Binafsi nimeguswa na funga ya wakristo kipindi hiki cha kwaresma,Funga yenu haina kelele Wala majisifu

Kwenda kufuturu mbona maaskofu wako wanaenda😅😅... Ramadan ni heshima hata nyie mnakuja ofisini mmevaa vizuri ...Jamaa anaumia hata wao hawafungi .
 
Uko sahihi ,kila mtu ana dini.
 
Ongezea na hii.... Hakuna kufatiliana kama umefunga kwani kufunga ni kati ya mtu na Mungu na siyo kuwindana nani anakula ili kuchapana viboko na kupeana majina ya ajabu ajabu.
Mbaya zaidi ni pale ambapo hadi vitoto vya darasa la kwanza na la pili vinalazimishwa kufunga! Sijui kwa dhambi gani vilizonazo masikini na sijui kama vinaelewa maana ya kufunga au wanavitia kwenye mkumbo tu na kuvitesa bure kwa sababu ya ujinga wa kutoelewa maandiko
 
Utaumia sana kama hautokuwa busy na mambo yako ,unaumia hayo tu ila omba omba unawapita pale acha unafiki ni mpumbavu.

Waislamu tutaendelea mpaka siku ya mwisho ,wewe mwenyewe mbinafsi unafuatulia ya wengine ...Fanya yako uislamu unakua kwa kasi sana utaendelea kukonda.

Sisi hatujui ya kwenu ila nyie mnajua yetu 😅
 
Funga ya kristo ni kufunga usiku na mchana siku 40.
Siyo unafunga mchana usiku unakula halafu ujiita mkristo!
Mkristo gani mroho mwenye Imani ndogo anayeshindwa kujifunza kwa kristo?!

Yesu alifunga siku 40 kwa kusudi la kipekee, lakini hakuagiza Wakristo kufunga kwa namna ileile. Badala yake, aliwahimiza kufunga kwa dhati, kwa moyo safi, na kwa uongozi wa Mungu. Ndiyo maana Wakristo hufunga kwa njia tofauti, kulingana na uelewa wao wa kiroho na mazingira yao.

Yesu alifunga kwa muda wa siku 40 mfululizo jangwani (Mathayo 4:1-2, Luka 4:1-2). Alifanya hivi kama maandalizi ya huduma yake ya kuhubiri na kuokoa wanadamu. Pia, ilikuwa njia ya kushinda majaribu ya Shetani na kujionyesha kuwa Mwokozi wa kweli aliyekuwa tayari kufuata mapenzi ya Mungu kikamilifu.

Hakuna sehemu maalum katika Biblia inayotoa agizo moja la kufunga kwa Wakristo wote kwa namna fulani au kwa muda fulani. Hata hivyo, Yesu alizungumzia kufunga kama tendo muhimu la kiroho:

• Mathayo 6:16-18 – Yesu alisema, “Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki…” Akimaanisha kuwa kufunga ni tendo la binafsi kati ya mtu na Mungu.


• Mathayo 9:14-15 – Yesu alisema wanafunzi wake hawatafunga wakati akiwa nao, lakini watakapofiwa naye, watafunga.


• Matendo 13:2-3, 14:23 – Kanisa la mwanzo lilifunga kabla ya kufanya maamuzi makubwa kama kuchagua viongozi.


Tofauti katika kufunga kwa Wakristo zinatokana na mambo kadhaa:


1. Uhuru wa Kiroho – Hakuna amri ya lazima ya kufunga kwa siku 40 kama Yesu, hivyo Wakristo wana uhuru wa kufunga kulingana na hali zao za kiroho na kimwili.


2. Mazingira na Uwezo – Yesu alikuwa jangwani peke yake, bila shughuli za kila siku, lakini Wakristo wengi wana majukumu ya kila siku yanayohitaji nishati.


3. Desturi za Madhehebu – Madhehebu tofauti yana mitazamo tofauti kuhusu kufunga. Mfano:


• Wakatoliki hufunga kipindi cha Kwaresima (Lent).


