Jana katika ziara ya Mhe. Rais katika Wilaya ya Itilima Mhe. Mpina Mbunge wa Kisesa alipewa muda kusema machache kuhusu Jimbo lake la Kisesa. Mhe. Mpina alisema kero za Jimbo lake likiwemo kwa nini mnunuzi wa pamba anakuwa ni mmoja katika kila Wilaya jambo ambalo ni la msingi.
Pia Mhe. Mpina aligusia tatizo la uvamizi wa tembo na pia aliomba Kituo cha Afya cha mwandoya kiwe hospitali kamili. Hapo kuna ubaya gani. Kusema kuwa Mhe. Rais anadaiwa na Wananchi wa Kisesa kuna ubaya gani. Mhe. Rais ni Mama, Baba, Mzazi wa kila Mtanzania hivyo Mpina kusema anadaiwa siyo kitu cha ajabu.
Mhe. Mpina katika hitimisho lake alimsifisia Mhe. Rais kwa usimamizi mzuri wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile SGR, Bwawa la Mwalimu Nyerere na miradi mingine mikubwa. Hapa kuna mbaya gani. Baadaye Mhe. Waziri Kilimo anakuja kumponda mbele ya Mhe. Rais. Hii inaonyesha chuki ya waziwazi. Mawaziri wanatakiwa wapendane na jambo kama lile wangeitana pembeni na kuzungumza kwa pamoja na jambo linaisha.
Kumsema vibaya Mhe. Mpina mbele ya wapiga kura wake ni jambo linalokatisha tamaa.
Binafsi sijaona kibaya alichosema Mhe. Mpina. Tunatakiwa tupendane Watanzania wote.