Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wivu tu wala hamna kipya hapo.Sijui kwa nini nikimuona mtu anahangaisha akili juu ya hizi imani huwa namdharau.
Kwani ukisimama unapopaamini wewe na kuheshimu wengine hata kama unawaona hawapo sahihi utapungukiwa nini?
#HebuMkue.
Uko sahihi ,kila mtu ana dini.Ukisikia muislamu anasema ukristo sio dini huyo mtu kakosa elimu sahihi ya dini!
Iwe kuabudu masanamu ni dini , kuabudu misalaba ndio isiwe dini!
Kwa taarifa yako hata upagani ni dini!
Dini ni aina yoyote ya mfumo wa maisha ambao mtu kauchagua kuwa ndio mwongozo wa maisha yake.
Kwa hiyo yule anayeabudu mizimu basi hiyo ndiyo dini yake na anayeabudu jua, mwezi, nyota, moto, mawe nk hcho anacho kuabudu na utaratibu wa kuabudu hiyo dini yake !
Kwahiyo uislamu ni dini, ukristo ni dini, uyahudi ni dini, ubudha ni dini, uhindu ni dini, ubaniani ni dini nk.
Dini ziko nyingi sana ila DINI YA HAKI NA SAHIHI MBELE YA ALLAAH NI UISLAMU kama alivyosema mwenyewe Allaah katika Suurat Aali Imrani Aya ya 19 ya kwamba :,
"{ إِنَّ ٱلدِّينَ عِندَ ٱللَّهِ ٱلۡإِسۡلَٰمُۗ
Bila ya shaka Dini (ya haki na sahihi)mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. "
Na akasema pia katika sura hiyohiyo Aalu Imrani Aya ya 85 ya kwamba :.
"{ وَمَن يَبۡتَغِ غَيۡرَ ٱلۡإِسۡلَٰمِ دِينٗا فَلَن يُقۡبَلَ مِنۡهُ وَهُوَ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ }
Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kupata hasara"
Mbaya zaidi ni pale ambapo hadi vitoto vya darasa la kwanza na la pili vinalazimishwa kufunga! Sijui kwa dhambi gani vilizonazo masikini na sijui kama vinaelewa maana ya kufunga au wanavitia kwenye mkumbo tu na kuvitesa bure kwa sababu ya ujinga wa kutoelewa maandikoOngezea na hii.... Hakuna kufatiliana kama umefunga kwani kufunga ni kati ya mtu na Mungu na siyo kuwindana nani anakula ili kuchapana viboko na kupeana majina ya ajabu ajabu.
Utaumia sana kama hautokuwa busy na mambo yako ,unaumia hayo tu ila omba omba unawapita pale acha unafiki ni mpumbavu.Mbaya zaidi ni pale ambapo hadi vitoto vya darasa la kwanza na la pili vinalazimishwa kufunga! Sijui kwa dhambi gani vilizonazo masikini na sijui kama vinaelewa maana ya kufunga au wanavitia kwenye mkumbo tu na kuvitesa bure kwa sababu ya ujinga wa kutoelewa maandiko
Funga ya kristo ni kufunga usiku na mchana siku 40.
Siyo unafunga mchana usiku unakula halafu ujiita mkristo!
Mkristo gani mroho mwenye Imani ndogo anayeshindwa kujifunza kwa kristo?!
Sioni kama ni mjadala kwa sababu mwenzio ndiye kaleta mada.Yesu alifunga siku 40 kwa kusudi la kipekee, lakini hakuagiza Wakristo kufunga kwa namna ileile. Badala yake, aliwahimiza kufunga kwa dhati, kwa moyo safi, na kwa uongozi wa Mungu. Ndiyo maana Wakristo hufunga kwa njia tofauti, kulingana na uelewa wao wa kiroho na mazingira yao.
