Sikio la muazini
JF-Expert Member
- Jun 17, 2026
- 262
- 519
Binamu yangu simuelewi, eleweni hivi. Nakumbuka kabla hajaolewa tulikuwa na utani wa kawaida, ila sasa kaolewa Zenji. Juzi kanunua simu akaomba namba yangu, akanipigia akisema amenimiss.
BINAMU: Jamani nimekumiss mme wangu..?
MIMI: Hata mimi nimekumiss mke wangu..!
Lakini mimi sikuwa serious, nachukulia ni utani tu. Ila nashangaa ananipigia akilalamika kwa nini yeye ndiye anitafute tu, lakini mimi simtafuti. Mimi nampotezea tu.
Juzi kasema niende Zenji nikakae kwake, atanitumia nauli. Nikampotezea tena, akapiga na kusisitiza tena kwamba atanitumia nauli. Kama vipi atanitafutia kazi nisikae bure.
Bado sijamjibu, nimemwambia nitamjibu.
Je, niende au natafuta balaa?
Mchango wenu wakuu, karibuni.