Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,992
- 22,396
Mkuu mnaanza kufukuza watu kwa kusema kweli??Afukuzwe yeye na mke wake haraka arudi CCM
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu mnaanza kufukuza watu kwa kusema kweli??Afukuzwe yeye na mke wake haraka arudi CCM
Chadema ni Mbowe hahahahaahTangu Mbowe ametekwa na vibaka wa Simon Sirro, sijawahi kusikia tena kuhusu Makongamano ya Katiba Mpya
Tunaendelea kusisitiza kwamba hoja zijibiwe kwa hojaAnalishwa na mke hana kazi,mke ni kundi la covid 19 lazima atetee....anajua bila huo ubunge wangekua sombetini wanapika vitumbua na mkewe
Wananuna na kutaka kufukuza watu uanachamaChadema bila Mbowe wanabaki weupe kama theluji. Sijui kwa nni Mbowe hajaandaa mtu mwenye spirit ya kupambana kama yeye. Waliobaki wote wamebaki wapiga kelele mitandaoni. Na wakiambiwa ukweli wanaishia kununa nuna
Wanasema Mama aingilie kati kesi ya Mbowe lakini ya Sabaya iendelee hahahahahahaSubiri mahakama iamue, simnasema mahakama ziwe huru
Acheni kuchunguza maisha ya watu.Nje ya siasa Ali Bananga ana shughuli gani inayomuingizia kipato? Anayoyasema siku hizi unaweza husiamini kama alikuwa kwenye timu ya kampeni ya Lissu! Uhalisia Bananga ana kinyongo kwasababu ya ubunge feki wa mkewe.
Bananga mumewe Msando kapata UDC sasa upweke unamfanya ahangaikeUshauri aliotoa Binamu Bananga kwa CHADEMA kuhusu Mahojiano ya Rais Samia na BBC
Makamanda habari za jioni? Naamini wengi tumesikiliza mahojiano ya mama Samia na Kikeke, Nimeona Kaka yangu Lema ameandika Mahali kwamba Chama Kitakutana kumjibu, nimeshtuka kidogo, tunataka kujibu nini? Mimi naendelea kusisitiza tusikurupuke.
Najua mtasema natetea CCM kwasababau ya Ubunge wa Hawa, lakini mimi nashauri kwasababu ya mapenzi yangu kwa CHADEMA, Mama Samia kasema kuna Uhuru wa Habari, Baada ya Uchaguzi tujenge Nchi, Kesi ya Mbowe ilikuwepo lakini upelelezi haukuwa umekamilika, pengine ndio sababu ya Mwenyekiti kuwa nje.
Kati ya hayo aliyosema lipi la uongo? Kuna Vyombo vya Habari vilivyofungiwa Tanzania? Hapana. Wote humu tunajua kwamba ni kweli kesi ya Mbowe ilikuwepo, sio ya sasa, amesema uongo hapo? Hapana. Kuhusu hili la kujenga Nchi sisi CHADEMA ndio tunalichelewesha kwa migogoro isiyoisha. Sasa kama ukweli ni huu, tunataka kumjibu nini?
Imekuwa ni kawaida sana kwa Chama chetu kucheza ngoma ya CCM, Hivi kweli leo sisi CHADEMA ndio wakutaka Rais aingilie uhuru wa mahakama? Tatizo tulilolipigia kelele enzi za Mwendazake, tunataka lirudi tena, Tumehubiri Utawala wa Sheria na Uhuru wa Mahakama kwa miaka 6 halafu ndani ya miezi minne ya Samia tunataka kubadili gia angani kwa kushinikiza huyu Mama kuingilia Mahakama?
Maamuzi ya Mahakama hayapaswi kuingiliwa na Rais, Mama Samia kasema Issue ya Mwenyekiti ipo mahakamani, hawezi kuiingilia Mahakama, Kauli hiyo ina shida gani? Hatuoni kama kutaka aingilie Mahakama ni kutaka avunje Katiba? Kwanini tudai katiba Mpya kwa kuvunja Katiba ya Sasa? This is not right, I am sorry guys kama nitawakwaza lakini we really need to change our think tanks.