Yesu alifunga kwa muda wa siku 40 mfululizo jangwani (Mathayo 4:1-2, Luka 4:1-2). Alifanya hivi kama maandalizi ya huduma yake ya kuhubiri na kuokoa wanadamu. Pia, ilikuwa njia ya kushinda majaribu ya Shetani na kujionyesha kuwa Mwokozi wa kweli aliyekuwa tayari kufuata mapenzi ya Mungu kikamilifu.
Hakuna sehemu maalum katika Biblia inayotoa agizo moja la kufunga kwa Wakristo wote kwa namna fulani au kwa muda fulani. Hata hivyo, Yesu alizungumzia kufunga kama tendo muhimu la kiroho:
• Mathayo 6:16-18 – Yesu alisema, “Mnapofunga, msiwe na huzuni kama wanafiki…” Akimaanisha kuwa kufunga ni tendo la binafsi kati ya mtu na Mungu.
• Mathayo 9:14-15 – Yesu alisema wanafunzi wake hawatafunga wakati akiwa nao, lakini watakapofiwa naye, watafunga.
• Matendo 13:2-3, 14:23 – Kanisa la mwanzo lilifunga kabla ya kufanya maamuzi makubwa kama kuchagua viongozi.
Tofauti katika kufunga kwa Wakristo zinatokana na mambo kadhaa:
1. Uhuru wa Kiroho – Hakuna amri ya lazima ya kufunga kwa siku 40 kama Yesu, hivyo Wakristo wana uhuru wa kufunga kulingana na hali zao za kiroho na kimwili.
2. Mazingira na Uwezo – Yesu alikuwa jangwani peke yake, bila shughuli za kila siku, lakini Wakristo wengi wana majukumu ya kila siku yanayohitaji nishati.
3. Desturi za Madhehebu – Madhehebu tofauti yana mitazamo tofauti kuhusu kufunga. Mfano:
• Wakatoliki hufunga kipindi cha Kwaresima (Lent).
• Waprotestanti wengi hufunga kwa namna zao binafsi.
• Waorthodoksi wana vipindi vya kufunga mara kadhaa kwa mwaka.
4. Uongozi wa Roho Mtakatifu – Wakristo wanahimizwa kufunga kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, si kwa sheria ngumu.
Uko mkoa gani?Hivi sasa ni saa 11:25 alfajiri,naruhusiwa kudakua au nimechelewa?
Hakuna ubaya wowote kwenye hiloMaaskofu wenu, wachungaji na maparoko wakialikwa iftaaaaaari ikulu au kwa kiongozi yoyote wa mkoa au wilaya au kwa tajiri fulani wanakuwa wakwanza kuwahi nafasi kuwashinda hata hao waislamu waliofunga na mkitaka ushahidi wa picha naweka!.
Wanakula Milo mitatu usiku wanakuonea wivu wewe unayekula mmoja mchanaUpande ule sasa, ni pata shika nguo kuchanika!
Mimi nashangaa watu kula Milo mitatu usikuNyinyi huwa mnatafuta nini kwenda kuwachungulia na kuwapeleleza waislamu wanavyofuturu?!
Si muangalie mambo ya ugalatia wenu ?!
Kwanini mfatilie futari na daku za waislamu?! Kama sio umbea na viherehere ni nini?!
Ukweli usemwe sisi wanaofunga ni chini ya 5%. Sio kwamba hatuna mbwembwe ukweli ni kuwa wengi wetu hatufungi.Binafsi nimeguswa na funga ya wakristo wa madhehebu yote yanayofunga kipindi hiki Cha kwaresma,Funga yenu haina kelele Wala majisifu.
Sijasikia mkristo yeyote akijisifu utakatifu Kwa kufunga kwake.
Sijaona wakristo wakizuia wengine kula hadharani Wala kuonesha kuchukizwa na Hilo
Sijaona wakristo wakihangaika na vikombe vya uji Wala sahani za magimbi muda wa kufuturu.
