Binamu Bananga: CHADEMA tunakutana kujadili mahojiano ya Rais Samia na BBC ili kujibu nini? Nasisitiza tusikurupuke

Nje ya siasa Ali Bananga ana shughuli gani inayomuingizia kipato? Anayoyasema siku hizi unaweza husiamini kama alikuwa kwenye timu ya kampeni ya Lissu! Uhalisia Bananga ana kinyongo kwasababu ya ubunge feki wa mkewe.
Acheni kuchunguza maisha ya watu.

Muwe mnajibu hoja kwenye mjadala husika. Ukitaka habari za kipato cha bananga kafungue uzi wake tutakuja kukueleza huko
 
Bananga mumewe Msando kapata UDC sasa upweke unamfanya ahangaike
 
Mkuu, wahalafu inabidi waendelee kukamatwa tu. Na Bora wakamatwe maana hawa wanafanya matukio na kujificha kwenye mgongo wa Chadema.

Wanakichafua chama hivyo wahuni wote waendelee kukamatwa tu
Uhuni gani wanafanya? Na kama wanakichafua chama chao wewe usie mwanachama inakuhusu nini?
Kumkamata mtu kwa kuwa ana mawazo tofauti na yako sio sahihi. Kumkamata mtu kwa sababu unaona hakuheshimu sio sahihi. Hatuna mahabusu za kutosha lakini tunajaza watu ambao kosa pekee walilofanya ni kushika bango usilolipenda? Hiyo ni haki kweli?

Amandla...
 
Mkuu, mimi na wewe hatuwezi jua ila Jeshi letu la polisi na intelijensia yake wanajua na wanazo taarifa nying sana za ki-intelijensia. Tuwaache wafanye kazi zao na mahakama zetu zitathibitisha au kutupia mbali madai ya polisi.

Tukiamini jeshu letu la polisi na system zetu za ulinzi na usalama wa nchi yetu.

Kuhusu Chadema inanihusu maana wao ni chama kikuu cha upinzani na kinasaidiana na serikali kujenga nchi hivyo kikiwa na weledi na kikiwa katika njia nyoofu tunafaidika sote kama taifa. Ila kikiwa na wahuni kama Mdude na wenziwe hasara ni kwetu sote.

Unadhani Sisi wengine hatujawachangia viongozi mbali mbali wa Chadema watoke magerezani ili waje wasaidie kujenga Tanzania yetu??
 
Je Bananga amepiga kwenye mshono? Mbona hawajibu hoja zaidi ya matusi? Inawezekanaje makamu mwenyekiti aongoze chama cha siasa kupitia mtandao wa Twitter? Yaani sie tupambane na polisi yeye yupo Europe anakula mkate wa kumimina?
Eti tugomee kula hotelini na kununua maji, hizi ndio sera za Upinzani kuweza kuchukua dola kweli? Ni kweli kabisa hiki chama kitapata hata wabunge watatu 2025?
Mchakato wa katiba mpya ni nani aliuharibu na kukimbia bungeni? Yaani hoja moja ya muungano ndio ivunje mchakato mzima wa katiba? Niseme ukweli tu, RIP Chadema.
 
kwa hiyo mnataka akubaliane na ile kauli ya yule jamaa aliyeko Canada watu wasusie bidhaa na huduma eti serikali ikose mapato..

Hilo la Lema linatosha kabisa kuona upumbavu mwingi kwa watu eti tunawategemea ni chama mbadala na tuwape dola...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…