Sio kila kitu cha kujibu, tusijichoreshe, Chama kimestuck kama Tekno, hakuna kazi nyingine zinazoendelea, CHADEMA ni MSINGI hatujui hata Documents ziko wapi, Sera mbadala ishakuwa Zilipendwa, Mwenyekiti kuwa mahabusu siku 20 Chama kimeparalaizi kabisa, Hivi kweli Siku Mbowe akitoka CHADEMA, chama kitabaki hai?
Makamu Mwenyekiti Kaka yangu Lissu toka huko Ulipo, tunakuhitaji uwanjani, Maria Space na Clubhouse ni vijiwe vya story tu, havina maajabu, Lema anasema watu wasinywe bia, wasinywe maji ya kunywa, wasile hotelini, Yaani kweli huu ndio mkakati wa Chama kikuu cha upinzani? Kama tuko serious, Tusiwe na mipango unrealistic kama huu wa kaka yangu wa Canada.
Lema unasema hayo kutokea Canada, labda nikuulize, tukigomea maji huku Tanzania ili Serikali ikose pesa, Wewe na familia yako huko Canada mtagomea nini ili Serikali ya Tanzania ikose pesa? Au nyie mtaendelea kuishi kama kawaida wakati sisi tukiisoma namba kwa kugomea Dawasco huku? Bro kaa chini ufikirie tena wazo lako.
Narudia kushauri, tuachane na press za kila siku, Kama tunataka Mbowe atoke tukubali kwamba propaganda za Twita haziwezi kubadili kilichoandikwa kwenye Hati ya Mashtaka, tuna wanasheria wazuri, wasimame na Mwenyekiti, tuache sanaa.
Yangu ni hayo kwa leo, Samahani kwa watakaokwazika. Tusipoambiana ukweli Chama kitakufa.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂Lema ni kielelezo kimojawapo kwamba chadema hawapo serious!
Anataka wananchi waache kunywa maji ilj serikali isipate pesa!
Uhuni gani wanafanya? Na kama wanakichafua chama chao wewe usie mwanachama inakuhusu nini?Mkuu, wahalafu inabidi waendelee kukamatwa tu. Na Bora wakamatwe maana hawa wanafanya matukio na kujificha kwenye mgongo wa Chadema.
Wanakichafua chama hivyo wahuni wote waendelee kukamatwa tu
Mkuu, mimi na wewe hatuwezi jua ila Jeshi letu la polisi na intelijensia yake wanajua na wanazo taarifa nying sana za ki-intelijensia. Tuwaache wafanye kazi zao na mahakama zetu zitathibitisha au kutupia mbali madai ya polisi.Uhuni gani wanafanya? Na kama wanakichafua chama chao wewe usie mwanachama inakuhusu nini?
Kumkamata mtu kwa kuwa ana mawazo tofauti na yako sio sahihi. Kumkamata mtu kwa sababu unaona hakuheshimu sio sahihi. Hatuna mahabusu za kutosha lakini tunajaza watu ambao kosa pekee walilofanya ni kushika bango usilolipenda? Hiyo ni haki kweli?
Amandla...
Mkuu, mimi na wewe hatuwezi jua ila Jeshi letu la polisi na intelijensia yake wanajua na wanazo taarifa nying sana za ki-intelijensia. Tuwaache wafanye kazi zao na mahakama zetu zitathibitisha au kutupia mbali madai ya polisi.Uhuni gani wanafanya? Na kama wanakichafua chama chao wewe usie mwanachama inakuhusu nini?
Kumkamata mtu kwa kuwa ana mawazo tofauti na yako sio sahihi. Kumkamata mtu kwa sababu unaona hakuheshimu sio sahihi. Hatuna mahabusu za kutosha lakini tunajaza watu ambao kosa pekee walilofanya ni kushika bango usilolipenda? Hiyo ni haki kweli?
Amandla...
Huyo ni CCM fullMkuu mnaanza kufukuza watu kwa kusema kweli??
Mimi najua ana kadi ya CDM lakiniHuyo ni CCM full
Kwanini hutaki muwe naye CCM?Mimi najua ana kadi ya CDM lakini
Mkuu, with all due respect Bananga ni mwanachama wa Chadema.Kwanini hutaki muwe naye CCM?