• Waprotestanti wengi hufunga kwa namna zao binafsi.


• Waorthodoksi wana vipindi vya kufunga mara kadhaa kwa mwaka.


4. Uongozi wa Roho Mtakatifu – Wakristo wanahimizwa kufunga kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, si kwa sheria ngumu.
 
Sioni kama ni mjadala kwa sababu mwenzio ndiye kaleta mada.


Kumbuka sisi waislamu kama mimi sijui hiyo funga yenu yaani sipatilizi ila nyie hata wenye biashara wanaweka tangazi '' Punguzo mwezi wa Ramadhan '' imekuwa kama identify na kwetu iko kwenye nguzo za Uislamu ni ibada kabisa.


Kwa vile unaona waigizaji sio wanaofunga real ,katika uislamu funga ni siri baina ya mja na mola wake ...Mtu anaweza kudanganya au kufanya uzinzi ,wizi huko machoni anajifanya kafunga.

Kufuturu pamoja ni jambi jema naona ndugu yako analia lia hapo hata viongozi wa kikristo wanakuja kujumuika ni utaratibu mzuri ..Pia, ni sehemu muhimu ya kuwakumbuka wenye uhitaji.
 
1. Yesu ni Mungu na Mwanadamu kwa Wakati Mmoja

Katika Ukristo, Yesu anafahamika kama Mungu aliyefanyika mwili (Yohana 1:1, 14). Hii inamaanisha kwamba Yesu alikuwa na asili mbili:

• Asili ya Uungu – Kama Mungu, Yesu ana uwezo wote, anajua yote, na yuko kila mahali.

• Asili ya Ubinadamu – Kama mwanadamu, Yesu alihisi njaa, uchovu, na majaribu kama binadamu wengine.

Katika Wafilipi 2:5-8, Biblia inaeleza kuwa Yesu alijinyenyekeza na akajifanya mdogo kwa kuvaa ubinadamu, ingawa alikuwa sawa na Mungu. Hii inamaanisha kwamba alipokuwa duniani, aliamua kwa hiari yake kutokuwa na baadhi ya haki zake za uungu ili aweze kuishi kama mwanadamu kamili.

2. Kwa Nini Yesu Aliruhusu Kujaribiwa?

Yesu hakujaribiwa kwa sababu alikuwa na udhaifu wa kiroho, bali kwa sababu alikuja kuwa mfano kwa wanadamu wote. Biblia inasema:

• Waebrania 4:15 – “Kwa maana hatuna Kuhani Mkuu asiyeweza kushiriki nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.”

Kwa hivyo, Yesu alijaribiwa ili aonyeshe jinsi wanadamu wanavyoweza kushinda majaribu kwa kutegemea Mungu na Neno Lake.

3. Kwa Nini Shetani Alimjaribu Yesu?

Shetani hakujaribu Yesu kwa sababu hakujua kuwa ni Mungu, bali alijaribu kumshawishi Yesu atumie nguvu zake za uungu kwa ajili yake mwenyewe badala ya kutii mapenzi ya Mungu Baba.

Majaribu aliyopitia Yesu yanafanana na yale wanadamu wanakutana nayo kila siku:

1. Kubadilisha mawe kuwa mkate (Mathayo 4:3) – Jaribu la tamaa ya mwili (njaa).

2. Kurukwa kutoka juu ya hekalu (Mathayo 4:5-6) – Jaribu la majivuno na kutaka kujionyesha.

3. Kupewa falme za dunia kwa kumsujudia Shetani (Mathayo 4:8-9) – Jaribu la tamaa ya mali na mamlaka.

Yesu alishinda kila jaribu kwa kutumia Neno la Mungu, akisema “Imeandikwa…” kila mara, akionyesha kuwa nguvu ya kweli ni katika kuitii Biblia.

