivumiliki.

Wametusumbua sana kupata vitambulisho vya NIDA wengine mpaka leo hawajapata, mitandao ya simu inapandisha gharama kila siku na kutuibia bando zetu, serikali haijali na hata kuyatetea haya makampuni. Zikaja tozo za miamala, yaani wizi kila sehemu na hakuna wa kututetea.

Huu ni mgomo wangu binafsi. Simshawishi mtu yoyote ajiunge nami katika hili ila binafsi sipo tayari kutoa taarifa zangu zozote zile.
Zoezi la Sensa ni kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kwa Tanzania tunaongozwa na sheria ya takwimu Sura 351 inayoeleza kuwa kila mtu "anawajibika" kutoa taarifa sahihi katika zoezi hili na huyu atakayepewa /kusanya taarifa hizo "anawajibika" kutunza Siri za kila mtu.
Taarifa zote zitakusanywa kwa ajili ya matumizi ya kitakwimu na kimaendeleo na si vinginevyo

Hivyo kwa sheria hiyo ya takwimu, kila raia anawajibika kuhesabiwa/kutoa taarifa zake na endapo taarifa hizo itabainika zimetumika kinyume na malengo tarajiwa mwananchi anayo mamlaka ya kuishitaka NBS kwa kusababisha taarifa zake kuvuja.
 
Hili zoezi makinda angemuuliza Mukandala yule wa tume ya katiba maana Kisha onana na watz wote
 
Zoezi la Sensa ni kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kwa Tanzania tunaongozwa na sheria ya takwimu Sura 351 inayoeleza kuwa kila mtu "anawajibika" kutoa taarifa sahihi katika zoezi hili na huyu atakayepewa /kusanya taarifa hizo "anawajibika" kutunza Siri za kila mtu.
Taarifa zote zitakusanywa kwa ajili ya matumizi ya kitakwimu na kimaendeleo na si vinginevyo

Hivyo kwa sheria hiyo ya takwimu, kila raia anawajibika kuhesabiwa/kutoa taarifa zake na endapo taarifa hizo itabainika zimetumika kinyume na malengo tarajiwa mwananchi anayo mamlaka ya kuishitaka NBS kwa kusababisha taarifa zake kuvuja.
Eti unaweza kuishtaki NBS, hahaah, ni Tanzania hii hii? Nyie kama mmekubali kuwa wanyonge kwenye nchi yenu hilo nawaachia wenyewe, ila mimi msimamo wangu ni huo huo. Sidhani kama kutoshiriki mimi kutaathiri hizo takwimu kutokusanywa.

Hakuna ambaye yuko juu ya sheria, kama na wao huwa wanadharau sheria tena walizotunga wenyewe, kwa nini mimi nizifuate?
 
Kuna namna mbili za kuendesha sensa: 'de facto', na 'de jure'. Kwa mtindo wa 'de facto' swali linaloulizwa ni kwamba watu wangapi walilala hapa nyumbani siku ya sensa? Kama ulilala nyumba ndogo, huhesabiwi nyumbani kwako bali huko kwenye nyumba ndogo. Kwa mtindo wa 'de jure' swali ni kwamba wangapi wanaoishi hapa nyumbani? Hivyo hata wewe uliyelala nyumba ndogo utahesabiwa nyumbani kwako na si kwenye nyumba ndogo. Kumbuka kwamba udadisi unafanywa nchi nzima wakati huo huo. Hivyo usijidanganye kuondoka nyumbani ili usihesabiwe. Utahesabiwa tu uwepo au usiwepo.

Siku ya sensa kunafanyika utaratibu hata stesheni au airport watu wanahesabiwa. Kwa hiyo takwimu zitapatikana watu wangapi walikuwa safarini siku ya sensa; wangapi kwenye nyumba za kawaida za kuishi; wangapi walikuwa kwenye nyumba za jumuia: kwa mfano jela, hospitali au hosteli ya wanafunzi; n.k.
Asante kwa Elimu
 
Sheria ya takwimu ya mwaka 2015 iliyofanyiwa revision 2019 sura ya 351 kifungu cha 43 (1) kimeeleza adhabu kwa watu watakaokataa kutoa ushirikiano, kukataa kujibu maswali, kutoa taarifa za uongo na kushawishi watu kugomea sensa, jela miezi 6 au faini milioni 1 au both
 
Hivi na smart phone nazo zinahesabiwa kwa ajiri ya nini
 
Mimi mwenyewe sina mpango wa kuhesabiwa. Nihesabiwe ili iweje. Maisha yangu hayategemei sensa wala serikali sina cha kupoteza
 
Ungekuwa arusha tungeungana tukanywe bia hata mimi nachapa songa au nalala tuli weee nitoe taarifa zangu wananionaje ??
Nasepa 23 to 24 au nalaa au naishi chooni.
 
Back
Top Bottom