Sijasikia wakristo wakipiga kelele alfajiri kwamba wanakula chakula Ili waweze kuvumilia njaa ya mchana kutwa Hadi muda wa kufuturu.
Sijaona vijana wa kikristo wakihangaika kwenda kula chakula kanisani kipindi hiki Cha mfungo wao.
Nimechunguza mengi Kwa wakristo na nimegundua wanafanya mambo Yao kiungwana bila kubugudhi wengine.
Nimeambiwa wakristo wanafunga siku arobaini na mwisho wa kula au kunywa ni saa 5 dakika 59 usiku baada ya hapo mkristo hatakiwi kula Wala kunywa ila wanaruhusiwa kusafisha kinywa Kwa mswaki na maji,na kuoga pia.
Hongera sana wakristo,BWANA wenu awabariki nyote katika mfungo wenu na iweni na kwaresma njema
Kulinganisha haina maana ya kulazimisha kufanana,Allaah ametuagiza tuwaambieni hivi :
"{ قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡكَٰفِرُونَ }
Sema: Enyi makafiri!
{ لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ }
Siabudu mnacho kiabudu;
{ وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ }
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
{ وَلَآ أَنَا۠ عَابِدٞ مَّا عَبَدتُّمۡ }
Wala sitaabudu mnacho abudu.
{ وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ }
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
{ لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِيَ دِينِ }
NYINYI MNA DINI YENU NA MIMI NINA DINI YANGU. .
--mwisho wa kunukuu--
Kwanini mnataka tufanane?!
Nyinyi mna dini yenu na sisi tuna dini yetu!
Nyinyi mna ibada zenu na sisi tuna ibada zetu!
Nyinyi mna sala zenu na sisi tuna swala zetu!
Nyinyi mna zaka na sadaka zenu na sisi tuna zaka na swadaqa zetu!
Nyinyi mna funga zenu na sisi tuna swaumu zetu!
Nyinyi mna hija zenu na sisi tuna hija na Umra zetu!
Msilazimishe tufanane wakati dini zetu ni tafauti na hivyo swala zetu haziwezi kufanana na sala zenu!
Zaka na swadaqa zetu haziwezi fanana na zaka na sadaka zenu!
Swaumu zetu haziwezi fanana na funga zenu?
Hija zetu haziwezi fanana na hija zenu!.
Sisi tunafanya ibada kulingana na tulivyofundishwa na mtume صلى الله عليه وآله وسلم wala hatuigi dini ya mtu yeyote kwa sababu
NYINYI MNA DINI YENU NA SISI TUNA DINI YETU katu! Ibada za kiislamu haziwezi fanana na ibada za dini yoyote nyingine.
Sasa kama mnaona nyinyi ndio mnafunga sawasawa endeleeni hivyohivyo na sisi tunafunga kulingana na tulivyofundishwa na mtume wetu
صلى الله عليه وآله وسلم.
Lakini mwisho nawauliza tena swali ambalo hamtaki kulijibu.
Yesu alifunga siku arobaini usiku na mchana!
Nyinyi ni shetani gani aliwafindisha kufunga mchana na kula usiku?!
Andiko la kuruhusiwa kula usiku mumefundishwa na nani?!
Kwanini mnashindwa kumuiga bwana yesu au imani zenu ni ndogo ?!
Hiyo inaitwa socializationMaaskofu wenu, wachungaji na maparoko wakialikwa iftaaaaaari ikulu au kwa kiongozi yoyote wa mkoa au wilaya au kwa tajiri fulani wanakuwa wakwanza kuwahi nafasi kuwashinda hata hao waislamu waliofunga na mkitaka ushahidi wa picha naweka!.
kila mtu ashinde mechi zake BOSS
We mwenyewe hapo unakubari huu mwenzi wa ramadhani unauona kabisa huu ni mwenzi wa ramadhani 7bu unaona kila MUISLAM anafunga katika kutaka kupata AFYA na MSAMAHA kwa mola wake
ipo hivyo
Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app