4. Je, Shetani Aliwezaje Kumpandisha Yesu Juu ya Hekalu na Milima?

Katika Mathayo 4:5 na Mathayo 4:8, Biblia inasema kwamba Shetani “alimchukua” Yesu juu ya kinara cha hekalu na juu ya mlima mrefu. Hii inaweza kufasiriwa kwa njia mbili:

• Kwa kweli – Shetani alimsogeza Yesu kimwili kwa uwezo wa kipepo.

• Kwa maono – Yesu alionyeshwa haya katika maono, kama ndoto ya kiroho.

Haijalishi ilivyotokea, kilicho muhimu ni kwamba Yesu alikataa kumtii Shetani na kushikilia ukweli wa Mungu.

Yesu alijaribiwa sio kwa sababu hakuwa Mungu, bali kwa sababu alikuwa pia mwanadamu. Aliruhusu hilo ili aweze kuwa mfano mzuri kwa wanadamu na kutufundisha namna ya kushinda majaribu. Shetani alijaribu kutumia udhaifu wa kibinadamu wa Yesu (njaa, mamlaka, na utukufu), lakini Yesu alisimama kwa Neno la Mungu na hakushindwa.
 
Hivi sasa ni saa 11:25 alfajiri,naruhusiwa kudakua au nimechelewa?
Uko mkoa gani?
Kama upo Kagera, Kigoma, Rukwa na Mbeya unazo kama dakika kama 20 hivi za kula daku. Ama Kama upo mikoa ya mashariki na pwani ya bahari ya Hindi kuanzia Arusha , Kilimanjaro, Tanga, Pwani hadi Lindi na Mtwara muda wa daku imeisha.
 
Ukweli usemwe sisi wanaofunga ni chini ya 5%. Sio kwamba hatuna mbwembwe ukweli ni kuwa wengi wetu hatufungi.
 
Kulinganisha haina maana ya kulazimisha kufanana,

Lakini pia yote uliyosema hayana uhalisia kwa sababu ukristu na biblia vilikuwepo kabila ya uislamu uliokuja miaka 500 baadae. Kwa hiyo kama kwenye uislamu kuna Zaburi na Torati pamoja na mitume kama Mussa bhasi hapo utajua vilitokea wapi

Na kingine hakuna mkristu aliyewahi kuforce mitume wala desturi zenu kufanana na ukristu ila ni waislamu ambao huwa wanamtanabaisha Yesu kama nabii Issa na Bikira Mariamu kama Maryam mama wa nabii Issa mwenye sura nzima kwenye Quran..

Hakuna mkesha wa wakristu unaoongelea uislamu HATA SIKU MOJA ila ni ninyi waislamu ambao huwa mnaweka mihadhara ya kuchambua Biblia na ni juzi tu mliweka muhadhara wenye jina YESU...

Kwa hiyo HAKUNA MKRISTO katika SESSION zal ukristu zenye kutaja UISLAMU ila ni ninyi waislamu ambao huwa mnautaja ukristu na Yesu katika session zenu..

Kwa kawaida yangu huwa sijihusishi na mijadala ya dini kwa mlengo huu ila kwa upotoshaji walo imebidi nikuweke sawa kutokana na uhalisia.. WAKRISTU hawana obsession na uislamu ila vice versa is true
 
Maaskofu wenu, wachungaji na maparoko wakialikwa iftaaaaaari ikulu au kwa kiongozi yoyote wa mkoa au wilaya au kwa tajiri fulani wanakuwa wakwanza kuwahi nafasi kuwashinda hata hao waislamu waliofunga na mkitaka ushahidi wa picha naweka!.
Hiyo inaitwa socialization
 

Na ile kupiga kelele na vopaza sauti kila siku kuanzia saa 2 usiku hadi saa 4 usiku inahusianaje na kufunga? Yaani ukipita kwenye mitaa ya misikiti ni mwendo wa kelele. Sijui wanao kaa karibu na misikiti wanaishije.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…