denoo JG
JF-Expert Member
- Oct 27, 2023
- 2,701
- 9,759
Habari zenu wana jamvi!.
Siku za karibuni Rais wa JMT Mh. Samia S. Hassan amekuwa akifanya teuzi na tenguzi za mara kwa mara, tena this time sio tu amekuwa akitengua wale ambao hakuonekana kuwaamini toka mwanzo, lakini sasa anatengua mpaka wale wandani wake wa karibu.
Binafsi nimekaa nikajiuliza nini malengo ya hizi teuzi na tenguzi, hasa wakati huu tukielekea chaguzi za S/M 2024, na uchaguzi mkuu 2025, hapa chini ni mambo makubwa manne yaliyonijia kama majibu.
-Anatupumbaza/kutudanganya; Baada ya serikali yake kukumbwa na kashfa mbalimbali, kubwa ikiwa kutoa rasilimali zetu watanganyika hovyo kwa wageni.
Huyu mama sasa ni kama anajua wazi ameshaharibu, haaminiki tena. Anachofanya kwa sasa ni kutudanganya kwa kuwaondoa wasaidizi wake aliokuwa akiwaamini mwanzo, na kuwarudisha wa mtangulizi wake JPM ili kutafuta kujirudishia imani kwa wapiga kura.
Inawezekana anafanya hivi kwa ajili tu ya kujivusha salama 2025, baada ya hapo sitashangaa akiwarudisha kina Nape, Makamba, na Ummy kwenye baraza lake la mawaziri atakapoapishwa 2025 kama akigombea na kushinda Urais.
- Amechanganyikiwa; wakati mwingine nikimtazama namuona kama mtu aliyechanganyikiwa, sasa hajui yupi amuamini, kwasababu wale aliowaona threat kwake kuelekea 2025 hata akawaweka pembeni, Kabudi na Lukuvi, leo amewarudisha. Huyu sasa ni sawa na mtu aliyekata tamaa anasukuma siku zake ziishe ajiondokee kwa amani.
- Ameanza kuyaona makosa yake, sasa anajisahihisha; Hili zaidi linasababishwa na matukio mabovu aliyofanya kwenye utawala wake, ikiwemo kuuza rasilimali zetu watanganyika, ikiwezekana ni ushauri mbovu aliopokea toka kwa wasaidizi wake aliowaamini.
Kutokana na kosa hilo, inawezekana sasa ndio maana ameamua kuwarudisha watendaji wa mtangulizi wake JPM, aliyeonekana kuwa mstari wa mbele kuzilinda rasilimali za taifa letu, kwa spidi hii siku sio nyingi zijazo tusishangae kumuona Luhaga Mpina barazani, na wakina Bashe kuondoshwa.
- Amenogewa na cheo cha Urais, anafanya kila awezalo kuendelea kubaki madarakani; Hili zaidi linachagizwa na matumizi mabaya ya vyombo vya dola kuwaminya wapinzani hasa Chadema, tukio la karibuni polisi kuwakamata, kuwapiga, na kuwasweka ndani viongozi wa juu wa Chadema ni mfano tosha.
Huyu inawezekana kabisa ameshauona utamu wa cheo chake, sasa anafanya kila jambo kuenfelea kukifaidi, hata sasa imemlazimu kwenda kinyume na ile falsafa yake mwenyewe ya 4R.