Binafsi ninaamini pamoja na Mapungufu Hayati Magufuli bado atabaki rais bora kiutendaji na kiuzalendo

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Hayati Magufuli alituchukia sana wapinzani ,kwake yeye aliamini wapinzani ndio wanarudisha nyuma Maendeleo na ni vibaraka wa Mabeberu.

Kwake yeye lolote litakalo mkuta mpinzani awe ana husika nalo au hausiki nalo ni halali yake na hawezi shughulika nalo .

Hilo ndilo lilikuwa tatizo kubwa lakini kiuhalisia aliipenda Nchi na Kaifanyia mengi .

Alijisemea mwenyewe akumbukwe kwa mema .
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Kama mwamba Tundu lissu anamkubali Jpm hafu utasikia wazalendo wa pale sinza hawamkubali ni ajabu
 
Pamoja na mapungufu yake lakini Magu alifanya maendeleo makubwa na yanaonekana..!! “Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni”
 
Safi. Hizo wanazotengeneza ni propaganda za kijinga tu kumchafua. Kinachosikitisha zaidi ni serikali kukaa kimya bila hata ya kufungia kitabu kile. Kama magufuli angelijua mapema kwamba anamsaidizi wa namna hii angemwondoa haraka sana
 
Safi sana mlinda legacy
 
Pale ndio alikosea sana. Angekomaa na Dr Hussein Mwinyi kumchagua kama makamu wake nchi ingeendela kunyooka na taarifa kutoka ikulu zisingevuja kila siku kama ilivyokuwa.
 
Achievements are not measured in words shehe. Maguli alikuwa anajipigua promo tu lamini alikuwa galasa kwa vitendo. Alichojua sana ni kuua tu na kumaliza upinzani kibabe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…