Kiraka
JF-Expert Member
- Feb 1, 2010
- 4,285
- 4,074
Ni bora kumuumiza mara moja kwa ukweli wa kuwa huna nia nae yoyote kuliko kumuumiza kila siku kwa uongo ambavyo unafanya sasa hivi.
Pale unapokuwa nae anajipa imani kuwa wewe ni mtu wake kumbe wewe unamuona hakufai. Kwa maana nyingine unamfungia njia yake ya kupata mtu atakeridhika na tattoo zake.
Ila kumbuka katika mahusiano siku zote ni bora kuwa na mtu anaekupenda zaidi kuliko wewe kumpenda yeye zaidi. Tattoo na matundu ya masikio haya define utu wa mtu. Walimwengu hawakosi la kukosoa. Utakuja kutana na mwenye matundu mawili tu ya masikio na bila tattoo ila mwili wake ushatobolewa kila sehemu na uume za watu na kuishi na hofu kila siku kama uko peke yako au laa.
Umeongea ukweli sana... Haswa sisi wanaume, tuombe sana Mungu tupate wanawake wanaotupenda kwa dhati... utaishi kwa amani.