Binafsi nakataa kuhesabiwa, kuna sheria yoyote ninavunja?

Why trouble yourself? Kuna njia nyingi sana za kukataa kuhesabiwa bila hata kukwazana nao-Binafsi sioni point ya kuhesabiwa as long as nimeshaona process yenyewe tokea mwanzo imekaa kisiasa
 
Hata usiwaze, Utatolea taarifa zako polisi tena kwa hiyari kabisa, tena watakuwa hawana haraka. Watatumia Kama wiki hivi kukuhoji huku ukitumia malazi na chakula cha serikali.
 
Hapa kwangu Kuna mwembe mkubwa nimeishaweka kitanda huko juu, wiki nzima nitakuwa huko maana madodoso yapo "too personal" yaani namba za simu, mitandao ya kijamii, kama nina account bank, kitambulisho cha nida, mbuzi wangapi, nineoa na kuacha mara ngapi....maswali hayo yote DINI haiulizwiv! Hii nchi ambayo taarifa za raia wake zinazagaa tu Kila siku tunapigiwa simu na kutumia sms za "hiyo pesa tuma kwenye namba hii" sasa hao wakipata taarifa zetu muhimu so watatuuza kabisa!

Pumbavu zenu sihesabiwi ng'o!
 
Naunga mkono hili kwa 100.01%
Kuhesabiwa sio lazima, kila mtu yuko huru katika kuamua. Mimi nami sitaki kuhesabiwa.
 
Huyu atakuwa miongoni mwa waliokatwa UKARANI
Sio kwa hasira hizi
 
Sidhani kama nahitaji kuhama au kuwakwepa kama sivunji sheria yoyote. Wakija nawaambia tu sitaki kutoa ushirikiano, waendelee tu na shughuli zao.
Jichanganye! Zoezi la sensa lipo kwa mujibu wa sheria.
 
Umuhimu wa Sensa unajulikana na ni budi kuhesabiwa. Hivyo basi, kukwepa kuhesabiwa ni kosa la jinai.

Lakini, lakini, Sensa ya mwaka huu hakika imeweka maswali mengi ya ubinafsi wa mtu km "kama umewahi kutoa mimba" ambayo yanitia ukakasi kujibiwa au jibu litakuwa la uongo. Maswali mengine yanayohusu kipato na matumizi ya mtu yangefanyiwa tafiti tofauti (Household Budget Survey) km umiliki wa vitu kama simu na matumizi yake.

Naamini kila sekta ya maendeleo inahitaji kupata takwimu za kuandaa mikakati ya utekelezaji ila kurundika maswali yote kwenye zoezi la Sensa ni mtihani mgumu
 
Hiyo sheria inasema rais ni mtukufu?
 
Uhuru wako hautapingwa na yeyote
 
Sidhani kama nahitaji kuhama au kuwakwepa kama sivunji sheria yoyote. Wakija nawaambia tu sitaki kutoa ushirikiano, waendelee tu na shughuli zao.
hilo ni kosa la kukataa agizo au amri halali. kama hautakuwepo ni sawa
 
Mimi sitaki kuwasikia kabisa. Na nitaacha viumbe wangu wazurure nje wiki nzima. Sasa wajichanganye walete miguu yao wakutane na Rottweiler mwenye njaa!
 
Hivi ukichinjiliwa baharini itakuwaje?
 
Kabla ya kuanza sensa, Rais hutangaza kwamba siku fulani itafanyika sensa. Kila mtu aliyemo nchini hulazimika kutii amri. La sivyo utatozwa faini kiasi fulani; au kwenda jela kwa muda fulani; au vyote viwili kwa pamoja. Sensa hutungiwa sheria maalumu kupitia Bunge; na siyo kwa Tanzania tu bali nchi zote ulimwenguni. Sensa pekee ndiyo unalazimishwa kutii. Ukusanyaji mwingine wa habari unaofanywa na hata chombo cha serikali unaweza kukataa kushiriki bila madhara yo yote. Si kwa sensa.

Sensa huanza saa 6 usiku wa kuamkia siku husika na huendelea hadi kuhesabu kwa watu kutakapokamilika; huenda ikawa hata wiki mbili. Lakini swali linabakia hilo hilo hata kama watafika kwako wiki mbili baada ya siku ya sensa. Watakuuliza: hiyo siku ya sensa walilala watu wangapi hapa nyumbani? Baadaye kunafuatia kudadisi taarifa za kila mmoja wa watu uliosema walilala hapo nyumbani.

Ikiwa mtu atafariki siku tatu baada ya siku ya sensa na kwako wakaja wiki mbili baadaye, ni lazima umtaje na huyo marehemu kwa kuwa alikuwa akiishi siku ya sensa. Kinyume chake ni kwamba kama mtoto atazaliwa siku moja baada ya sensa na wakaja kwako wiki mbili baadaye, huyo mtoto hahesabiwi kwa kuwa hakuwa akiishi siku ya sensa.

Ukijumlisha hesabu zote hizo ndipo unapata nchi ina idadi gani ya watu. Na kutokana na maswali yanayofuatia, tutajua raia ni wangapi; wanawake ni wangapi; watu wangapi hawana ajira; n.k.

Kwa ufupi huwezi kukataa kutoa habari kwenye sensa. Papo hapo, wakusanyaji wa habari kwenye sensa hawaruhusiwi kutaarifu chombo kingine cha serikali habari wanazozipata kwenye sensa. Kwa mfano ulipaji kodi. Habari zote zinazokusanywa zinabakia kuwa takwimu tu na mtoa habari hadhuriki kutokana na taarifa anazozitoa.
 
Huu ni utawala mwingine hesabiwa kwa amendeleo ya jamii yako
 
Rejea Sheria ya Takwimu ya mwaka 2009
Takwimu ni muhimu kwa serikali na Washirika wake wa Maendeleo
Rais Kesha toa tamko yakhe
Kuhesabiwa ni lazima
#Jiandae_kuhesabiwa@sensa2022
Sawa kabisa. Hakuna hiari kwenye sensa.
 
Kuna swali la kutoa taarifa zako za NIDA ili tukubane vizuri...
 
Kuna upotoshaji mkubwa humu ndani. Zoezi la sensa hawachukui majina ya watu bali taarifa zako tu, sasa mnaposema ni lazima nitoe taarifa zangu watajuaje nisipofanya hivyo?

Na hili zoezi ni la siku moja tofauti na baadhi ya watu wanavyosema.
 
Australia hata kupiga kura ni lazima kwa mujibu wa sheria..

Usipohesabiwa unataka uje utumie huduma za nani? Uwe unajihudumia kwa kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…